Uchaguzi 2020 Huu sio wakati wa upinzani kulialia mnaonewa, wananchi wanahitaji kuhakikishiwa jinsi gani upinzani utakavyolinda kura zao zisiibiwe Octoba 2020

Kumbuka hao watu milioni moja watakuwa wanapambana na vyombo vya dola vilivyoagizwa kufanya lolote, ili ccm watangazwe washindi. Sijui kama unalielewa hili. Hivi unajua fomu ya matokeo kila kituo itatolewa moja tu kwa mawakala iwapo tume itaona hivyo? Vyombo vya dola vitahusishwa moja kwa moja kwenye hii hujuma. Ninaposema silaha za Jadi nielewe nini ninasema, na wapinzani wawaambie kabisa wapiga kura wao kuwa hata polisi wasiaminike kwenye uchaguzi huu.
Exactly!!!
 
Inaonekana hukufuatilia hili, na wapinzani walitakiwa wasaini siku hiyo hiyo waliyokwenda kwenye kikao cha maadili, na sharti ilikuwa kama hutasaini sheria hiyo ya maadili siku hiyo hiyo hutaruhusiwa kushiriki uchaguzi. Hali hii ilimuacha Mnyika bila uchaguzi zaidi ya kusaini hiyo sehemu ya kanuni za uchaguzi. Iko hivi wanasema fomu za matokeo zinaweza kuwa chache, hivyo iwapo hazitatosha huna haki ya kuidai.

Mchezo uko hivi, sehemu ccm watakayoshinda kihalali fomu za matokeo zitatolewa, ila sehemu watakayoshindwa, maafisa wa tume watasema fomu za matokeo hazitoshi. Kama tayari sheria imetungwa kwa nia ovu, utapata wapi nafasi ya kupiga picha hiyo moja?

Hata ukipiga picha ndio utaenda kuitumia kama ushahidi mahakamani? Wanachama kwa wingi wao inawezekana wakawa hawajui maana vyama vya upinzani hawaongelei ana haya mapungufu, huenda ni kwa kukosa platform nzuri ya kuongelea haya, ama hawana watu wazuri wa elimu kwa umma, au vyote kwa pamoja. Ngoja kama Chadema watakuja kulielezea hili vizuri, au mdau mwingine aseme hili.

Cc: Chadema, Tumaini Makene, John Myika
 
Upinzani wameshashindwa kabla hata kampeni kuanza.

Badala ya kulia na kuwaza kuibiwa kura wasingeshiriki kabisa kwenye uchaguzi wajipange upya.
 
tindo,
Nimekusoma vyema mkuu 'Tindo'.

Kama hali ndivyo kama ulivyoielezea hapa, hao wapinzani wanakwenda kushiriki uchaguzi kwa mategemeo yapi?

Kusema kweli sio hilo tu, kuna mambo kadhaa ya namna hiyo ambayo wapinzani wameyaacha au wameyapuuzia bila maelezo yoyote, huku ikiwaacha watu wakidhani kwamba pengine wanayo 'plan B' wanayoificha itakayosawazisha sintofahamu nyingi hivi.

Kama hawana plan nyingine yoyote watakuwa ni watu wapuuzi kupindukia.
 
Mkuu ninapokuambia kushiriki uchaguzi kwa tume hii ni upunguani, lakini naona huwa hunielewi. Hata huyo Lissu ninayetaka aje kwenye uchaguzi, sio kwa Mantiki nipigie kura, bali nataka aje kwenye kampeni na kuamsha public awareness itakayopandisha hamasa, ila siku ya uchaguzi watu wahamasishwe kutokwenda, ili kushusha idadi ya wapiga kura. Idadi hiyo ndogo itapelekea mabadiliko makubwa sana kwenye nchi yetu. Nguvu ya umma sio lazima machafuko, bali hata kususia inakosesha serikali uhalali wa kuwa madarakani.
 
Mkuu ninapokuambia kushiriki uchaguzi kwa tume hii ni upunguani, lakini naona huwa hunielewi.
Hapana.

Katika hili tulishayamaliza kabisa.

Haya mengine yanayojitokeza sasa ni maswala tofauti kabisa, na tuyajadili yalivyo.
 
Mantiki nipigie kura, bali nataka aje kwenye kampeni na kuamsha public awareness itakayopandisha hamasa, ila siku ya uchaguzi watu wahamasishwe kutokwenda, ili kushusha idadi ya wapiga kura. Idadi hiyo ndogo itapelekea mabadiliko makubwa sana kwenye nchi yetu. Nguvu ya umma sio lazima machafuko,
Nilikuwa sijakusoma hadi huku chini.

Loo, acha tu kwa sasa nibaki nikishangaa haya uliyoyaandika hapa!
 
Nilikuwa sijakusoma hadi huku chini.

LOoo, acha tu kwa sasa nibaki nikishangaa haya uliyoyaandika hapa!

Shida yako unakunywa mtori unataka nyama uzikute juu. Mtori nyama zake huwa ziko chini kaka. Najua njia ya box la kura kwa amani haiwezi kuleta matokeo tarajiwa, ni wendawazimu kutumia mbinu zile zile ukitarajia matokeo tofauti.
 
Ukishapiga kura rudi nyumbani kasubiri majibu kwenye tv ama redio n.k.

Ingekuwa kuna tume huru hapo sawa, sio tume hii inayoagizwa na rais imtangaze nani mshindi. Uzuri wapiga kura wengi wanaojitambua, hawatajitokeza kushiriki hayo maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi.
 
tindo,
Hakuna lolote la kuhofu ndugu. Ata tume waweke masharti ya namna gani kinachotakiwa kusisitizwa mwaka huu ni kuwa wananchi walinde kura na mawakala na wananchi wasimamie kidete, kura zilivyohesabiwa na ndo na matokeo yatangazwe hivyohivyo kuanzia udiwani, ubunge hadi upraising. Mawakala watoe matokeo vituoni hapo hapo ya ngazi zote na records zitunzwe sawa. Tume ikitangaza tofauti wananchi waingie mtaani
 
Ingekuwa kuna tume huru hapo sawa, sio tume hii inayoagizwa na rais imtangaze nani mshindi. Uzuri wapiga kura wengi wanaojitambua, hawatajitokeza kushiriki hayo maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi.
Tume ni huru na mawakala wa vyama vyote watakuwepo kuhakiki kura za kila mgombea.baada ya kupiga kura rudi nyumbani.
 
Hakuna lolote la kuhofu ndugu. Ata tume waweke masharti ya namna gani kinachotakiwa kusisitizwa mwaka huu ni kuwa wananchi walinde kura na mawakala na wananchi wasimamie kidete, kura zilivyohesabiwa na ndo na matokeo yatangazwe hivyohivyo kuanzia udiwani, ubunge hadi upraising. Mawakala watoe matokeo vituoni hapo hapo ya ngazi zote na records zitunzwe sawa. Tume ikitangaza tofauti wananchi waingie mtaani
Wakitangaza tofauti wananchi waingie mtaani!?, unawaanda wapumbavu wapinge matokeo halali ya uchaguzi.
 
Wabishi na madikteta wote duniani wametolewa na Nguvu ya umma ndugu. Hata kenya Tume huru ilikuja baada ya nguvu ya umma kufanya yake. There is no fairness bila wewe kupigania iyo fairness
 
Tume ni huru na mawakala wa vyama vyote watakuwepo kuhakiki kura za kila mgombea.baada ya kupiga kura rudi nyumbani.

Niliona kwa macho yangu kwenye chaguzi za marudio, mawakala wa upinzani wakipigwa kama wezi na polisi ili wajaze fomu fake ya matokeo. Siwashauri wananchi kujitokeza kupiga kura chini ya tume hii, maana ni kuhalalisha uhayawani. Ni vyema wananchi kutokea kwa idadi ndogo sana ili kuharamisha huo ushenzi.
 
Unatunga uongo ili kuhalalisha mawazo yako,sawa bwashee mjukusanye kulinda kura.
 
Back
Top Bottom