Roma Mkatoliki na Waziri Mwakyembe waongea na waandishi wa habari

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,279
Roma Mkatoliki na wasanii wenzake kuongea na waandishi wa habari leo saa nane mchana katika Ukumbi wa Habari Maelezo, Posta Mpya, Dar.
==========

UPDATES


tmp_16514-IMG_20170410_1536492014051655.jpg


Mwakyembe akiongea na kujibu maswali ya waandishi



Anaeongea kwa sasa ni msanii Roma na anatoa shukrani kwa wote bila kujali itikadi zao, anasema kilichowapata watu wafanye kama case study.

Roma anasema hawana uhakika wa usalama wao hata kidogo, amesema nature ya tukio, studio zilizopo Tongwe records yuko tangu 2007 na ni eneo salama sana. Amesema wana majirani wanaowapa amani sana ikiwemo ujirani na Tibaigana, Waitara na mstaafu mmoja wa Magereza.

Amesema hofu hiyo isiishie kwao kwani inaweza ikarudi kwa yeyote muda wowote, mtu yeyote inaweza kumkuta. Amedai wao ni wachanga mno na hawawezi kupambana na yeyote. Anasema Bin Laden hayuko sawa na anastuka sana mpaka kuwastua watu wote.

Amedai kuna watu wanaamini hakuna kilichotokea kwa kudhani ni kiki na wengine wanasema wanatumika kisiasa labda kuchafua serikali.

ROMA: Tunatafuta ruzuku yetu kupitia mziki, tumelia sana kwa haya maneno tena mengine kutoka kwa watu wa karibu sana ikiwemo wanamuziki, si kweli. Tunaishi familia za kawaida na hatuwezi kurisk maisha yetu kwa ajili ya hela au sababu nyingine yeyote.

Kilichotokea ni kweli, nadhani mnaona mwili wangu(anaonyesha), linatuumiza sana mtu kusema tumepewa dola 5,000. Tumeumia, tumepigwa kiukweli na tumeripoti kwenye vyombo vya dola.

Sheria zetu zinasema jambo likianza uchunguzi ni njema kulielezea kwani wanasema linaharibu upelelezi.

Nilifika Tongwe na kuwakuta wenzangu, haikupita nusu saa wakaja watu na silaha za moto na amri ilikuwa kuingia ndani ya gari, tukiwa tumefungwa usoni na pingu, ilikuwa Jumatano jioni na tumekuja kupata usalama tumekuja kuupata Ijumaa jioni na kulikuwa na mahojiano yanaendelea yakiambatana na vipigo. Maojiano hayo ndo hayo temsharipoti.

Tulifungwa tena na kuachwa eneo ambalo hatulijui tukatupwa kwenye dimbwi la maji, tukajikuta tuko salama na baada ya kutembea sana tukakuta kibao kimeandikwa Mahaba beach na kugundua tulikuwa Ununio.

Swali: Mlingundua mlitupwa beach, mlienda beach Oysterbay police

JIBU: Ilikuwa ni usiku, baada ya muda tulipogundua Ununio, nilikuwa na madoa ya damu. Mpaka mtu ujue mimi ni Roma ilikuwa ngumu, tulifika hadi Kunduchi na kukuta boda sita na kumuomba Moni aite boda, tukaenda hadi nyumbani Mbezi, kuingia ndani hamna mtu, nikawaambia wenzangu tubadili nguo, ilikuwa inaelekea Alfajiri, mtu wa bajaji tukamuomba simu kumpigia bosi wetu.

Tulipofika alikuwa tayari amempigia Ruge Mutahaba, walikuwepo na waliumia sana, wao ndio wakatupa way forward na kusema walifungua hii kesi kituo cha polisi hivyo tukaenda kituo cha polisi Oysterbay.

SWALI: Waliwaachia masharti yoyote

JIBU: Ipo ndani ya upelelezi.

SWALI:Chanzo kilikuwa mziki wako?

JIBU: Siwezi kujua, upelelezi unaweza kuleta majibu.

Dada anaeonekana muongozaji anasema hamna swali jingine na anamkaribisha waziri Mwakyembe.

Mwakyembe: Pale ambapo kuna tatizo na msanii yeyote nitaarifiwe kwanza mimi waziri mwenye dhamana, wasanii wote ukihojiwa na mtu usiemjua wa ajabu nitafute, niliposikia taarifa hii nikajiuliza chombo cha dola kimekiuka tena taarifa yangu? Hili ni swala scientific tuache kupiga ramli, wenzetu wamesema tuwaache wafanye upelelezi, hii sio hali ya kawaida

Inaweza kuwepo wasanii(sio wanamuziki) wachache wanataka kutuvuruga, nawashukuru sana.

SWALI: Bashe amesema vyombo vya usalama vimehusika

JIBU: Umeleta maswala ya kina Bashe, mimi hapa Mwakyembe, mambo hayo yako bungeni.

Swali: Kuna mtu alisema Roma ataonekana kabla ya Jumapili na kweli akaonekana

Moderator: Sasa tuishie hapohapo.

Mwakyembe: Mkiendelea kupiga kelele kama watoto wa shule naondoka hapa, wewe unaamini ni vyombo vya dola? Siwezi kuamini mpaka nione ya recording ya huyo kiongozi.

========

Waandishi wa habari tupo njiani kuelekea ukumbi wa Posta Mpya.

Waandishi wa habari tumeshafika ukumbini.

Ujumbe ambao tumepata Waziri wa Habari na Utamaduni na michezo Mwakyembe ataongea na waandishi wa habari muda mfupi ujao ndani ukumbi ambao tumeambiwa Roma ataongea na waandishi wa habari.

Msanii Roma Mkatoliki pamoja na wenzake bado hawajafika ukumbini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Mwakyembe akiwasili katika ukumbi wa Habari- MAELEZO kuzungumza na waandishi wa habari.

Waandishi wa habari tulijua Press conference itakuwa ya Roma pamoja na management yake,Lakini Waziri wa Habari na Utamaduni na michezo Mwakyembe ameshafika ukumbini.

Mpaka muda huu 14.44 bado msanii Roma Mkatoliki na wenzake hajafika ukumbini ambaye yupo ukumbini muda Waziri wa Habari na Utamaduni na michezo Mwakyembe.

PICHA Wanahabari wakisubiri mkutano wa msanii Roma Mkatoliki katika ukumbi wa Habari Maelezo, anayesubiriwa ni Waziri Dkt. Mwakyembe.

Muda mfupi ujao tutakuletea mkutano wa moja kwa moja kutoka ukumbi wa habari maelezo, msanii Roma Mkatoliki anatarajia kuzungumzia na waandishi wa habari.
Msanii Roma Mkatoliki pamoja na wenzake bado hawajafika ukumbini muda huu saa 15.26 !!!

Msanii Roma Mkatoliki akiwa na Waziri wa Habari na Utamaduni na michezo Mwakyembe wameshaingia ukumbini muda mkutano unaanza.
 
Ni heri Roma akae kimya kuzungumza lolote maana akisema jambo kuna hatari ya kuacha mianya ya maswali mengi maana tayari ishu ishaanza kuonekana kama ni movie ya kihindi picha inaanza starring anakufa kwenye maua...ngumi inapigwa inalia kama dufu la daku! Loh! Sometimes wanasema even silence is an answer!

And sometimes your weakness can be your strength...! Kwamba ukimya wako ambao watu wanaweza uona kama weakness yako unaweza kuwa ndo uimara wako kwa kukaa kimya na kuacha watu watafsiri wanavyojua maana kwa sasa tayari hata ukumbi wako tu wa press unajizungumza kwa namna kengefu...you are in trouble man. Watch out!! Not to that extent.

Lakini huko ni kusrisk career kama alivyorisk Dr Dree alivyomsaini Eminem wakati niqqa hawana imani na white kutoboa katika mziki wa hip hop at the end Eminem akawa legendary kwenye hip hop.

Sasa bahati yako utoboe kama Eminem ambae hakumwangusha Dr Dree ila ole wako ubume...career yako na brand yako ndo basi tena!

Mungu wa Vatican akuongoze Mroma mwenye sigida gotini utoe ekarist fresh na nzengo ikuelewe.
 
Monday, April 10, 2017
Sintofahamu kuhusu mkutano wa Roma na waandishi
  • Mapema leo kaka yake Roma, Omary Musa amesema mkutano huo ungefanyika saa tano.
  • Hata hivyo Musa hakuweka wazi eneo la kufanyia mkutano huo kwa kile alichodai bado hawajapata eneo.
By Elizabeth Edward, Mwananchi
Dar es Salaam.

Hali ya sintofahamu imeanza kujitokeza tokea leo asubuhi hadi saa 5: 48 baada ya mkutano aliotakiwa kuufanya Roma Mkatoliki na waandishi wa habari kushindwa kufanyika kwa wakati.


Mapema leo kaka yake Roma, Omary Musa amesema mkutano huo ungefanyika saa tano.

Hata hivyo Musa hakuweka wazi eneo la kufanyia mkutano huo kwa kile alichodai bado hawajapata eneo.

"Eneo tulilopata awali mwenyewe anaonekana kuwa na hofu, tunatafuta eneo lingine tutawajulisha kabla ya saa tano ila tunalenga maeneo ya Kinondoni, "amesema

Ilipofika saa tano mwandishi alimtafuta kujua eneo Musa akajibu bado hawajapata na huenda mkutano huo ungesogezwa hadi saa nane.

"Bado tunatafuta kuna watu wamepewa jukumu hilo, hatuwezi kufanyia popote lazima liwe eneo salama, hatujui waliomteka walikuwa na nia gani"
 
Back
Top Bottom