Huu ni ushauri wa bure kwa wasanii wetu wote wa kitanzania..

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,283
976
Ninafahamu kiingereza ni lugha yetu ya tatu, hivyo sio ajabu mtu kutokuifahamu kiufasaha.. Lakini unapofanya kazi yako ya sanaa, iwe kuimba au kuigiza na ukataka 'kuchomekea' au kutumia neno la kiingereza, basi uwe umelihariri vizuri au mtu anayejua lugha hiyo vizuri awe amehariri kabla ya wewe kutumia.. Kwa wale waigizaji, basi upande wa kuongea au pale kwenye "subtitle" au tafsiri inayopita chini ya runinga..
Kwa wanamuziki, ni wakati wa kuimba.. Mfano: kuna wimbo unaitwa "bwashee" wa Ally Kiba na Baby J.. Badala ya kutamka "playboy" wao husema "playerboy"..
Tuwe makini ili tushindane vyema kimataifa!!

Ongezea na unaowajua..
 
Back
Top Bottom