Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Wakati fulani nikisoma shule ya Sekondari, baba alikuja kunitembelea shuleni, nikashangaa kwa nini amekuja kwa miguu na ana mavumbi mengi miguuni?

Akanikabidhi TZS 12,000/= yani 10,000/= ya kulipia hostel na 2,000/= ya matumizi. Nikamuuliza mbona leo huna baiskeli? (mara zote alikuwa akiendesha baiskeli 40kms kuja shuleni). Akanijibu "...nimekuja kwa basi", nikaamini ni kweli!
_
Miaka mitano baadaye, nikiwa Chuo Kikuu, wakati nimerudi likizo nyumbani, nikawa nimekaa nje saa za usiku mnene, niko na baba akinipigia stori za vita za Uganda, Msumbiji nk.

Ghafla akanipigia stori iliyomkuta miaka 5 iliyopita, kwamba alikuwa na shilingi 12,000 tu ndani, akapata taarifa kuwa wanafunzi wanarudishwa kwa kutolipa hela za hostel. Akafunga safari ya baiskeli kuja shuleni kwetu (alikuwa anaanza safari zake saa 8 au 9 usiku), ili kuniletea ile pesa, safari ya kilomita 40.

Alipofika kilomita 13 baiskeli ikaharibika, "tyre tube" ya nyuma ikapasuka, ikawa haifai. Akaamua kuacha baiskeli kwa wenyeji na kuanza safari ya saa nyingi kwa mguu hadi shuleni kwetu, zaidi ya kilomita 27.

Akafika ametabasamu ana furaha mno, akanikabidhi zile pesa na akaanza safari nyingine ya kilomita 27 + 13, ananiambia alifika nyumbani kesho yake.

Usiku nilipojua safari ile ya Mzee wangu nililia sana, sikulala, ilinipasa nijitafakari juu ya huyu mtu anayeitwa BABA, ambaye yuko tayari kufa na kutokwa jasho la damu kwa ajili ya familia yake.
_
Kila mwanaume 1 anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini, familia yake, hata kama hana senti tano! Uwepo wake na tabasamu na kurudi kwake, kunainong'oneza familia "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI.."
_
Hadithi ya baba yangu mzazi, inatukumbusha mwanaume anatembea na mengi sana kichwani na moyo wake, na hawezi kuyasema, kama wanaume wangelikuwa wanawaeleza wake zao namna wanavyopambana kwa ajili ya familia zao, wanawake wangelikufa kwa mshtuko.

And you know what? Baba hakuwahi kumpigia mama hii stori, hadi mimi nilipomsimulia mama.

Si ajabu ndiyo maana wanaume tunakufa mapema, maana tunauawa na mengi!
 
Shukuru Mungu kama Ulizaliwa na baba wa aina hiyo! Siyo watoto wote wana historia kama hizo na baba zao!

Sidhani kama kuna mtu anayemchukia baba yake bila sababu! Ukikuta mtu anamchukia baba yake tafuta kujua chanzo!

Na mara nyingi mtoto akimchukia baba yake lawama zote hutupiwa mama! Wamama wengi wana wakati mgumu sana!
 
Huwezi kunivua upendo kwa BABA! Nimelelewa na single dad toka na miaka miwili, nafahamu role ya baba na nafahamu namna gani maisha yanakuwa settled na baba.

Pamoja na propaganda na chuki za watu wachache kuzielekeza kwa jinsia ya kiume kipindi hiki chini ya tawi fulani bado wanakazi kubwa ya kubadili ukweli.
 
Angekuwa baba yangu hapo nisingekuwa shule muda huo. Kuna watu wengi wenye umuhimu kwangu kumzidi yeye, mtu anayekwambia mbona unanipigia sana kwani sijui kama upo unategemea maajabu gani kwake. Hapo ushamtafuta mwaka mzima hapokei sasa jichanganye umpigie kwa namba nyingine apokee atabadili gia angani kama hivi;

Mimi: Inaita
Yeye: Anapokea
Mimi: (Salamu na maelezo kwa mkupuo maana najua hatoongea sana, hela hazihusiki kabisa)
Yeye: Kumbe ni wewe, mbona namba nyingi. Simu yangu hii ina shida
Mimi: Siku nyingi hatuongei kulikoni
Yeye: Hello! mbona sikusikii
Mimi: Wazima uko
Yeye: Hello! Hello! Naona mtandao una shida, sikusikii ntakupigia nikikaa kwenye network.

Kuna siku usanii wake nikauchoka nikamtukana we mpuuzi nini kila siku mtandao unasumbua. Kesi nikaisikia kwa aunt yangu ikiwa na nyongeza ya mashtaka kwamba simpendi na natamani afe. Kazi yake kwangu ni kunifanya nisiitwe yatima, hafai hata kunipa ushauri.
 
Nimelalewa na baba yangu pekee yake, japo mauti yalimkuta mapema. Nampenda sana hadi sekunde hii japo hayupo tena ulimwenguni, hata kama sina ratiba ya kwenda nyumbani nikimkumbuka basi naenda hata kusabahi kaburi lake tu.

Wanaume wapo wenye moyo wa kipekee sana kwa watoto wao japo akina mama wanaonekana wao ndiyo mashujaa wa hili ila.basi tu sisi wanaume ni mwendo wa kupambania familia huku akina mama wakisaka haki sawa.
 
Angekuwa baba yangu hapo nisingekuwa shule muda huo. Kuna watu wengi wenye umuhimu kwangu kumzidi yeye, mtu anayekwambia mbona unanipigia sana kwani sijui kama upo unategemea maajabu gani kwake. Hapo ushamtafuta mwaka mzima hapokei sasa jichanganye umpigie kwa namba nyingine apokee atabadili gia angani kama hivi;

Mimi: Inaita
Yeye: Anapokea
Mimi: (Salamu na maelezo kwa mkupuo maana najua hatoongea sana, hela hazihusiki kabisa)
Yeye: Kumbe ni wewe, mbona namba nyingi. Simu yangu hii ina shida
Mimi: Siku nyingi hatuongei kulikoni
Yeye: Hello! mbona sikusikii
Mimi: Wazima uko
Yeye: Hello! Hello! Naona mtandao una shida, sikusikii ntakupigia nikikaa kwenye network.

Kuna siku usanii wake nikauchoka nikamtukana we mpuuzi nini kila siku mtandao unasumbua. Kesi nikaisikia kwa aunt yangu ikiwa na nyongeza ya mashtaka kwamba simpendi na natamani afe. Kazi yake kwangu ni kunifanya nisiitwe yatima, hafai hata kunipa ushauri.
Exactly the same story .
Mshua wangu alitengana na bimkubwa kitambo sana Kabla ya kuzaliwa kwangu. Kusoma kwangu,kula na kuvaa ni mama mpaka nimemaliza chuo.kiukweli huwa najiuliza hata kama walitofautiana na mama basi angenionyesha ule upendo basi kama baba yangu lakini wapi .hali hiyo ya kukosa upendo wa baba imeniathiri kisaikolojia hadi sasa . Najiuliza kwanini asingenionyesha upendo hata basi wa kinafiki. Kwa kweli nikikumbuka maisha haya niliyoyapitia nasema anyway ...
 
Angekuwa baba yangu hapo nisingekuwa shule muda huo. Kuna watu wengi wenye umuhimu kwangu kumzidi yeye, mtu anayekwambia mbona unanipigia sana kwani sijui kama upo unategemea maajabu gani kwake. Hapo ushamtafuta mwaka mzima hapokei sasa jichanganye umpigie kwa namba nyingine apokee atabadili gia angani kama hivi;

Mimi: Inaita
Yeye: Anapokea
Mimi: (Salamu na maelezo kwa mkupuo maana najua hatoongea sana, hela hazihusiki kabisa)
Yeye: Kumbe ni wewe, mbona namba nyingi. Simu yangu hii ina shida
Mimi: Siku nyingi hatuongei kulikoni
Yeye: Hello! mbona sikusikii
Mimi: Wazima uko
Yeye: Hello! Hello! Naona mtandao una shida, sikusikii ntakupigia nikikaa kwenye network.

Kuna siku usanii wake nikauchoka nikamtukana we mpuuzi nini kila siku mtandao unasumbua. Kesi nikaisikia kwa aunt yangu ikiwa na nyongeza ya mashtaka kwamba simpendi na natamani afe. Kazi yake kwangu ni kunifanya nisiitwe yatima, hafai hata kunipa ushauri.
Duh!!!
 
Back
Top Bottom