KAKADO
JF-Expert Member
- Nov 8, 2012
- 230
- 336
Mapema siku juma tatu msanii wa miondoko ya kufokafoka Roma mkatoliki alitimiza ahadi aliyohiahidi ya kukutana na wana habari katika muktadha wakuweka wazi mambo kadhaa wa kadhaa yaliyomsibu wakati akiwa mateka..
Roma mkatoliki ambaye alikuwa mateka kwa siku kadhaa aliibuka,siku ya jumamosi na kuongea na waandishi wa habari kwa ufupi Kisha akaahidi jumatatu ataweka wazi yote yaliyomsibu.
Binafsi nilifanikiwa kumsikiliza mambo yote aliyoyaongea,tutafanya uchambuzi wa kina dhidi ya kauli zake utakao husisha nukuu ya kauli zake lengo hasa ni kuwa na strong argument juu ya hoja yake anayokiri aetekwa na sio kujiteka kama wengine wanavyo Dhani.
Twende kazi
Roma anaanza kuonyesha sehemu ya ndani ya mdomo alipojeruhiwa na watekaji,Roma anasema "tukio lilitokea siku ya jumatano ilikuwa majira ya saaaa,jioni saa 11 kwenda saa 12 jioni pale pale Tongwe record nilifika pale kwa ajili yakufanya shughuli zangu,nilipofika nilimkuta moni,bin Laden pamoja na imma tulikuwapo pale,wakati naendelea na shughuli zangu,haikupita hata muda wa nusu saa,walikuja watu ambao hatukuweza kuwafahamu,mbaya zaidi walikuwa na silaha za moto na amri yao yakwanza ilikuwa ingieni ndani ya gari mara baada yakuingia ndani ya gari nakumbuka hawa watu walinifunga usoni wakatuamuru tulalee chini kwa hoja ya kwamba inama chini usiinuke huku wameshika silaha za moto,hofu yetu ikatufanya tukainama chini na gari ikawashwa kuondoka maeneo ya studio na kuelekea ambako sisi hatukupajua"
Maneno haya machache ya Roma mkatoliki tunaweza tukayalinganisha na shahidi namba moja(the city) ambae nae alikuwapo eneo la tukio watu hawa wakiwa wanatekwa.
The city (shuhuda namba moja)anasema
"ilikuja Noah nyeupe na wakashuka watu watatu,baada ya hapo wakatuamrisha mimi,bin Laden na wageni kutoka morogoro tuingie ndani ya geti,tulipoingia ndani ya geti walituuliza kwamba tumemkuta junior au tumemkuta Roma,tukasema junior hayupo ila Roma yupo ndani,wakatuamrisha Tukamuite Roma,tukamuita Roma,Roma akatoka akaulizwa wewe ndio ROMA na ilivyoonekana hawakumjua na pia walimuambia simu yake ipo wapi atokenayo Roma alitokanao sikuweza kujua nini kiliendelea kwa sababu waliongelea nnje ya gari,walirudi ndani wakamlazimisha binladen aingie studio akiwa amesindikizwa na mmoja wao na Wakarudi tena wakachukua TV zilizopo pale,wakatoka na imma walikuwepo wote ndani ya studio,studio ikabaki tupu,walivyotoka hapo wakaniambia mimi na wageni wengine waliotoka morogoro tusiende popote na nilichosikia baada ya hapo ni mshindo wa gari na gari kuondoka "
Shuhuda ( the city)na watekwaji wapishana maelezo Roma anasema baada ya gari kuwasili amri ya kwanza waliamrishwa kuingia ndani ya gari nae shuhuda anasema baada ya gari kufika waliamriwa waingie ndani ya geti na watekaji wakaulizwa wamemkuta junior au Roma.
Uchambuzi.
kauli ya Roma na shuhuda imetofautiana kana kwamba huenda nimatukio mawili yanazungumziwa,shuhuda hakugusia kabisaa kuhusu kujificha sura kwa watekaji kitu ambacho ilikuwa rahisi mno kutamka Kama kweli tukio hili lilifanyika na watekaji walificha sura. Zao
Eheeeh tuendelee kunukuu maelezo ya Roma wakati akijibu swali la mwandishi wa mwanannchi,Roma anasema "nilikuwa nimevaa white,nilikuwa mchafu sana nilitapakaa damu,nilikuwa na madoa sana ya damu,ikawa gari likitumulika tunahofu,ikawa ikitokea gari tunajificha tulitembea mpaka kunduchi.
Uchambuzi:
Kwa kauli ya Roma anaskika akisema alikuwa mchafu sana nguo zake nyeupe zililowa damu,hali hiii ilipelekea mateka wenzake kutembea kwakumficha swali lakujiuliza je? nimajeraha yapi aliyonayo yaliyo pelekea kulowesha mavazi yake kwa damu??au watekaji walikuja na damu yao wakamwagia nguo za Roma??
Roma anaendelea anasema "Baadaye tukaanza kutembea usiku ule umbali mrefu mpaka tukakuta kibao kimeandikwa ununio,tuliomba boda boda tupande mskaki wawili wawili,walikubali tukapanda bodaboda tukaenda hadi mbezi,mm naishi mbezi kuingia ndani familia hamna,hii ilikuwa pigo jingine kwasababu sikujua ilipo familia yangu "
Uchambuzi.
Roma alifika nyumbani hakuikuta familia lakini aliweza kuingia ndani je nani alimfungulia mlango usiku huo??na kama alivunja mlango kwa hali zao za maumivu na mateso waliyotoka kuyapata ni kweli walikuwa na nguvu yakuvunja mlango?ni moja ya chambuzi nzuri inayoweza kutupa picha Kamili kama tukipata ufafanuzi mzuri kutoka Kwa watekwaji.
Afya ya Roma
Roma alizungumza na wana habari kwa kifupi sana siku ya jumamosi ambapo aliahidi kuzungumza tena siku ya jumatatu huku akiomba apewe muda mwingi wakupumzika,baada ya mapumziko ya takribani saa 30 jumatatu ikafika na Roma akatokeza tena mbele ya waandishi wa habari mbaya zaidi hali yake yakiafya ikaonekana mbaya zaidi ukilinganisha na alivyozungumza na wana habari siku ya jumamosi,Roma alionekana kujikaza sana na mtu anayepata maumivu makali kitu ambacho kinaashiria hayupo sawa.
Huenda swala hili linausani na userious ndani yake hatupaswi kuwapuuza na kuwakebehi kwa asilimia miamoja na vilevile hatupaswi kukubaliana nao kwa asilimia zote miamoja,tunapaswa kuwa wavumilivu kusubiri upelelezi ukamilike tutajua ukweli upo wapi,yapo maeneo machache upelelezi ukifika huko hakika lazima ukweli ujuliKane,tuwe wavumilivu upelelezi ukiwa tayari napo tutaweka mezani tutaonganisha dot tutafanya uchambuzi yakinifu.
My take:kwa sasa mateka wote wanapaswa kupewa matibabu yakisaikolojia ,wote kwa pamoja wanaonekana hawapo sawa kiakili embu vuta picha vijana wameathirika kiasi wakiona mwanga wa gari wanakimbia,wanakuwa na hisia zakutekwa unaweza usielewe sana waswahili wanasema unapoumwa na nyota Jani linapokugusa lazima utashtuka.hali yao yakisaikolojia haipo salama wanaitaji matibabu ya kurudisha imani juu ya mwanga hata huyu mwenzao tunaambiwa anapiga kelele sana usiku huenda ni mwanga wa taa(balbu)unamsumbua TUSIWAPUUZE tutibu saikolojia yao.