Huwa tunakuwa nao huu Ujinga sana linapokuja suala la Waarabu na Wazungu. Wao wanatuonesha kitu...

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,363
11,519
Tena niseme afadhali na baadhi ya waswahili huwa wanaweza wakosoa vizuri tu Wazungu ukiacha wale wajinga wachache ambao nao huwa hawaoni makosa kwa wazungu.

Kuna Sisi waswahili wengine wapumbavu choka mbaya hutuambii kuhusu waarabu. Yaani hata kwenye match tukicheza nao wakitufanyia uhuni hatuzungumzii....nimeangalia matches za Simba wakienda Uarabuni...toka miaka ya 90s mpaka sasa. Jamaa hawana ubinadamu ukienda kwao.

Leo sasa Azam ambao wakiwa hapa Bongo hujiona wao ni Waarabu wameenda kukutana na waarabu wenzao huko. Nlidhani ndugu wakicheza wanakuwa na fair play. Hamna.

Kipa wa azam anamulikwa usoni na torch. Mwamuzi msaidizi anatupiwa chupa za maji. Ndani vurugu na mpira wa kibabe hasa. Hali hii nakumbuka Simba walikutana nayo pia kwenye kombe la mbuzi huko Sudan na hawa jamaa waliocheza na Sisi wananchi leo.

Yaani kwenye mpira ni bora ukakutane na wazungu uwanjani hata kwao hawana figisu kama za waarabu. Sasa najiuliza hawa ndugu zetu huwa wanatusahau? Sisi waarabu na wazungu wa Buza, Buguruni kwa Mnyamani, Tandale kwa Mtogole, Tandale kwa Tumbo, Mabibo Majimatitu na Mbagala Charambe...je huwa tunajipendekeza itusaidie nini?

Kupata tende na misaada toka kwao? Tuacheni huu upuuzi. Tuanze kujiamini tusifie na kukosoa pale inapobidi.

NIMEKAA PALE 👉
 
Back
Top Bottom