Huu ni ulimbukeni au utoto?

Huu ni ulimbukeni au utoto?

Watu wavivu kuandika muda mrefu kwa hiyo ndio maana wanafupisha ili kurahisisha..
 
Jumbe za watu wanaopenda kufupisha kwangu huwa naziona ni ngumu sana, siwezi hata kujibu.
 
Hiv miss, chaga ni mzuri km jina lake na waridi pembeni au ,,,,,,
 
Kuna watu wanafedhehesha sana, tena wengine wakiwa ni watu wazima waliofika miaka 40 au zaidi huku wakiwa wanaandika hovyo wakati wa kutuma ujumbe hasa WhatsApp au hata sms za kawaida.

Mtu mzima unamtumia mwanaume mwenzako sms eti inasema "oi, xafi, vepee, xhwari nk! Hivi watu huwa hamuoni kama ni upuuzi huo? Tena mnatuma hata kwa mtu mwenye heshima zake, si atajihisi umemuona ni wa aina yako? Hivi sijui ni kwanini kuna watu hawajishtukii hata ukipotezea jumbe zao!

Kwa kweli kama bado unaandika kipumbavu hivyo ni bora ukaacha tu, na wale mnaokereka na watu wa aina hiyo ni vema mkapotezea mawasiliano yao kama hamuwezi kuwapa cha mbavu ili wajue wewe sio mpuuzi kama wao.
Ukiachia hizo..Mi uwa inanisumbua sana mwanaume kumwita mwanaume mwenzake WANGU
 
Kuandika xaxa badala ya sasa utakuwa umefupisha nini?
Sio hvo 'xaxa' ni mbwembwe/njonjo za vijana wa kileo.. Baadhi ya maneno wanayofupisha ni K-ok...P-poa.... Lkn-Lakini... Miss You - Mic u....Oyaaa- oi Niaje-aje...na kadhalika WANACHOFANYA NI KUDONDOSHA BAADHI YA VITAMKWA ILI KUPATA NENO FUPI ZAIDI
 
Back
Top Bottom