incredible terminator
JF-Expert Member
- Aug 1, 2016
- 2,533
- 4,290
HUU NDIO UKWELI AMBAO WATU WENGI WANAOGOPA KUSEMA.
Leo Ijumaa Kuu kwetu wakristo tunaiita ni siku ya kumbukizi ya Mateso kwa mwana wa Mungu.
Nami nimeona sio vibaya niseme maneno ambayo baadhi ya watu wanaogopa hata kuyasikia.
Lengo langu sio kuhimiza uasi wala ubaya ila napenda kusema ingependeza kila mtu aishi katika kile anachokiamini.
Lengo la maandiko yangu ni kuhimiza watu waache maigizo katika maisha yamkini wayafuate yale ambayo nafsi na mioyo yao inawasukuma kufanya pasipo kuwa na maigizo.
Kama unajijua wewe ni mtenda Mema basi ishi katika kutenda wema kila siku, kila dakika na kila saa, Tenda wema usiokusudia malipo.
Na kama wewe ni mtenda ubaya ishi katika ubaya, ishi katika visasi, ishi katika uovu ishi katika dhuluma, ishi katika ubinafsi uliotukuka! Acha kufanya maigizo ya kutenda wema fanya kile ambacho kinakupa furaha.
Lengo la kuyasema haya ni kukufungulia pasword ambayo Dunia ya mwanadam imemficha kumwambia ukweli.
1. HAKUNA SIKU ASILI ITAKULIPA JEMA KWA WEMA.
2. HAKUNA SIKU ASILI ITAKULIPA BAYA KWA UBAYA.
Hapa namaanisha kwamba kila jambo linalotokea katika maisha yako jua lilikuwepo katika mtililiko wa maisha yako.
Hakuna jambo litawahi kukutokea katika maisha yako kama matokeo ya Wema uliotenda au ubaya uliotenda.
Isipokuwa tu! Matokeo haya yanaweza kuonekana iwapo Ulimwengu utachukua hukumu ya matendo yako mfano ukitenda ubaya unaweza kushtakiwa kwa mjibu wa sheria za nchi uliyopo na ukaadhibika,
Vilevile ukitenda wema unaweza kulipwa wema na uliemtendea au mashahidi walioshuhudia wema wako.
Lakini tofauti na hapo Asili ya Dunia haijawai wala haitowahi ku repay chochote ulichowahi kufanya.
Wapo wengi wanaopitia mapito flani hadi mioyoni wanaanza kujihukujum kuwa pengine ni kwa sababu niliwahi kufanya kitu flani katika maisha ndio maana napitia haya... "Sio kweli"
Amini unachokipitia kilipaswa kikupitie ni mda wa wewe kupambana namna ya kujiokoa ila sio kukumbuka mapito yako.
Pia ukipata baraka amini ilipangwa utaipata isifikie mda ukaamini umebarikiwa kwa sababu ulijitoa kufanya jambo flani.. "sio kweli"
Sababu kuu ni kwamba wapo waliowahi kufanya wema au mazuri zaidi ya hilo ulilofanya wewe na hawajapata neema kama hiyo uliyopata wewe.
Pia wapo waliotenda maovu zaidi ya hayo yanayokusuta wewe hadi ukashindwa kusonga mbele ila bado wapo katika mstari ulionyooka na hakuna baya lolote lililowasibu na bado wanaishi vzuri sana.
Lengo langu sio kukufundisha wewe kutenda mabaya au kutenda wema.. no" Natamani tuwe na uwezo wa kuishi na kuitawala Dunia katika maisha yale yanayotupendeza wenyewe na sio kutawaliwa kifikra.