Huenda Wabunge wengi wa CCM wakashindwa kurudi 2025 na upinzani ukalamba dume

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
2020 Kulikuwa na upepo wa ajabu kwa wabunge wengi wa CCM kwani walibebwa kama watoto wachanga na JPM na Livingston Lusinde ni shahidi kwani yeye alisema kuwa kunawabunge hata kwa kuzikiri bila nguo wasinge rudi ila Magufuli aliwabeba na mbeleko.

Taarifa nilizo zipata kutoka chanzo cha uhakika lakini hakina ushahidi wa kutosha kinasema kuwa wabunge hao ambao kumbe wanajitambua kuwa walipita na ule upepo wameanza kuweka akiba ya kutosha kifedha hili kuja kutetea nafasi zao 2025 kwani mazingira kama yale wanaona hayatakuwepo tena.

Hii ni turufu kwa wapinzani kama wataweza kujipanga na kugawana majukumu, wengine washughulikie mambo ya ujenzi wa chama na wengine washughulikie mambo ya kesi. Kinachoonekana katika Mfano CHADEMA macho, akili, nguvu na kilakitu vimeelekezwa mahakamani tu, utashangaa kulikuwa na ujenzi, ukarabati na ufunguzi wa ofisi za chama nchi nzima CHADEMA DIGITALI lakini kwa sasa hakuna kitu kama hicho tena kwani chama ni mtu mmoja tu chama chote kipo mahakamani.

CCM imekuwa ikitumia mbinu nyingi sana za kiakili tofauti na wapinzani wamekuwa wakitumia nguvu za misuri au nguvu za umma kama wanavyodai, hii ni ngumu sana kwa siasa za hivyo kuiondoa CCM. Dunia nzima ilishaacha matumizi ya nguvu zamani, isipokuwa nguvu inatumika kama biti lakini hakuna taifa kwa kalne hii linaloweza kupoteza muda katika nguvu isipokuwa akili tu.

Nakumbukuka Mzee Lowasa aliwai kushauri kuachana na matumizi ya nguvu na kubadilisha kabisa staili ya mapambano kutoka nguvu/harakati na kuwa chama cha kujiandaa kuchukuwa nchi mikakati akili. Mzee alishambuliwa na watu wote wa Ufipa kwani wanaamini katika nguvu tu na si akili. Mi sitaki kujua wala kujadili nani aliwapa Chadema jina la NYUMBU lakini nadhani ifike wakati wakubali walifute hilo jina kwa vitendo na si kutukana mitusi watu.

Sisi kama wananchi wa kawaida inafika wakati sasa tunachoka kwani nchi karibuni zote Afrika zimebadili vyama isipokuwa Tanzania tu kunani? Kunatatizo, tena katika vyama vya upinzani, mi sitaki haya maneno ya kinyumbu kilasiku eti wametuibia kura, tume siyo huru, polisi wametupiga. Kalne hii mnaongea polisi? Kuibiwa tena kilasiku mpaka sasa tunakuwa wazee CCM tu. Mbona Zambia kiliondoka, Malawi kiliondoka, Kenya kiliondoka, Ghana, Zaire/Kongo inamaana huko kulikuwa hakuna polisi, awaibi, hakuna tume. Acheni bwana sisi tunataka mlete mabadiliko tena kwa amani na kwa akili kwani kama nguvu hamna hata robo.

Tena mfaham nahii fasheni ya Democrasia inaweza kuisha, ya kuwa na vyama vingi kwani hamjui kuwa wazungu walileta kwa sababu zao wakiona imepitwa na wakati wataleta kitu kingine kama huku kwetu kanisani kwani hamuoni walituletea makanisa sasa hivi wameacha kwenda kanisani na wanampango wa kuleta kitu kingine na si mnajua sisi waafrika tunafuata kwa wazungu kilakitu mpaka jinsi ya kwenda msalani.

CCM imechoka sana ila upinzani umechakaa kabisa upo kibinafsi hivi, yani upinzani wa Tanzania uwezi kubisha ni mtu tena mmoja angalia kila chama ni mtu tu, mtu, mtu tu. Unaweza kuona kuna mwenyekiti mmoja Profesa alijiondoa madarakani alafu akajirudisha. Ndiyo maana utasikia wanasema CCM itakaa miaka 9000 huu si utabili ni akili za hisabati tu badilikeni mchukuwe nchi tuone mabadiliko mbona dunia inazunguka kwanini Tanzania haizunguki.

Mtoto wa mchungaji nawasilisha.
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa...Maana wamebebwa ila wameamua kuchana mbeleko.

Tutaona nani mjanja sasa kati ya wao na mbeleko iliyowabeba
 
Upinzani gani unaouzungumzia hapa? Vyama vilivyokufa vifufukie kwenye ushindi wa uchaguzi ?! Hiyo ni ndoto ya mchana.
 
2020 Kulikuwa na upepo wa ajabu kwa wabunge wengi wa CCM kwani walibebwa kama watoto wachanga na JPM na Livingston Lusinde ni shahidi kwani yeye alisema kuwa kunawabunge hata kwa kuzikiri bila nguo wasinge rudi ila Magufuli aliwabeba na mbeleko...
Labda kwa Katiba ya Kenya
 
Tatizo ni huyu jamaa👇
8860003675.jpg
 
CCM tuna uhakika wa kushinda uchaguzi wa urais 2025 na idadi kubwa ya wabunge na madiwani.
Hongera Kwa uhakika huo, ila msiwatumie polccm, na akina neck ongeza na mbeleko nyingine tuone. Nini kinawakuteni.
 
CCM hawana uwezo wa kushinda uchaguzi wowote. Kama tu kujenga matundu ya vyoo kumewashinda mambo ya uchaguzi watawezea wapi
 
Mchawi katiba, haya mengine ni "ujinga" wako tu.

Akina Lissu "wamepigwa" risasi sababu ya katiba mbovu, akina Saanane "wamepotezwa" sababu ya katiba mbovu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom