HUU NDO USHAHIDI WIZI WA BENKI KUU YA TANZANIA ( BoT)

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
Hatimaye Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, amewasilisha ushahidi wa awali kwa Katibu wa Bunge, kuhusu tuhuma alizozitoa bungeni dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba, kwamba ni mmoja wa watuhumiwa katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya fedha uliofanywa katika Akaunti ya Malipo ya Nje (Epa) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).


Hatua hiyo imechukuliwa na Mnyika kutekeleza maelekezo aliyopewa na Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, ambaye alimpa siku saba kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kauli yake hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mnyika katika kikao cha Mkutano wa Bunge unaoendelea hivi sasa mjini hapa, kilichofanyika, Julai 3, mwaka huu, katika mjadala kuhusu makadirio ya mapato ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Siku hizo ziliisha juzi.

Kwa mujibu wa Mnyika, ushahidi huo aliuwasilisha kwa Katibu wa Bunge, mjini hapa juzi.

“Kuhusu tuhuma dhidi ya Mwigulu Nchemba, ushahidi wa awali nilishawasilisha leo (juzi) ndani ya siku saba kama ilivyotakiwa,” alisema Mnyika.

Katika mkutano huo uliotawaliwa na mvutano, malumbano, hisia kali na maneno ya kashfa miongoni mwa wabunge, Mnyika pamoja na mambo mengine, alisema Nchemba aliwahi kuwa mtumishi wa BoT, ambayo ilikumbwa na kashfa hiyo na kwamba, naye ni mmoja wa watuhumiwa.

Kauli hiyo ya Mnyika ilimfanya Mhagama kusimama na kumpa Mnyika siku hizo awe amewasilisha ushahidi wa kauli yake.

Kwa upande wake, Nchemba wakati akichangia mjadala wa Bunge, alisema alijiunga na BoT mwaka 2006 wakati huo ukwapuaji wa fedha BoT ulikwishafanyika.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
GUMZO LA JIJI: HUU NDO USHAHIDI WIZI WA BENKI KUU YA TANZANIA ( BoT)
 
kichwa cha habari kizuri, lakini habari yenyewe haionekani kulikoni? au ni kwa upande wangu tu!!!


Kama kweli hakuna kwanini kutuhadaa? kama ipo tueleweshe iko wapi?
 
Mnyika kwenye hili amechemka sana. Sio kila mtu anayefanya kazi au aliyefanya kazi BOT anahusika EPA.

EPA ilihusisisha watu wachache ndani ya BOT kwenye vitengo fulani fulani na sidhani kama huyu Mwigulu alikuwa na cheo chochote BOT. Mwisho mtasema na ma messengers na madereva wa BOT wamehusika!
 
saidieni huyo Blog yake ipate matangazo kwa japo siku moja ilipata visitors wengi. Yaani ameshindwa kuikopi hiyo stori aweke hapa hadi atulazimishe kwenda kwenye Blog!?
 
Uhakika zaidi anajua Mnyika,tumpe nafasi akajieleze hapo atakapoitwa ila tunataka spika atoe na ushahidi mbalimbali unapotolewa
 
Back
Top Bottom