Naunga mkono hoja,Kuondoa ukomo au kumuongezea Rais ukomo wa uongozi bila shaka unataka umakini wa hali ya juu, vinginevyo tunakaribisha shetani awe miongoni mwetu bila sababu ya msingi.
Kunahitajika kutumia fedha nyingi ambazo hatunazo kupiga kura ya kujua nani wanapenda na nani hawapendi. Wale wanaopenda ni kwanini na wale ambao hawapendi ni kwanini.
Mtu ambae ni mnufaika wa moja kwa moja hawezi kuwa chanzo cha kubadilisha Katiba ili aendelee kunufaika kupitia mabadiliko pendekezwa. Wazo la kuongeza, kupunguza au kubakiza vilevile ni swala la wananchi sio kikundi.
Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.
5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.
6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.
7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.
8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.
Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.
Paskali
Naunga mkono hoja,
Hili la rais Magufuli kuongezewa muda, wengi ndio wanalisikia sasa, angalia hapa limependekezwa toka lini
Hili ni bandiko la 2015
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.
P
Kumbe Mangula nae ni kitambo eehKomandoo Salmin Amoor jitihada zake za kuongeza muda ziliishia Kizota Dodoma tena na akina Mangula hawa hawa, sijui kama huyu itawezekana
Kuondoa ukomo au kumuongezea Rais ukomo wa uongozi bila shaka unataka umakini wa hali ya juu, vinginevyo tunakaribisha shetani awe miongoni mwetu bila sababu ya msingi.
Kunahitajika kutumia fedha nyingi ambazo hatunazo kupiga kura ya kujua nani wanapenda na nani hawapendi. Wale wanaopenda ni kwanini na wale ambao hawapendi ni kwanini.
Mtu ambae ni mnufaika wa moja kwa moja hawezi kuwa chanzo cha kubadilisha Katiba ili aendelee kunufaika kupitia mabadiliko pendekezwa. Wazo la kuongeza, kupunguza au kubakiza vilevile ni swala la wananchi sio kikundi.
Tuanzie kwa kikwete akimaliza ukomo ndo amepewe yesu.kuanza na yesu sio hakiHii ishu sio tetesi tena chama cha kijani wako serious na utawala wa kifalme ila kwa uwezo wa Mungu mipango yao haitatimia.
Mpeleke kwa bi mdashi wako akamtawaleHuku field watu huwaambii kitu kuhusu Magufuli, na hao ndo majority na ndo wapiga kura.