Ushauri wa bure kwa waajiriwa wote

Samedi Amba

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
227
178
Habari wanaJF!
Natumaini Jumapili imeanza vyema. Katika pitapita zangu, nimekutana na mawaidha yafuatayo yanaweza kukusaidia wewe mwajiri kuwa na mwisho mzuri na kufurahia maisha ndani (na baada) ya kazi.

1. Jenga nyumba mapema. Iwe kijijini au mjini. Usisubiri kufikia miaka 50. Usizoee nyumba za serikali au kampuni. Urahisi utakaopata katika nyumba hizo sio za kudumu. Iruhusu familia yako kuenjoy ndani ya nyumba yako mwenyewe.

2. Kumbuka kurejea nyumbani. Usiishie kufanya kazi tu mwaka mzima. Wewe si nguzo ya idara yako. Endapo utakufa leo, mfanyakazi mwingine atatafutwa na shughuli zitaendelea. Fanya familia yako kuwa kipaumbele.

3. Usifukuzie sana kupandishwa cheo. Bobea katika kazi na uwe na ujuzi kwelikweli kwa kile unachokifanya. Endapo watataka kukupandisha cheo, freshi. Vinginevyo, jivunie ujuzi ulio nao usioweza kughushiwa.

4. Epuka siasa za ofisini. Ondokana na mambo yanayochafua jina lako. Usijiunge na wadau wanaokejeli wakuu wako au wafanyakazi wengine. Kaa mbali na watu ambao ajenda yao kuu ni kuwajadili watu wengine.

5. Kamwe usishindane na mabosi zako. Utaunguza vidole vyako bure. Usishindane na wafanyakazi wenzako, utaishia kukaanga ubongo wako.

6. Anzisha biashara ya kukupa hela za ziada. Au mishe fulani hivi ya kukuongezea kipato. Mshahara wako hautakidhi mahitaji na ndoto yako ya muda mrefu.

7. Hifadhi kiasi fulani cha pesa. Ikiwezekana, omba mwajiri wako aikate juu kwa juu kwenye mshahara wako.

8. Chukua mkopo kwa ajili ya biashara au kubadilisha hali fulani ulionayo na sio kwa ajili ya anasa. Endapo unataka kuenjoy, tumia faida ya biashara kufanya hivyo.

9. Tunza siri za maisha yako, ndoa na familia. Ni muhimu kutochanganya kazi na maisha nje ya kazini.

10. Kuwa mwaminifu kwa nafsi yako na kwa kazi yako. Kumwamini sana bosi wako kutakutenganisha na wenzako na bosi wako huenda ataondoka hatimaye (na kukuacha mataa).

11. Panga kustaafu mapema. Anza kujipanga punde unapopokea barua ya ajira. Anza leo. Mpaka unafikia miaka 40 hadi 50 uwe ushasepa.

12. Jiunge na vyama vya ustawi kazini na uwe mwanachama hai. Itakusaidia sana wakati tukio lolote litatokea.

13. Tumia likizo kujenga nyumba yako au kufanya miradi itakayokusaidia siku zijazo.. kawaida unachofanya wakati wa siku za likizo ya picha fulani ya maisha utakayoishi baada ya kustaafu..Ikiwa muda huu kutazama Bongo mobie, usitegemee chochote tofauti utakapostaafu.

14. Muda mzuri wa kuanzisha miradi na biashara ni wakati bado upo kazini. Utakuwa na nafasi ya kujaribu vitu mbalimbali bila presha. Endapo mradi wako utaenda vizuri, basi utakuwa na haki ya kustaafu ili kusimamia biashara yako. Wastaafu wengi hushinda na maisha kwa sababu wanastaafu kisha wanaanza mradi, badala ya kustaafu na kisha kuendeleza mradi waliouanzisha tayari.

15. Hela ya pensheni sio ya kuanzisha mradi au kujengea nyumba, bali ni fedha kwa ajili ya kujitunza katika afya njema. Sio salama kutumia hela hizi kulipia karo ya shule au kuoa mke mdogo bali zitumie kujitunza.

16. Kumbuka, kustaafu kwako kusiwe sababu ya gumzo mtaani, watu wakikusondea kwa namna ulivyofeli. Tafuta kuwa mfano wa kuigwa na wenzako.

17. Usistaafu tu kisa umri umeenda, au wewe ni mzigo kwa kampuni, au unasubiria siku ya kufa. Pumzika ukiwa bado kijana, ambaye ana uwezo wa kunywa kinywaji pendwa asubuhi, uwe na muda wa kupokea pesa kutoka kwa biashara yako, na pia unaweza kutembelea maeneo pendwa, na kuwa na muda mzuri na familia yako. Wale wanaostaafu wakiwa wamechelewa, hutumia takribani asilimia 95 ya muda wao kazini badala ya kuwa na familia zao na ndiyo maana wanaona ni vigumu kukaa na familia zao wanapostaafu. Wengi huishia kutafuta kazi nyingine na kuhangaika hadi kaburini. Vnginevyo, wengi hufa mapema.

18. Iache hiyo nyumba ya serikali/kampuni mapema, ili unapostaafu uweze kufit katika jamii inayokuzunguka. Si rahisi kuzoea mazingira mapya baada ya kukaa kwa miaka mingi kwenye nyumba ya kampuni au katika nyumba ya serikali.

19. Kamwe usiruhusu marupurupu ya ajira yakufanye usahau kupanga maisha baada ya kustaafu. Marupurupu yana tabia ya kukupumbaza vili, ili utulie huku mda unakwenda... Kumbuka ukistaafu hakuna mtu atakayekuita bosi endapo huna biashara inayoweza kukubeba.

20. Usichukie maisha ya kustaafu. Utastaafu tu siku moja, ama kwa kutaka au kutotaka.
 
Mwenye kuelewa na aelewe.
 
Hivi mshahara wa 420000 unatosha kujenga nyumba pamoja na kuendesha familia?
 
Basi sawa nimekuelewa mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom