Mm nilikashfiwa na mdada ambae nilizaa nae Mtoto na kunambia Sina hela, maana nilikua ndo nmemalza chuo cna hata ajira lakn kpind nipo nae mungu alibark tukapata Mtoto kiume, alitoa kila aina maneno, nmemchafua kumzalisha wakat bado Sina mbele na nyuma japo nilikua naweza kuhudumia kila kitu ila aliona Mtoto amemuharbia CV, maana wenzake aliona wanajirusha na maboss kila kukicha, ikafka muda hata ndg zake wakamshawishi aachane nami na awe na mtu Fulani alionesha nia na anaweza kulea hata Mtoto wangu bila mm ktoa chochote, bila woga binti akawa anatafta kila sababu tugombane, akataka anicontrol kama TV,nikaona upuuzi ikafkia kipnd akanipa mashart kwenda kuona Mtoto kwao licha yakuwa nahudumia,
Marafk zake wakanambia siku hz anatoka na boss Fulani ndo anamtia jeuri, nikamuulza nikatukanwa kila aina ya tusi, mi maskn, familia maskn, elimu na pesa kipi bora? Nile elimu yangu, nikitaka nichkue Mtoto ili nisimsumbue kwa lolote, kpnd hcho Mtoto anamiaka 2 tu, jamaa yake akampa namba Simu kanambia nisimsumbue, mjomba wake na ndg wengn wakanikashfu kupta kiasi niliumia sana aisee, hapo ndo nilijuta kwa kila kitu,
Familia yake ndo ilikua YA kawaida sana(maskn) kuliko hata yangu,
Nikapata kaz ya muda nikawa napata hela si chn 800k-1m kwa mwez, nikiwa bado na maumivu hayo! Nikajfanya mjnga nikapata upenyo kuiba Mtoto wangu, nikamchukua nikampeleka kw mama yangu(hapajui), akaona nmempunguzia mzgo, ikawa tena anakashfu hvohvo naktaka nimrudshie Mtoto wake ila sikufanya hivyo,
Akanitumia watu na police siku 1 aliponiona natoka uwanjani kuchek mechi ya ligi Kuu, nikashkwa nikawekwa ndani siku 2 na kesi yake ikawa nimemuibia Mtoto akiwa Mdogo, nikaomba kesi ipelekwe ustaw maana nilikua na SMS na audio ushahd kutaka nichkue Mtoto maana anambana,
Akaamua kufta kesi na ktamba eti ananikomesha, leo Mtoto anamiaka 4 hajawah hata kumuona, yule jamaa yake alikua mkurugenz h/mashauri fulan hv, kumbe anafamilia bwana, ikafka muda jamaa akamuacha tena kwa kashfa nakuitwa malayaaaaaa, akataka Kurd kwangu hata mawasiliano yake siktaka na staki na stataka, maana tayr anajua nimepata kaz permanent na Niko vzr,
Pia tayr nipo na mtu makn sana na sio muda mrefu nafunga ndoa, sasa imekua Simu haziishi kuomba msamaha nk, kaenda hadi kanisani kutubu na kumweleza mchungaj na akanipgia Simu kumuombea msamaha na nmpe nafasi hata kumuona Mtoto maana nae ni mzazi nikamjb mchungaj futa no yangu kabsa stak hzo habr, Mtoto akikua atamtafta mama yake,
Note; tuache kutendea mtu kibaya na kumkashfu huku huijui kesho, uktaka kumuacha mtu muache kimyakmya bila faraka! Mkiktana msalimiane hata kupasha kipolo pia, ukimuacha mtu kimyakmya hata umia sana kuliko kumkashfu, hujafa hujaumbka aisee!
Binafsi nilivoumia hata stak mtu anishaur chochote na mzaz mwenzangu, kaniachia Mtoto na anatapatapa kila kukicha, IWE MWANAUME AU MWANAMKE TUJIFUNZE KUTOKUMUUMIZA MTU KIMAPENZI, [emoji174] [emoji174] [emoji174] [emoji174] [emoji174] [emoji180] [emoji180] [emoji180] [emoji180] vigumu sana kuziba haya maumivu!