Huu mfumo wetu Tanzania wa kukusanya mapato, kutoa malipo na kulipa kodi unaniweka hoi. Ijapokuwa malipo ni halali na unapewa risiti, kuna uwezekano kuwa risiti hizo ni feki (kuna watu wanarudufu risiti zao), na malipo hayo yakaishia matumboni mwa walafi.
Nimeona mfumo wa nchi moja, ambapo malipo yoyote rasmi, iwe katika sekta ya umma au binafsi, daima hupeleki pesa ofisini na kuwaachia watu kuchota na kuchachachua. Badala yake unapewa risiti kwenda kulipa benki (hata kama ni senti 5), ambako idara au shirika husika lina akaunti yake. Lakini petu, mtu unamlipa barabarani. Huu si wizi ni nini? Ama kweli sisi ni wadanganyika!