Uchaguzi 2020 Huu sio wakati wa upinzani kulialia mnaonewa, wananchi wanahitaji kuhakikishiwa jinsi gani upinzani utakavyolinda kura zao zisiibiwe Octoba 2020

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Maji ukiyavulia ngua sharti uyaoge. Huu sio wakati wa upinzani kulialia eti mnaonewa, mnazuiwakufanya mikutano hata ya ndani, eti hakuna demokrasia!! Huu ni wakati wa mapambano sio kulialia.

Salamu ziwafikie Zitto K, Mbowe, Lema, Sugu, Heche na Mdee kutaja kwa uchache. Wananchi wanaosapoti upinzani wengi wao bado hawajafanya maamuzi Octoba 2020 waenda wakapige kura au wasiende.

Hofu kubwa ya wanaoungamkono upinzani ni kuibiwa kura zao au kutangazwa mgombea wa CCM hata kama hajashinda, hivyo, ni jukumu la nyinyi viongozi wa upinzani kuwahakikishia wananchama wenu, mashabiki nzenu namna gani mtalinda kura zao na kwa namna gani mtazuia asitangazwe mgombea ambae hajashinda!

Huu ni wakati wa mapambano, ni wakati wa kuwaaminisha wananchi kuwa mnaweza.
 
Hapo ccm ndo watajuwa kuwa wananchi wameamua kutiana moyo au wanamwaga au wanapiga bao.
 
Ha ha haaaaaaaaaa

Umeota umemukuja kuandika ndoto..

Mupinzank mna shida.. nani akwambia watapigiwa kura!!!..

Chama tawala kitashinda kwa kushindo..

Upinzani upi. eti huu. ambao hauna hata sera kupita CCM. ni kulalamika tu. hakuna hara A to Z munayofanya. Zaidi ya viongozi wenukutamani pesa. Hata Lissu hajuihadi sasa. Kama atawania. Hiyo chadrama nayo ilishaingia.. Kwa futi sita zamani.. weak viongozi, lazy, hawakujui muntu mwananchi anataka nini.. ni wadaku tu class ya kwanza.. mengine unayakujua..

Anza tu kulia..
 
Hawajitambuagi kwanini ccm wasiwape sikumoja tu nchi

Mtasahau kama kuna upinzani hawana lolote ni wasumbufu tu.
Mpeni kura tundu muone nchi itakavyoaribiwa .
Kwanza yeye anahasira za hapa na pale

Sasa mtu anamatusi basi tu seif ataendekeza mambo ya kidini na mengi tu ambayo itaharibu nchi.
Haya zitoo tu ndio afadhali anajitambua .
Na mrema hata akiwa mzee kiasi gani.

Ila Lowassa ni mtu mnafiki haifai huyoo lazima tuseme ukweli .
Ndio maana watu watawapa kura ccm sio kwamba wanapenda ila wanaogopa sana upinzani kabisa tuseme tu bado hawajatuaminisha wabakie tu kuwa wabunge, madiwani na vyiti vya chini.

Ila hiki kiti waachie CCM
 
Bado mimi kucheka.. nikikuuliza.. kura mupigiwe za nini haswa.. unanijibuje.. 😀😀😀
 
Hebu weka ushauri unataka hatua gani zichukuliwe ili kura zisiporwe, au kutangazwa mtu asiyestahili.
Naona hujibiwi.

Mimi nitaweka ninayoamini kwa moyo wangu wote.

Wapinzani, kwa vile wamekubali kuruhusu na kushiriki kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba, chini ya tume isiyoaminika kuwa ni huru, na katika mazingira magumu kwao, ikiwa ni pamoja na wasimamizi wa uchaguzi wakiwa watu wa chama ambacho wanatafuta njia ya kukiondoa..., wameamua kushiriki; lakini hawaelezi matumaini yao ya kupata ushindi yatategemea nini..., hawasemi mikakati yao ni ipi!

Mimi napendekeza.
Kampeni yao ijikite katika kuwahimiza wapiga kura wajitokeze kwa wingi sana kuliko ilivyowahi kutokea katika historia ya nchi yetu.

Watu wakapige kura zao wanavyoona wenyewe inafaa. Watakuwa wametimiza wajibu wao wa kwanza.

Wizi wa kura na kuvuruga uchaguzi ni rahisi sana kufanyika wakati wapiga kura ni wachache mno. Hii inawapa fursa tume, na wengine kuziharibu kura hizo, na ni vigumu sana kuzifuatilia kujua palipofanyika uharifu. Ni rahisi kupoteza ushahidi.

Kura milioni tatu za ziada, zikiwa zimeelekezwa kwa wapinzani, halafu tume iziharibu tu na zisijulikane zimeenda wapi?

Hapo kuna kila sababu ya kufanya lolote kama ikibidi.
 
Hawajitambuagi kwanini ccm wasiwape sikumoja tu nchi .
Mtasahau kama kuna upinzani hawana lolote ni wasumbufu tu.
Mpeni kura tundu muone nchi itakavyoaribiwa .
Kwanza yeye anahasira za hapa na pale .
Sasa mtu anamatusi basi tu seif ataendekeza mambo ya kidini na mengi tu ambayo itaharibu nchi.
Haya zitoo tu ndio afadhali anajitambua .
Na mrema hata akiwa mzee kiasi gani.
Ila lowassa ni mtu mnafiki haifai huyoo lazima tuseme ukweli .
Ndio maana watu watawapa kura ccm sio kwamba wanapenda ila wanaogopa sana upinzani kabisa tuseme tu bado hawajatuaminisha wabakie tu kuwa wabunge,madiwani na vyiti vya chini.
Ila hiki kiti waachie ccm

Mahaba niue.
 
Iwapo Tundu Lissu pamoja na mapungufu yake kadhaa atagombea urais, hapo ndio nitaweza kwa shingo upande kushawishi watu wajitokeza wakapige kura kwa tume hii. Ila lazima wahakikishe kuwa tume hii ya uchaguzi inavuliwa nguo, na iwe ni uchaguzi wa mwisho wa tume hii isiyoaminika.
 
hapo ndio nitaweza kwa shingo upande kushawishi watu wajitokeza wakapige kura kwa tume hii. Ila lazima wahakikishe kuwa tume hii ya uchaguzi inavuliwa nguo, na iwe ni uchaguzi wa mwisho wa tume hii isiyoaminika.
Ni hatua mhimu uliyoipiga kwenda mbele.

Sasa tushirikiane kuwahimiza wapinzani wafanye kazi ya ziada kuwahimiza wananchi wafanye kweli.
 
Ni hatua mhimu uliyoipiga kwenda mbele.

Sasa tushirikiane kuwahimiza wapinzani wafanye kazi ya ziada kuwahimiza wananchi wafanye kweli.

Sio wafanye kweli, bali wawe tayari kwa machafuko, jambo ambalo naliona gumu kwa watanzania wengi wa sasa. Ngoja niweke imani ya mashaka.
 
Sio wafanye kweli, bali wawe tayari kwa machafuko, jambo ambalo naliona gumu kwa watanzania wengi wa sasa. Ngoja niweke imani ya mashaka.
CHADEMA na ACT- wawe na wanachama zaidi ya milioni sita (kama wanavyodai wao), halafu wakose watu hata milioni moja waliojitoa kulinda haki ya ushindi wao usivurugwe?

Hivi vitakuwa ni vyama vya siasa, au ni vyama vya kufurahishana tu huko waliko? Nitawashangaa sana.
 
Hatutakiwi kuwapa wapinzani jukumu la kutuambia ni vipi watazilinda kura zao,ni jukumu letu kuwauliza serikali no jinsi gani tutafanya uchaguzi Wa huru na haki na wenye kuheshimu maamuzi ya wananchi.
 
CHADEMA na ACT- wawe na wanachama zaidi ya milioni sita (kama wanavyodai wao), halafu wakose watu hata milioni moja waliojitoa kulinda haki ya ushindi wao usivurugwe?

Hivi vitakuwa ni vyama vya siasa, au ni vyama vya kufurahishana tu huko waliko? Nitawashangaa sana.

Kumbuka hao watu milioni moja watakuwa wanapambana na vyombo vya dola vilivyoagizwa kufanya lolote, ili ccm watangazwe washindi. Sijui kama unalielewa hili. Hivi unajua fomu ya matokeo kila kituo itatolewa moja tu kwa mawakala iwapo tume itaona hivyo?

Vyombo vya dola vitahusishwa moja kwa moja kwenye hii hujuma. Ninaposema silaha za Jadi nielewe nini ninasema, na wapinzani wawaambie kabisa wapiga kura wao kuwa hata polisi wasiaminike kwenye uchaguzi huu.
 
Hizo kura zenyewe chache sasa watazilinda vipi,
Watakimbia mabox wao wenyewe.
 
Sijui kama unalielewa hili. Hivi unajua fomu ya matokeo kila kituo itatolewa moja tu kwa mawakala iwapo tume itaona hivyo? Vyombo vya dola vitahusishwa moja kwa moja kwenye hii hujuma. Ninaposema silaha za Jadi nielewe nini ninasema, na wapinzani wawaambie kabisa wapiga kura wao kuwa hata polisi wasiaminike kwenye uchaguzi huu.
Mkuu Tindo, hili siko tayari kulisimamia na kulijengea hoja.
Sijui kama fomu ya matokeo ni moja, na vyama vya upinzani bado wakaona ni jambo la kawaida sana kiasi cha kukubali uchaguzi uendelee.

Hili nikiri kabisa silijui, kama wewe unalijua vizuri, nipo tayari kujifunza toka kwako.

Na kama utajitolea kuwa mwalimu wangu, nitashukuru pia kujua kama hizo fomu za matokeo haziruhusiwi pia kupigwa picha au kunakiliwa kwa njia nyingine yoyote.
Haya ni mambo nisiyoyajua. Inawezekana pia hawa wanachama wa vyama hivi vya upinzani pia wakawa hawajui chochote kuhusu hali hiyo!
 
Kulinda kura ni neno rahisi lakini utekelezaji wake ni mgumu.Kama una uwezo na nafasi pitia uchaguzi mdogo wa Kinondoni na Siha kwa Mollel.Naamini ya kuwa utaelewa.Ni ngumu na hasa kwa awamu hii ubabe uliopitiliza utatumika.Wana demokrasia na wapenda mabadiliko wanatakiwa kurudi nyuma(retreat) kwa manufaa yao binafsi na nchi.
 
Back
Top Bottom