Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 874
Kama kuna kero ambayo wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanaipata hasa kwa wamiliki wa magari ya abiria basi hili la kuchukua ushuru unaoitwa wa kuboreshwa kwa mji wa Songea.Kila barabara inayoingia mjin Songea kilomita 5 hadi 6 imewekewa kizuia(road block) kwa ajili ya kusimamisha magari yote yanayofanya biashara na kukusanya pesa ya maendeleo.lakini cha ajabu na kwa uchunguzi niliofanya kwa muda mrefu sasa imeonekana kuwa huu ni mradi wa baadhi ya watawala hapa mkoani.Kwani pesa inayokusanywa kila siku haioneshi kama inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Bado barabara zetu ni chafu.Ukija stand kuu ya mabasi napo kuna kamba imewekwa pale ili kila gari linaloingia stendi na kutoka linapaswa kulipa pesa.Jamani sijapata ona stand ovyo kama hii ya Songea.Utadhani sio Manispaa.Ni bora isingepandishwa hadhi ya kuitwa manispaa.Tunajiuliza hivi hizi pesa zinazokusanywa zinakwenda wapi?Nimepata kuwauliza wale wakusanya ushuru,walitoa kauli ambazo zinathibitisha kuwa huu ni mradi wa wajanja.Nao kwa kutambua kuwa huu si mradi wa serikali iliyo makini huwa hawatoi risiti kwa madereva baada ya malipo.Sasa tunajiuliza ikiwa mtu anakusanya pesa bila kuwaonesha ushahidi wa makusanyo hayo,je kweli kuna uhalali hapo?Tuite ufisadi mdogo mdogo?Wako wapi viongozi wetu?Tupeni majibu kwanini stand hii ipo katika hali mbaya?