Huu ni ushamba au itafiki ya lazima katika kutambulisha viongozi na watu maarufu hapa nchini?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,619
46,258
Katika matukio mbalimbali imezoeleka kusikia viongozi au watu maarafu wakitambulishwa kwa kuanza na viwango vyao elimu kabla ya majina yao (wakati mwingine hata kama ni digrii za heshima tu!).

Utasikia Professor au Dokta fulani katika shughuli za kijamii, harusi na hata mazishi!

Ningependa kufahamu utambulishaji wa aina hiyo ni kuzingatia itifaki au ni ushamba?

Nauliza kwa sababu huwa sioni utambulishaji wa aina hiyo katika mataifa yaliyoendelea na ambayo Idadi kubwa ya viongozi wake huwa ni maprofessa na madokta wabobevu katika nyanja zao.
 
Kwan kinakuuma nn Mimi kwangu it's OK...let them celebrate hayo majina siyo kazi mdogo mpaka wakayapata
 
Kama tatizo lako ni Kukereka kusikia Wenzako wakitajwa kwa Kuitwa Profesa au Dakta bado nawe hajachelewa Kwenda Chuo Kikuu ili ukasome ili baadae nawe uje uitwe hivyo kisha utatupa Mrejesho wako kuwa unajisikiaje. Acha Wivu na Ulugaluga tafadhali!!
 
Hii huwa inachosha sana pia, sijui kwa nini huwa wanapenda kurefusha sana salama.
Nafkiri kutambua uwepo wa viongozi wakuu wawili watatu wanaohusika na tukio moja kwa moja na kisha kutoa salamu ya jumla kwa watu wote inatosha sana kuliko kutaja misururu ya watu.
Hivi hawawezi tu kuanza hituba bila itifaki ya kutambulishana, huwa inachosha sana. Unakuta viongozi wako kumi na wote wnatambulishwa na kusimama kupunga mkono, huwa tunachoshana sana.
 
Kama tunamtambulisha mtu kama Mhandishi Juma kwa nini tusimtambulishe mwingine kama CPA Mhasibu Mwajuma?
Kwan kinakuuma nn Mimi kwangu it's OK...let them celebrate hayo majina siyo kazi mdogo mpaka wakayapata
 
Hii protocol ni kwa Tanzania tu? sijwahi kuona kituko cha aina kwa wenzetu ambao viongozi wao wengi ni Maprofesa, madokta na Wahandisi!
And that is what we call protocol,
 
Hii protocol ni kwa Tanzania tu? sijwahi kuona kituko cha aina kwa wenzetu ambao viongozi wao wengi ni Maprofesa, madokta na Wahandisi!
Kwani lazima kila kitu tuwaige wao? Kama inakuuma sana na wewe kasome kama una ubavu uitwe "MHANDISI YODA"
 
Kwani Waliosoma ni wahandisi tu? Mimi nataka nitambulishwe kama CPA Mhasibu Yoda na mke wangu awe anatambulishwa kama nesi Bahati

Jitambulisheni hvo hakuna anaewazuia.
Na mimi mkulima nitajitambulisha "Mkulima Mundende"
 
Back
Top Bottom