Huu ni ulimbukeni au utoto?

Wisest man

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
993
332
Kuna watu wanafedhehesha sana, tena wengine wakiwa ni watu wazima waliofika miaka 40 au zaidi huku wakiwa wanaandika hovyo wakati wa kutuma ujumbe hasa WhatsApp au hata sms za kawaida.

Mtu mzima unamtumia mwanaume mwenzako sms eti inasema "oi, xafi, vepee, xhwari nk! Hivi watu huwa hamuoni kama ni upuuzi huo? Tena mnatuma hata kwa mtu mwenye heshima zake, si atajihisi umemuona ni wa aina yako? Hivi sijui ni kwanini kuna watu hawajishtukii hata ukipotezea jumbe zao!

Kwa kweli kama bado unaandika kipumbavu hivyo ni bora ukaacha tu, na wale mnaokereka na watu wa aina hiyo ni vema mkapotezea mawasiliano yao kama hamuwezi kuwapa cha mbavu ili wajue wewe sio mpuuzi kama wao.
 
Mkuu watu kama haounapotezea tu, utapasuka kichwa kujali ya wapuuzi
 
Nadhani shida ipo katika kufupisha maneno ya kiswahili. Hatuna mfumo mzuri wa kufupisha maneno, hasa maneno marefu. Kuna lugha nafahamu wao wanafupisha maneno yao, na inakubalika kabisa kwenye jamii. Mf, neno "kiswahili" - "k-hili", "mtangazaji" - " mt-zaji"..etc. Na inawezekana lugha yetu hairuhusu kufupisha maneno, lakini kuandika xaxa, xo ...mmh
 
xaxa ni kifupi cha nini?
 
Back
Top Bottom