Uchaguzi 2020 Huu sio wakati wa upinzani kulialia mnaonewa, wananchi wanahitaji kuhakikishiwa jinsi gani upinzani utakavyolinda kura zao zisiibiwe Octoba 2020

Unatunga uongo ili kuhalalisha mawazo yako,sawa bwashee mjukusanye kulinda kura.

Sina sababu yoyote ya kutunga uongo, hii ndio sababu ya msingi watu kuacha kupiga kura hasa awamu hii, na hayo mambo yalifanyika mbele ya macho ya wananchi. Haya mambo hakuna asiyeyajua, japo watu wako kimya kwa hofu ya maisha yao.
 
lukoma,
Ushauri wangu kwakuwa kuna watu wameshajitokeza kugombea kupitia upinzani basi sisi wananchi tuwape moyo kwa kuzilinda kura, tunalindaje.....
 
Shida yako unakunywa mtori unataka nyama uzikute juu. Mtori nyama zake huwa ziko chini kaka. Najua njia ya box la kura kwa amani haiwezi kuleta matokeo tarajiwa, ni wendawazimu kutumia mbinu zile zile ukitarajia matokeo tofauti.
"Mbinu zile zile"zipi mkuu wangu 'Tindo'.

Ninayopendekeza mimi sio "mbinu zile zile" unless kama una maana nyingine ya msemo huo.

Nadhani kuna tatizo mahala fulani na hawa wapinzani, hasa CHADEMA. Mambo yao hayaeleweki kabisa.

Mwanzo nilidhani ni mbinu, na niliwasifu sana jinsi walivyoweza kuepuka mitego mingi waliyowekewa kuwamaliza, hasa ya kuwategeshea wafanye fujo ili wawafute. Lakini kwa haya mengine, kama hawana mkakati ambao wameuweka kuutumia wakati huu hadi kuelekea uchaguzi, basi watakuwa hawana maana yoyote.

Mikutano ya Kamati Kuu, sijui kamati gani, tunasikia tu wamekutana, lakini hawaelezi wamekutana kuzungumza nini na kuamua nini.

Hii ni mikutano ya kunywa maji na soda au chai? Wengine tulidhani mikutano hiyo ni ya mambo mazito; lakini mambo mazito yasiyoonyesha mwelekeo wowote hadi sasa?

Haijawahi kuwepo na nafasi nzuri kama iliyopo wakati huu wa kuiondoa CCM, na wao kama watashindwa kutekeleza jukumu hilo, hawatapata tena nafasi nyingine. Baada ya uchaguzi huu, Magufuli anawafungia milango yote, na hawawezi tena kufurukuta.
 
Tangu kuzaliwa kwa CCM huu ndio uchaguzi mgumu kuliko zote kwa (upande wao), na ni uchaguzi mwepesi & sahihi kwa CDM kushika dola iwapo mambo kadhaa yatatiliwa maanani:-

1. Kutafuta ushindi kupitia sanduku la kura. Kwa dalili zilizopo kuna kama 2% tuu za njia hii kufanya kazi.
2. Kutafuta ushindi/dola nje ya box la kura. Kwa watu wanaojua kusoma alama za nyakati, hii ndio njia ya kipekee na uhakika wa ufanisi kwa zaidi ya 100% bila kujali itagharimu muda gani(miezi/miaka).

Hitimisho; Ni ukweli mtupu kwamba CDM ilishavuka hatua zote za kisiasa kama, kutafuta wanachama, kura, umaarufu, falsafa n.k
Kilichobaki sasa ni chama hiki pendwa kutafuta DOLA kwa njia yoyote ile, na muda wa kufanya hivyo ni October 2020.
Hii ndio nafasi ya mwisho kwa CDM & Watanzania kufika pale tulipokuwa tukitamani miaka yote.

NB: Hasara za CDM kuacha huu uchaguzi upite kama ilivyofanya kwa chaguzi za nyuma ni kubwa kuliko, kwani chama kitaenda kubaki kwenye damu na mioyo yetu lakini kwa upande wa NGUVU na MAMLAKA vitabaki kwa dikteta jambo ambalo litafanya iwe vigumu kuitofautisha (CDM) kama chama cha siasa na kikundi cha kiimani.
 
Ukombozi wa kweli toka mikononi mwa udhalimu kote duniani huwa unaletwa na nguvu ya umma. Kuwaachia jukumu hili viongozi wa upinzani pekee wanaokamatwa na kubambikiziwa kesi feki na kuwekwa ndani Kila wakati ni kuwaonea tuu
 
Ukombozi wa kweli toka mikononi mwa udhalimu kote duniani huwa unaletwa na nguvu ya umma. Kuwaachia jukumu hili viongozi wa upinzani pekee wanaokamatwa na kubambikiziwa kesi feki na kuwekwa ndani Kila wakati ni kuwaonea tuu
Mkuu 'antimatter' ni wapi uliponisoma nikisema "kuwaachia jukumu viongozi wa upinzani pekee"?

Unaposoma jaribu kuelewa unachokisoma kwanza kabla hujajibu chochote.

Hapa naweza kusema unapindisha kwa maksudi niliyoandika mimi.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom