Huwa kuna burudani tamu sana CHADEMA na CCM wakikutana uwanjani.

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
611
724
Mechi kati ya hivi vyama hasa katika chaguzi ndogo huwa ni tamu sana. Nakumbuka mechi ya Igunga , Busanda, Tarime , Arumeru nk zilikuwa mechi za kukata na shoka.

Uchaguzi huu mdogo timu moja imejitoa kwa kulalamikia mazingira ya mchezo kutokuwa mazuri , hii mechi imepoa kabisa .Hakuna tena amsha amsha tuliyoizoea kwa mda mrefu.

Katika chaguzi kama hizi hapo zamani jukwaa kama hili lilichangamka kwa nyuzi nyingi za uchaguzi . Hata mzunguko wa pesa uliongezeka katika eneo husika, leo sioni tena.

Wito , nawaomba waandaji wa mechi kati ya CHADEMA na CCM warekebishe kasoro zilizopo ili sisi wananchi tufaidi mechi kali kati ya hizi timu mbili.
 
Asiyekubali kushindwa si mshindani! Timu zote mbili zimeshindwa kushindana
 
Mechi kati ya hivi vyama hasa katika chaguzi ndogo huwa ni tamu sana. Nakumbuka mechi ya Igunga , Busanda, Tarime , Arumeru nk zilikuwa mechi za kukata na shoka.

Uchaguzi huu mdogo timu moja imejitoa kwa kulalamikia mazingira ya mchezo kutokuwa mazuri , hii mechi imepoa kabisa .Hakuna tena amsha amsha tuliyoizoea kwa mda mrefu.

Katika chaguzi kama hizi hapo zamani jukwaa kama hili lilichangamka kwa nyuzi nyingi za uchaguzi . Hata mzunguko wa pesa uliongezeka katika eneo husika, leo sioni tena.

Wito , nawaomba waandaji wa mechi kati ya CHADEMA na CCM warekebishe kasoro zilizopo ili sisi wananchi tufaidi mechi kali kati ya hizi timu mbili.
Wanaoendesha na kusimamia hizi mechi wamesema hakuna kasoro zozote, kila kitu kiko sawa kama inavyotakiwa! Kwa mujibu wa wasimamizi hao,huyo atakayechukua ushindi ndiye anayependwa sana na wananchi.
 
Kwa taarifa yako ccm inajua haipendwi na imechokwa, hivyo haiko tayari kupambana kisiasa bali kutumia ubabe. Kwa hiyo usitarajie watakubali ushindani sawa kisha washindwe na kuishiwa kukejeliwa hapa jukwaani. Wako tayari hata uchaguzi upooze lakini washinde wao. Sio kwamba hawaoni aibu kwa hii hali iliyoendelea leo, lakini kwao ni bora kuliko wasimangwe. Hiyo ni kawaida kabisa ukishapitwa na wakati na bado ukawa unataka kuonekana bado umo lazima utafanya mambo ya aibu. Hujawahi kumuona mwanamke mzee anavaa vijisketi vifupi ili aonekane naye kijana? Sasa ole wako umuambie kazeeka na hapendwi na vijana atakumwagia vurugu za hatari, ndivyo ilivyo ccm.
 
Back
Top Bottom