Huu Ubunifu wa Roma Mkatoliki kila aingiapo Stejini hautakuwa na madhara baadae?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,176
Nimemfuatilia katika Shows zake karibia zote za Tigo Fiesta na kugundua kwamba mara nyingi huingia Ukumbini au pale Stejini akiwa na mienokano ya aina hii:
  1. Kabebwa katika Wheelchair
  2. Kakunja mkono kama amewekewa hogo
  3. Kafunga bandeji Kichwani
  4. Anachechemea kama Mtu aliyeumizwa
  5. Mikono yake imefungwa nyuma
  6. Kashika mnyororo mkubwa
  7. Kashika Fimbo
Je hii haitokuja kuwa na madhara makubwa labda Kwake kwa siku za baadae? Na je kwa kufanya hivi anajaribu kutuma Ujumbe gani katika Jamii na kwa wale waliomteka na kumtesa hadi kumtupa Ununio mkabala na Mahaba beach? Je kama kweli Roma Mkatoliki anajambo linamtatiza moyoni na anataka kuwaambia / kuwahabarisha Watanzania na Wapenzi wake kwa ujumla basi kwanini asiitishe tu Press Conference ili atiririke na aserereke vizuri kuliko kila siku kufumbafumba kupitia Jukwaa la Tigo Fiesta?

Ushauri

Kwa aliye karibu na Roma Mkatoliki ajaribu kumsaidia Kisaikolojia kwani naona bado hayuko vizuri na kwamba pengine Yeye anaweza kudhani amemaliza Kazi ila yawezekana kabisa wabaya wake wanamtathmini na labda wanaweza wakija mara ya pili asitupwe tena Ununio na badala yake tukamuokota pembezoni mwa Fukwe zetu akiwa ndani ya Sandarusi na Jiwe juu. Afanye tu Mziki na aache masuala ya harakati kwani nina uhakika hayawezi na yatamgharimu na kuja Kujuta.

Ni Msanii mzuri sana hata Mimi namkubali na nampenda ila nahisi kama vile ama anatumika bila Yeye kujua au ana agenda fulani ambayo labda anahisi itafanakiwa japo Mimi kila nikipima kwa macho yangu ya kuona mbali zaidi naona ni kama tu anapaka rangi upepo.

Yangu ni hayo tu Wadau.

Nawasilisha.
 
Mtoa post inaonekana hujui hata nini maana ya sanaa (Fasihi), ina mbwembwe zake za uwasilishwaji. Roma yuko sahihi kabisa na ndiyo sababu humuoni wa kuitisha press conf kumjibu.
 
Roma ana kiherehere sana ni bora anyanyuke na aseme kilichompata....kuliko kujificha nyuma ya maigizo....hata mwenzie waliotekwa nae aliwai kusema kuwa msanii mwenzie ni mnafiki......na wanafiki hutumia mafumbo sana....
Roma anatumikia chadema na muziki....
 
Roma ana kiherehere sana ni bora anyanyuke na aseme kilichompata....kuliko kujificha nyuma ya maigizo....hata mwenzie waliotekwa nae aliwai kusema kuwa msanii mwenzie ni mnafiki......na wanafiki hutumia mafumbo sana....
Roma anatumikia chadema na muziki....
Ulitaka atumikie ccm?
hapo ndo ungekenua mpaka jino la mwisho tulione!!
Kwani kutumikia chadema dhambi?
 
Bado sijaona kosa la Roma, yule ni msanii anaruhusiwa kubuni chochote katika kutuma ujumbe fulani kwa jamii, na uzuri yy ni miongoni mwa watekwaji basi tumuache ajiachie na sanaa yake.
 
Back
Top Bottom