Huu ndiyo utaratibu wa kuondoa ukomo wa Urais kwenye katiba ya JMT ya 1977

Ili kufanya mabadiliko ya kifungu cha katiba kinachohusiana na ofisi ya Urais wa JMT kwenye Cap 2 (URT Constitution of 1977), kinachohitajika ni Serikali kupeleka muswada bungeni kama miswada mingine wa kubadili kifungu tajwa. Isipokuwa tu kwenye upitishaji itahitajika theluthi mbili za wabunge kutoka bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar. Hii ni kwa mujibu wa article 98 ya Katiba (Cap 2, 1977) na Second schedule thereto.

Hivyo CCM ihakikishe tu inapata kuanzia aslilimia 67 ya wabunge kutoka pande zote mbili za muungano katika uchaguzi mkuu October 2020 ili waweze kumuongezea muda wa kutawala Mheshimiwa Sana Rais John Pombe Magufuli.

Kila la kheri chama cha mapinduzi!

Wajinga jinga Je akifa kesho itakuwaje!!. Wekeni mifumo imara Watu milioni 60 hatuezi kumtegemea mtu ambaye ana mashine kwenye moyo (Pace Maker) toka akiwa 35
 
Ili kufanya mabadiliko ya kifungu cha katiba kinachohusiana na ofisi ya Urais wa JMT kwenye Cap 2 (URT Constitution of 1977), kinachohitajika ni Serikali kupeleka muswada bungeni kama miswada mingine wa kubadili kifungu tajwa. Isipokuwa tu kwenye upitishaji itahitajika theluthi mbili za wabunge kutoka bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar. Hii ni kwa mujibu wa article 98 ya Katiba (Cap 2, 1977) na Second schedule thereto.

Hivyo CCM ihakikishe tu inapata kuanzia aslilimia 67 ya wabunge kutoka pande zote mbili za muungano katika uchaguzi mkuu October 2020 ili waweze kumuongezea muda wa kutawala Mheshimiwa Sana Rais John Pombe Magufuli.

Kila la kheri chama cha mapinduzi!

Kwa hiyo nia ya kuuwa upinzani ni kuondoa kikomo cha madaraka ya Raisi.
 
Kuondoa ukomo au kumuongezea Rais ukomo wa uongozi bila shaka unataka umakini wa hali ya juu, vinginevyo tunakaribisha shetani awe miongoni mwetu bila sababu ya msingi.

Kunahitajika kutumia fedha nyingi ambazo hatunazo kupiga kura ya kujua nani wanapenda na nani hawapendi. Wale wanaopenda ni kwanini na wale ambao hawapendi ni kwanini.

Mtu ambae ni mnufaika wa moja kwa moja hawezi kuwa chanzo cha kubadilisha Katiba ili aendelee kunufaika kupitia mabadiliko pendekezwa. Wazo la kuongeza, kupunguza au kubakiza vilevile ni swala la wananchi sio kikundi.
 
kavulata,

Bwana mdogo, utawala wowote ukizidi miaka 10 unaharibu yote yaliyojengwa miaka kumi ya kwanza. JPM anafanya mengi kwa future ya Tanzania ila akizidisha miaka 10 umangimeza unaanza mfano Mseveni, Kagame etc. cha msingi ni succession plan. Imagine JK angelikuwa sasa ni Rais, Wachina wangetutawala kama Angola au Zambia. Namkubali JPM ila kuongeza muda baada ya 2025 Big NO
 
Twende na hali hii hii ya kupokezana kijiti baada ta miaka kumi,madhara ya kubaki madarakani baada ya miaka 10 tutaharibu mfumo mzima wa utaratibu wa maisha ya kisiasa Tanzania, kuna siku nasi tutakuwa na waasi kama nchi jirani za maziwa makuu, yaani hata hayo maendeleo hayatakuwa na maana , maana amani itapotea,nampenda JPM,lakini miaka 10 ikiisha achape lapa.yeye sio Mungu,ni binadamu tu kama wengine,hana uspesho wa kuharibu mfumo wa maisha ya kizazi kijacho.
 
Bwana mdogo, utawala wowote ukizidi miaka 10 unaharibu yote yaliyojengwa miaka kumi ya kwanza. JPM anafanya mengi kwa future ya Tanzania ila akizidisha miaka 10 umangimeza unaanza mfano Mseveni, Kagame etc. cha msingi ni succession plan. Imagine JK angelikuwa sasa ni Rais, Wachina wangetutawala kama Angola au Zambia. Namkubali JPM ila kuongeza muda baada ya 2025 Big NO
Point! Suala jingine Kama katiba itabadilishwa kuondoa ukomo wa Magufuli jee rais atakayekuja baada ya Magufuli naye atakuwa Hana ukomo au katiba itabadilishwa Tena kwa ajili ya rais ajaye na kumuwekea ukomo?

Vp kuhusu rais wa CCM Zanzibar nae akidai asiwe na ukomo atakubaliwa au wazanzibar wao watakuwa wanaukomo JMT hakuna ukomo?
 
Back
Top Bottom