Huu ndiyo utaratibu wa kuondoa ukomo wa Urais kwenye katiba ya JMT ya 1977

Usha sema tayari watanzania wengi wanataka ukomo uondolewe, ni wazo zuri pia faida zipo na hasara zipo pia

Ila huyu ndo alikuwa na akili zaidi aliwaza mbali sana,
JamiiForums361028994.jpg
 
Kuondoa ukomo au kumuongezea Rais ukomo wa uongozi bila shaka unataka umakini wa hali ya juu, vinginevyo tunakaribisha shetani awe miongoni mwetu bila sababu ya msingi.

Kunahitajika kutumia fedha nyingi ambazo hatunazo kupiga kura ya kujua nani wanapenda na nani hawapendi. Wale wanaopenda ni kwanini na wale ambao hawapendi ni kwanini.

Mtu ambae ni mnufaika wa moja kwa moja hawezi kuwa chanzo cha kubadilisha Katiba ili aendelee kunufaika kupitia mabadiliko pendekezwa. Wazo la kuongeza, kupunguza au kubakiza vilevile ni swala la wananchi sio kikundi.
Rais huchaguliwa kila baada ya miaka 5.

Isitoshe Tanzania inaongozwa kwa demokrasia ya vyama vingi.

Kwa sababu hizo mbili uwezekano wa Rais kutawala milele ni mdogo kiasi cha takwa la kikatiba la ukomo wake kuwa halina mantiki.
 
Wakati wanaweka huo ukomo wewe uliombwa ushauri kwa njia ya kura?
Nchi wakati ule ilikuwa na mtu muadilifu kabisa na mwenye maono, mwl. Nyerere, Sasa hivi simuoni wa kufanana nae. Kama Jakaya, Mkapa na Mwinyi wangetaka pia kuongeza muda wa kubaki wangeweza lakini mbona waliondoka? Tuache ulevi ambao hata Rais JPM aliukataa upuuzi wa hivyo. Huko ni kuwafundisha panya kula sufi ya godoro, hatutabaki salama.

Njia sahihi Ni kuwa na taasisi imara zinazomlazimisha rais awe mchapakazi atake asitake.
 
Hiyo idadi itafikiwa maana hakuna uchaguzi, bali kuna kiini macho cha uchaguzi. Na tayari maagizo tume ya uchaguzi wameshapewa.
Kweli kabisa hamna uchaguzi ni kukamilisha ratiba tuu.Kichapo watakachopewa upinzni hawataamini watachakachuliwa balaa.
 
Kama ni hivyo, basi na wabunge na madiwani alioingia nao madarakani waachiwe nyadhifa zao maana inaonekana wamefanya kazi nzuri kwa kushirikiana nae, kusiwepo uchaguzi!.
Kwanza ni kutowandea haki watz, umasikini utaongezeka Sana, wasiojulikana watamaliza watu, waliobambikwa watasubiria Sana kukamilika kwa ushahidi,pia ni udumavu wa fikra means tz yote Hakuna madereva
 
.

Hivyo CCM ihakikishe tu inapata kuanzia aslilimia 67 ya wabunge kutoka pande zote mbili za muungano katika uchaguzi mkuu October 2020 ili waweze kumuongezea muda wa kutawala Mheshimiwa Sana Rais John Pombe Magufuli.

Suala la msingi siyo kumwongezea Magufuli muda wa kutawala. Kusema hivyo ni dhana potofu yenye harufu ya chuki kisiasa, kwani Katiba ya JMT(1977) imeweka ibara ambazo kimsingi zinatoa kikomo cha utawala wa Rais isipokuwa Ibara ya 40(2): Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais. Ibara hii kimantiki haina nguvu baada ya kurekebisha Katiba kwa kuwepo na Ibara zinazotoa ukomo wa Rais, nanukuu:-

Lakini kutokana na Ibara zifuatazo ni dhahiri kuwa uwezekano wa Rais kutawala milele ni mfinyu, hivyo hakuna sababu ya msingi kubadili Katiba, labda kama vyama vya upinzani vinakiri kuwa havitaweza kutawala nchi hii.

42(2): Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.

46A(1): Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

3(1): Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Ibara hii inatoa kikomo cha Urais pale ambapo vyama vya siasa vitakuwa vinabadilishana utawala wa nchi hii. Kinachohitajika ni kwa kila chama cha siasa kujiimarisha Kisera na Kiuongozi. Lakini uwepo wa migogoro ndani ya vyama, wa aina yoyote, kunavidhoofisha.
 
Suala la msingi siyo kumwongezea Magufuli muda wa kutawala. Kusema hivyo ni dhana potofu yenye harufu ya chuki kisiasa, kwani Katiba ya JMT(1977) imeweka ibara ambazo kimsingi zinatoa kikomo cha utawala wa Rais isipokuwa Ibara ya 40(2): Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais. Ibara hii kimantiki haina nguvu baada ya kurekebisha Katiba kwa kuwepo na Ibara zinazotoa ukomo wa Rais, nanukuu:-

Lakini kutokana na Ibara zifuatazo ni dhahiri kuwa uwezekano wa Rais kutawala milele ni mfinyu, hivyo hakuna sababu ya msingi kubadili Katiba, labda kama vyama vya upinzani vinakiri kuwa havitaweza kutawala nchi hii.

42(2): Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.

46A(1): Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

3(1): Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Ibara hii inatoa kikomo cha Urais pale ambapo vyama vya siasa vitakuwa vinabadilisha utawala wa nchi hii. Kinachohitajika ni kwa kila chama cha siasa kujiimarisha Kisera na Kiuongozi. Lakini uwepo wa migogoro ndani ya vyama, wa aina yoyote, kunavidhoofisha.
Uko sahihi, mtu anaposema tumuongezee muda anamaana kuwa lazima atashinda kwenye uchaguzi?. Itakuwaje Kama mnaondoa ukomo wa urais kisha mliyemkusudia aendelee akashindwa uchaguzi? Maana yake mtakuwa mmemuongezea muda mtu ambae hakukusudiwa. Au mlengwa lazima ashinde hata kwa bao la mkono?
 
Chadema huwa mnanikera Sana , Mimi Jana nilijua Hawa mashetani wa ccm wakiruhusiwa kwenda hospital wangeongea upuuzi na dharau. Issue wangezuiliwa getin au mgonjwa angekataza Hakuna kuonwa... Wenzenu wameshakuwa mashetani bado mnajipendekeza...

Wakimwaga mboga Nyie mwageni ugali. Ubaya ubaya tu.
hiko ndo ninachoshangaaa kwani mgonjwa si ana haki ya kukataaaa kuonwa na mtu wanaleta upendo kwa mashetani Ila nmefurahi kukaaaa kimya kwake kunazidi kuwapa shida
 
Ili kufanya mabadiliko ya kifungu cha katiba kinachohusiana na ofisi ya Urais wa JMT kwenye Cap 2 (URT Constitution of 1977), kinachohitajika ni Serikali kupeleka muswada bungeni kama miswada mingine wa kubadili kifungu tajwa. Isipokuwa tu kwenye upitishaji itahitajika theluthi mbili za wabunge kutoka bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar. Hii ni kwa mujibu wa article 98 ya Katiba (Cap 2, 1977) na Second schedule thereto.

Hivyo CCM ihakikishe tu inapata kuanzia aslilimia 67 ya wabunge kutoka pande zote mbili za muungano katika uchaguzi mkuu October 2020 ili waweze kumuongezea muda wa kutawala Mheshimiwa Sana Rais John Pombe Magufuli.

Kila la kheri chama cha mapinduzi!

Some tm tuwe tuna tafakari before kuleta mada.
 
Jana nilienda Dodoma,nikashukia stend mpya.Nimeshawishika kuwa JPM ni kiongozi ambae hatutampata Kama yeye hata 100 ijayo. Ni kweli huyu jamaa tumtumie hadi mwisho wa nguvu zake.
 
Back
Top Bottom