Huu ndio ‘uchawi’ unaopukutisha pesa zako

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
Wengi kati yetu wamejaribu kwenda kwa waganga kutafuta chanzo na pengine huko waliambiwa kuwa wanarogwa, wakagangwa kwa zindiko, lakini hali yao haijabadilika! Sasa kwa sababu saikolojia ni zaidi ya uchawi, leo nimeona ni bora nikafundisha kuhusu ‘uchawi’ wa kweli unaopokonya watu pesa zao na kuwaacha wakilalamika kuwa kipato ni kidogo.

Katika hali ya kawaida mchawi hasa wa pesa za wanadamu wengi ni ELIMU DUNI YA JINSI YA KUTUMIA PESA. Watu wengi wanafundishwa shuleni masomo mbalimbali na wanahitimu vyema, lakini wanapokuja katika uwanja wa maisha wanajikuta wanafeli vibaya kutokana na kutojua nidhamu ya pesa.

Wako madaktari, mainjinia na walimu wengi ambao wanapata pesa, lakini maisha yao ni duni kiasi kwamba wanazidiwa hata na watu ambao ni wauza dengu sokoni. Hii ina maana kuwa elimu ya darasani ni mbali na ile ya matumizi ya pesa binafsi.

Wataalam wa masuala ya pesa wanasema, ili mtu apate ziada katika pesa yake lazima awe na nidhamu ya matumizi. Sababu hii inatupa mbali dhana kwamba maendeleo yanataka wingi wa pesa. Dondoo zifuatazo zikizingatiwa hata mwenye kipato kidogo atapata ziada!

Tumia pesa taslimuKuna watu wengi sana wanaishi kwa kukopa kopa vitu madukani na kwa watu. Mtindo huu ni mbaya sana kwa ukadiriaji wa matumizi, kwani haumtii uchungu mkopaji hadi pale atakapokuwa analipa. Mara nyingi ukopaji huongeza gharama, hivyo inashauriwa ukiwa na 500 itumie hiyo, bila kutafuta ziada kwenye deni.

Panga mafungu madogo madogo ya bajeti
Katika maisha pendelea kupanga bajeti yako kwa mafungu madogo madogo hasa ya wiki. Usivuke mipango hiyo kwa kutumia bajeti ya wiki inayofuata.

Pendelea kukaa nyumbaniWatu wengi wanapenda kutembea tembea mitaani huku wakiwa na pesa nyingi mifukoni. Fahamu kuwa kutembea na pesa usizozipangia bajeti utajikuta unashawishika kuzitumia.

Hivyo unashauriwa kutulia nyumbani na kama utatoka siku za weekend ni vema mtoko huo uwe na bajeti, si kukurupuka tu na ‘mapesa’ yako na kujikuta uko baa au kwenye majumba ya starehe!

Nunua vitu kwa jumlaKama unataka kupata ziada katika kipato chako pendelea sana kununua vitu kwa jumla ambavyo utavitumia kwa mwezi mzima. Epuka kununua vipimo vidogo vidogo kwani vinaumiza na kuvuruga bajeti.

Pika chakula nyumbani kwakoWatu wengi hasa vijana wanapenda sana kula kwenye migahawa na hotelini. Ulaji huu ni ghali, hivyo inashauriwa kila mtu ajipikie chakula chake nyumbani. Hii itamsaidia kutumia pesa kidogo katika suala la chakula.

Ifundishe familia kubana matumizi Kuna watu hawawafundishi watoto na wake zao nidhamu ya matumizi ya pesa. Mume/mke asinunue vitu ambavyo familia haikuvitengea bajeti na asiwepo mtumia hovyo vitu vilivyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Mazoezi ni muhimuFamilia nyingi hazitilii mkazo suala la kufanya mazoezi, lakini wataalam wanasema ufanyaji wa mazoezi unajenga afya na hivyo kupunguza gharama za matibabu. Hii inakwenda sambamba na ulaji wa milo bora.

Akiba na mipangoFamilia lazima ijiwekee akiba benki. Utunzaji wa pesa nyumbani au mfukoni umebainika kuwa ni mgumu na mara nyingi hushawishi matumizi. Lakini sambamba na hilo la akiba lazima pesa zinazotunzwa zipangiwe malengo ya matumizi na malengo hayo yatimizwe kidogo kidogo si mpaka yasubiri pesa ziwe nyingi.

Upunguzaji wa familiaIngawa ni hali halisi ya maisha ya kiafrika kwa familia moja kuwa na watu wengi lakini inashauriwa kwamba, ili kupata ziada ya kipato lazima familia iwe ndogo, vinginevyo mshahara wote unaweza kutumika kwa chakula tu. Laa kama familia itakuwa ni kubwa basi kila mmoja afanye kazi ili uwepo usaidianaji wa kuendesha familia.
Yako mengi ya kujifunza katika somo hili asanteni.
 
BRAVO: Mada nzuri sana - inafaa kwa msomaji - Pamoja na kuiunga mkono mada hii napenda kuongezea yafuatayo:-
1) zingatia kuishi kulingana na kipato chako - usipende kupata vitu ambayo huna uwezo navyo -
2) nunua vitu unavyohitaji tu na si - vinginevyo - mfano una shati tatu nyeupe tayari, lakini ukiona ingine nyeupe unataka kununua - what for?? Au una mafuta ya kupaka tayari - unataka ununue mengine simply because you want to try another brand
3) usifanye mashindano ya kuvaa, kula katika maisha - watu wengine wana fedha nyingi ambazo hujui wanazipataje - kama ni mafisadi, au wana biashara haramu - you never know - jifunze kuridhika na kutumia kipato chako ipasavyo kwa kadri ya income yako.
4) Weka malengo - na upange vizuri hela unayopata utaitumiaje - kwa malengo hayo weka akiba kidogo kidogo - ili uwe na kianzio cha kufanya mradi - hata mdogo - siku moja utapanda tu.
5) Kwa wale wanaomcha Mungu - wasaidie maskini hasa yatima, toa sadaka na zaka - kwani Utajiri na heshima vyatoka kwa Mungu -
6) Acha kutumia fedha zako kwa vitu visivyofaa - e.g. ulevi, kujirusha kwani mwisho wa siku ni KUWEKA FEDHA ULIYO NAYO KWENYE MFUKO ULIOTOBOKA -
AGAIN - HONGERA KWA MTOA MADA YA KUELIMISHA JAMII
 
katika muda wote niliokaa darasani, leo ndio nimepata lecture itakayonifaa maishani, asante sana mkuu.
 
Hapa ndipo unapoithibitishia jamii kuwa we are the great thinkers,but you are not only a thinker but also a great teacher,mimi sijalishi wapi umeitoa hii article but mi nakubali kuwa wewe ni daktari mzuri kwa wanajamii,ukweli ni kwamba kwa hiki chakula ulichotoa leo kila atakae kionja basi atapata uponyaji,nashukuru sana mzizi mkavu,kwakuiokoa jamii nzima!!!
 
Mademu ni balaa ambayo hujaizungumzia. Unampa drinki na food etc poketi money something like 30- 40 thousand gone. Ukienda kuanguka nae ulipe room like 30- 40 again otherwise unaenda guest mshenzi za alfu 10. ukiweka na miscelenoeus unakuta kihadred thou kwishnei. Mimi mmm apana taka . fanya mara mbili kwa mwezi utajua penye demu bageti maana yake nini .
 
Mademu ni balaa ambayo hujaizungumzia. Unampa drinki na food etc poketi money something like 30- 40 thousand gone. Ukienda kuanguka nae ulipe room like 30- 40 again otherwise unaenda guest mshenzi za alfu 10. ukiweka na miscelenoeus unakuta kihadred thou kwishnei. Mimi mmm apana taka . fanya mara mbili kwa mwezi utajua penye demu bageti maana yake nini .


kula gwala mkuu,
uko sawa kabisa, tena kama yuko mkoani ndo balaa!, hapo mara umetoroka kazini. heeee siku umerudi asubuhi toka moro na hood imechelewa inabidi ukodi teksii ikukimbize kibaruani posta, utajuuuta.
icon10.gif
icon10.gif
 
Mti Mkavu yaani nimepata darasa la nguvu sana leo,BIG UP mkuu kwa hii post yaani nimejifunza kitu kipya leo.
 
Back
Top Bottom