Shida yako unakunywa mtori unataka nyama uzikute juu. Mtori nyama zake huwa ziko chini kaka. Najua njia ya box la kura kwa amani haiwezi kuleta matokeo tarajiwa, ni wendawazimu kutumia mbinu zile zile ukitarajia matokeo tofauti.
"Mbinu zile zile"zipi mkuu wangu 'Tindo'.
Ninayopendekeza mimi sio "mbinu zile zile" unless kama una maana nyingine ya msemo huo.
Nadhani kuna tatizo mahala fulani na hawa wapinzani, hasa CHADEMA. Mambo yao hayaeleweki kabisa.
Mwanzo nilidhani ni mbinu, na niliwasifu sana jinsi walivyoweza kuepuka mitego mingi waliyowekewa kuwamaliza, hasa ya kuwategeshea wafanye fujo ili wawafute. Lakini kwa haya mengine, kama hawana mkakati ambao wameuweka kuutumia wakati huu hadi kuelekea uchaguzi, basi watakuwa hawana maana yoyote.
Mikutano ya Kamati Kuu, sijui kamati gani, tunasikia tu wamekutana, lakini hawaelezi wamekutana kuzungumza nini na kuamua nini.
Hii ni mikutano ya kunywa maji na soda au chai? Wengine tulidhani mikutano hiyo ni ya mambo mazito; lakini mambo mazito yasiyoonyesha mwelekeo wowote hadi sasa?
Haijawahi kuwepo na nafasi nzuri kama iliyopo wakati huu wa kuiondoa CCM, na wao kama watashindwa kutekeleza jukumu hilo, hawatapata tena nafasi nyingine. Baada ya uchaguzi huu, Magufuli anawafungia milango yote, na hawawezi tena kufurukuta.