Huu ni ubabe au ulimbukeni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni ubabe au ulimbukeni.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by GAGL, Mar 30, 2011.

 1. G

  GAGL Senior Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nov 1884 - Feb 1885 ulifanyika mkutano jijini Berlin ukiongozwa na Otto Von Bismark akipendekeza kuligawa bara la Africa. Kuligawa bara la Africa hayakuwa matakwa ya Africa hata kidogo. Takribani miaka miaka 150 imepita tangu mkutano huu ufanyike ila cha ajabu bado hawa jamaa wana mawazo na mitazamo ya akina Bismark. Jana wamekaa huko ulaya wakiwemo na viongozi wa Afrika na Kiarabu, wakijadili muafaka wa Libya mpya huku wakianisha mambo ambayo walibya wanahitaji. Lakini hebu tuwaulize hawa jamaa. Je, ni kweli majority ya walibya hawamtaki Gaddaf? Je, UN, EU na USA ndo wanaofahamu wanayohitaji walibya zaidi ya walibya wenyewe hadi wafikie hatua ya kuwasemea? Je, kama walibya hawamtaki Gaddaf, hawamtaki kwa lipi? Kwa kuwa dikteta au kwa kukaa muda mrefu madarakani au kwa kushndwa kuwaletea maendeleo? Je, wanawafahamu wanaompinga Gadaf na wako tayari kuiongoza Libya? Je, walibya wako tayari kuongozwa na raisi mwingine? Nani aliyekusanya maoni kutoka kwa walibya kuwa hawamtaki Gadaf? Wakitujibu haya maswali bila shaka hata mkutano wa jana bila shaka ulikuwa na tija.
   
Loading...