Sasa wanamuhoji ili iweje , Dunia ya sasa unafatwa kwa sababu umeifanyia nini Dunia au kitu gani umekifanya kinakutofautisha na binadamu wengine au nyumbani kwako unasifikaje !!
Hana impact kwenye maisha ya wabongo , itakua huko kwa wenzetu ?
Labda kama mnataka ahojiwe kwa sababu ya jinsia !! Gender Balance
Acha ujinga wewe, Hivi Nani asiye Tambua kazi ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani katika ukanda huu wa Afrika mashariki na Kati? Unapozungumza Tanzania maana yake unamzungumza mama yetu Samia, Sasa utamkwepa vipi mama Samia katika kulinda amani ya ukanda huu na Afrika kwa ujumla?
Tanzania chini ya mama Samia imeendelea kuwa kimbilio la wanyonge na wanazohitaji kupumzika Kama ulivyoona Raila Odinga akina hapa Tanzania kupumzika,
Dunia inamtambua na unatambua mchango wa mh Rais wetu mpendwa kwa kupigania haki ya Elimu kwa mtoto wa kike, Hata ukienda Taasisi kubwa za kiharakati na haki za kibinadamu wanatambua Alama ya mama yetu Katika kumuwezesha mtoto wa kike kupata Elimu biila kikwazo
Dunia inatambua mchango wa mama Samia katika kupunguza vifo vya mama na mtoto baada ya juhudi zake za kuboresha huduma za Afya na kusogeza huduma karibu ya mwananchi
Dunia inatambua mchango wa mama yetu Katika kuhakikisha usalama wa chakula unakuwa imara na hata kuwalisha majirani zetu Kama Kenya wenye shida ya chakula kutokana na ukame kwao
Dunia inatambua mchango wa mama yetu Katika kupambana na mfumuko wa Bei, kuvutia wawekezaji na kuifanya Tanzania kuwa chaguo namba moja kwa mgeni yoyote atakaye kuja katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika
Mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani ndio kioo Cha Afrika kwa Sasa katika uongozi Bora na utawala wa sheria