Huu ndio msimamo wa J. Mnyika na posho

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,930
1,165
Msimamo wangu juu ya suala zima la Posho! Kufuatia habari tarehe 28 Novemba kuhusu ‘kupanda kimya kimya kwa posho za wabunge kwa zaidi ya asilimia 150' tarehe 29 Novemba 2011 nilitoa kauli yangu kama mbunge na katibu wa wabunge wa CHADEMA kuhusu suala husika.

Katika kauli hiyo nilieleza kuwa: "Wabunge wa CHADEMA hatujapokea taarifa rasmi kwamba masharti ya kazi ya ubunge yamebadilika na kwamba viwango vya posho vimeongezwa. Wala kamati ya wabunge wa CHADEMA haijawahi kuridhia ongezeko lolote la posho ya vikao (sitting allowance) kwa wabunge. Napenda kutumia fursa kusisitiza msimamo wetu wa kutaka posho za vikao (sitting allowance) ziweze kufutwa kwa wabunge na katika mfumo mzima wa malipo ya wakati wa kazi miongoni mwa watumishi wa umma".

Hivyo, kama mbunge na katibu wa wabunge wa CHADEMA nilitoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kwa niaba ya Serikali na Spika Anna Makinda kwa niaba ya Bunge kutoa kauli kuhusu suala hili ili kuondoa hisia zinazojengeka kwamba ‘wabunge wote tumekaa bungeni na kukubaliana kujiongezea posho ya vikao'. Kufuatia Spika Makinda kutoa kauli na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari tarehe leo tarehe 7 Novemba 2011 naomba kutoa msimamo wangu kama ifuatavyo: " Ongezeko la posho ya vikao lilofanyika linapaswa kusitishwa kwa kuwa limefanyika kinyume na taratibu na pia halina uhalali wowote kimantiki na halijazingatia uhalisia wa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla; nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni haramu (Illegitimate).

Bado narudia kutoa mwito kwa Rais Kikwete kutoa kauli wake na wa Ikulu na Ofisi ya Rais kwa ujumla unaacha ombwe lenye athari kubwa kwa serikali na kwa bunge mbele ya wananchi ambao kwa mujibu wa katiba ibara ya nane ndio wenye mamlaka na madaraka. Aidha, kauli ya Spika Makinda kwamba nyongeza hiyo ya posho za vikao ni kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha mkoani Dodoma haina ukweli, wala mantiki na ina mwelekeo wa upendeleo. Nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni matumizi mabaya ya madaraka na ni dharau kwa walipa kodi wanaohangaika na kupanda kwa gharama za maisha na athari za ubadhirifu wa fedha za umma.

Ni udhaifu kufikiri kwamba suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha ni kuongeza posho za kikao; tatizo la kupanda kwa gharama za maisha linapaswa kushughulikiwa kwa kuchukua hatua dhidi ya matatizo ya kiuchumi katika nchi ili kuweza kuwa na tija kwa wananchi wengi ambao ni waathirika zaidi wa kupanda kwa gharama za maisha kuliko wabunge. Pia, utetezi wa Spika Makinda kuhalalisha upandishaji wa kinyemela wa posho za vikao kwa wabunge haina maana kuwa kama sababu ingekuwa chanzo ni kupanda kwa gharama maisha ingepandishwa posho ya kujikimu (subsistence allowance) ambayo imebaki pale pale 80,000 .

Aidha kufuatia kauli ya Spika Makinda, hatua za kinidhamu zinapaswa zichukuliwe na Rais Kikwete dhidi ya Katibu wa Bunge Dr Thomas Kashilillah ya kutoa taarifa potofu kwa umma kwa kukanusha kwamba ofisi ya bunge haijaongeza posho kwa wabunge na pia kwa kufanya malipo kinyume na taratibu. Kugongana kwa kauli baina ya Spika na Katibu wa Bunge ni ishara ya kuwepo kwa jambo ambalo linafichwa kuhusu suala hilo la nyongeza haramu ya posho za vikao kwa wabunge na pia ni ushahidi wa taratibu kukiukwa hali ambayo inahitaji kauli kutoka kwa mwenye mamlaka kwa mujibu wa sheria kuhusu masuala ya posho za wabunge ambaye ni Rais.

Pia, katibu wa wabunge anapaswa kutuomba radhi wabunge kwa kauli yake kwamba mabadiliko ya posho za vikao yametokana na mkutano wa wabunge tarehe 8 Novemba 2011 kuiomba serikali ipandishe posho hizo za vikao.

Binafsi nilikuwepo kwenye mkutano huo wa tarehe 8 Novemba 2011 na hakuna uamuzi wowote ambao ulifikiwa wa kuiomba serikali ipandishe posho za vikao. Kilichotokea ni kwamba katika kuchangia maelezo ya serikali na ya bunge kuhusu masuala mbalimbali ya bunge na serikali yaliyojiri baada ya mkutano wa nne wa Bunge na mpangilio wa mkutano wa tano wa bunge, wabunge walipewa fursa ya kujadili taarifa hizo. Katika kujadili taarifa hizo wapo wabunge wachache waliotoka nje ya hoja za msingi na kuzungumzia kuhusu nyongeza ya posho ya vikao; hata hivyo mkutano huo wa wabunge haukufanya maamuzi yoyote na wala haukukamilika. Kabla ya majina yetu wengine kufikiwa kuweza kuchangia Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye kwa nafasi yake ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ni mwenyekiti wa mikutano ya wabunge alieleza kwamba muda umemalizika hivyo mkutano na kwamba tarehe nyingine ingepangwa kwa ajili ya kuendelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohojiwa na pia kuweza kutoa fursa kwa wabunge wengine kuweza kutoa maoni yao kuhusu masuala hayo. Katika hatua hiyo Waziri Mkuu Pinda alisoma majina yetu na kueleza kwamba mkutano huo wa wabunge ungeendelea katika tarehe nyingine lakini haukufanyika mkutano mwingine; hivyo katika mkutano wa tano wa bunge uliomalizika wabunge ambao mimi nilishiriki wabunge wote hatujawahi kukaa na kujipangia nyongeza ya posho za vikao kama inavyoelezwa hivi sasa wala.

Pia, wabunge hatujawahi kupatiwa nakala ya muktasari au kumbukumbu wa vikao vya kamati ya uongozi au vya tume ya bunge ambavyo vimekaa na kupitisha nyongeza ya posho ya vikao kutoka 70,000 mpaka 200,000 kama Spika alivyonukuliwa na vyombo vya habari. Ni muhimu watanzania wakazingatia kwamba mwenye mamlaka ya kupandisha posho za wabunge ni Rais na natoa mwito kwa Rais kukataa kupandisha posho za vikao kwa wabunge na badala yake azifute kabisa. Watumishi wote wa umma ikiwemo wabunge hatustahili kulipwa posho za kukaa kwenye vikao vyetu ambavyo mwisho wa mwezi tunalipwa mshahara kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Kufuatia hali hii, kwa kuwa sasa imeshatoka kauli rasmi ya bunge yenye kudhihirisha kwamba posho za vikao zimepandishwa kinyemela badala ya kufutwa kama tulivyotaka awali; tutaitisha kikao cha wabunge wa CHADEMA ili kukabaliana hatua za ziada za kuchukua kwa kuwa ofisi ya bunge na serikali wanaendelea kuingiza posho za vikao kwenye akaunti za wabunge hata baada za kuzipinga."

Katika kauli yangu ya tarehe 29 Novemba 2011 nilieleza kwamba ni vyema umma ukafahamu kwamba Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Administration Act) ya mwaka 2008 kifungu cha 19 kinataja aina ya posho ambazo zinaweza kutolewa kwa wabunge kama ambavyo Rais ataeleza kwa maandishi.

Katika kipengele (d) sheria imetaja orodha (i) mpaka (iii) ya posho ambazo wabunge wanastahili kulipwa za usafiri, kujikimu na wasaidizi. Katika orodha hiyo hakuna Posho ya Kikao (Sitting Allowance) ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja ambayo kamati ya wabunge wa CHADEMA tunataka ifutwe mara moja kama sehemu ya mchakato wa kubadili mfumo mzima wa malipo ya posho kwa watumishi wa umma.

Kifungu 19 (d) (iv) kimempa mamlaka Rais ya kutoa posho zingine kwa wabunge kwa kadiri atakavyoelekeza; kifungu hiki kimetoa mwanya wa kutolewa kwa waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais wa tarehe 25 Oktoba 2010 wenye kumbukumbu na. CAB111/338/01/83 masharti ya kazi ya mbunge ambao umeeleza viwango vya posho mbalimbali ikiwemo kutoa posho ya vikao (Sitting Allowance).

Hivyo, ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zinapaswa kuwaeleza watanzania iwapo waraka huo umebadilishwa na sababu za wabunge kutojulishwa kuhusu mabadiliko hayo. Aidha tarehe 29 Novemba 2011 nilieleza kuwa, iwapo mabadiliko hayo yamefanyika ni muhimu yakasitishwa kwa kuwa zitakwamisha utekelezaji wa mpango wa kufuta posho za vikao (sitting allowance) na kupunguza matumizi ya serikali kama ilivyoelezwa katika Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliopitishwa bungeni mwaka 2011.

Izingatiwe kwamba uchumi wa nchi hivi sasa unasuasua, serikali ina hali mbaya ya fedha kutokana na kupungua kwa kiwango cha fedha kinachopatikana katika kodi na washirika wa kimaendeleo ukilinganisha na mahitaji ya bajeti; na hivyo kukopa kibiashara kwa ajili ya kuziba nakisi iliyopo. Kupungua kwa uzalishaji, kiwango cha fedha pamoja na kuongezeka kwa ubadhirifu katika matumizi ya rasilimali za umma kunachangia katika mfumuko wa bei hali inayohitaji mpango wa dharura wa kunusuru uchumi wetu ukaohusisha pamoja na mambo mengine kubana matumizi ya serikali. "

Binafsi natarajia serikali ije kwetu wabunge na mpango wa kukabiliana na ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi badala ya kutuletea mpango wa kutuongezea wabunge posho za vikao huku mwelekeo wa uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo
ukiwa kwenye hali tete". Kamati ya wabunge wa CHADEMA ilikubaliana posho hizo zifutwe kwa kuwa Ilani ya CHADEMA ya mwaka

2010 imeeleza kwamba lengo la msingi ni kuondoa posho za vikao (sitting allowance ) hatua ambayo itaambatana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi, wajibu ili wafanyakazi walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki. Uamuzi huu ungewezesha pia kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo.

Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zizingatie kuwa Serikali ya CCM imeridhia msimamo huo na kuuingiza kwenye Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/2012-2015/2016 uliosainiwa na Rais Jakaya Kikwete tarehe 7 Juni 2011 ambao kwenye ukarasa wa 17 unatamka bayana kwamba posho za vikao na nyinginezo zinapaswa kufutwa au kuwianishwa hivyo kuziongeza ni kupuuza mpango huo.

J
ohn Mnyika (Mb) 07/12/2011
 
mh mnyika sikio la kufa halisikii dawa.ugiriki imefilisika hivi hivi,matumizi makubwa na madeni kwenye mabenki ya ndani.huko ndo nchi yetu inapoelekea.nchi haina hela za kujiendesha halaf tunaongeza matumizi.hatujifunz kutoka kwa wenzetu wagiriki?inakera na inauma sana.gharama za maisha zimepanda kwa kila mtu sio mbunge tu.bei juu kila kitu.madawa bei juu sana inabidi utafute hela kwanza ndio uamue kuumwa.balaa.
 
mie mtu anayepinga kitu uku anakipokea ananichanganya..... acheni kupokea posho ya vikao ili tuone kweli mna nia ya dhati na mnamaanisha mnachokisema.
 
Mfumo wa kupokea mishahara na posho kwa wabunge ni kupitia account za bank. Ingekuwa kama enzi hizo wanaenda ofisini kupokea cash au cheki ningekuelewa. Anachopata mbunge moja kwa moja ni pay check stub tu kuonyesha pesa zilizoingizwa kwenye account yake. Jaribu kufanya upembuzi njia wanazolipwa pesa hizo kabla ya kulaumu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

posho zinaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti together with mshahara.Ukigoma kusaini au usaini provided upo kikaoni hela inaingizwa sasa hapa pana tatizo la ziada manake akaunti za wabunge zimeorodheshwa
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hivi visingizio vya kwamba posho zinaingizwa kwenye akaunti moja kwa moja ndio sababu wanashindwa kukataa ni vya kipuuzi kabisa, mbona Zitto asiingiziwe kwanguvu kwenye akaunti yake hela za vikao vya posho? inawezekana kabisa nia ya dhati ikiwepo. Simple, wasi sign mahudhurio... mpaka hapo bunge litakaporekebisha mfumo mzima. No excuse, they should walk the talk

Mfumo wa kupokea mishahara na posho kwa wabunge ni kupitia account za bank. Ingekuwa kama enzi hizo wanaenda ofisini kupokea cash au cheki ningekuelewa. Anachopata mbunge moja kwa moja ni pay check stub tu kuonyesha pesa zilizoingizwa kwenye account yake. Jaribu kufanya upembuzi njia wanazolipwa pesa hizo kabla ya kulaumu.

posho zinaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti together with mshahara.Ukigoma kusaini au usaini provided upo kikaoni hela inaingizwa sasa hapa pana tatizo la ziada manake akaunti za wabunge zimeorodheshwa
 
Point of correction please sio msimamo wa Mh. J.J. Mnyika ni msimamo wa chama cha CHADEMA kwa ujumla wake ila umewakilishwa na Mh. Mnyika kama kaimu naibu katibu mkuu wa chama.

Now its time chadema waje wa strategic plan ya namna ya kujitoa ktk dhambi ya upokeaji hata kama wanapelekewa ktk akaunt zao ili kuonesha wanamaanisha basi watafute plan ya kuzikataa kabisa ikibidi wafungue kesi ya kupinga kuwekewa pesa kinyume na matakwa yao kama sheria inawaruhusu kufanya hivyo
 
Kaka mnyika tunahtj viongozi wa aina yako!2naomba wabunge wote hasa cdm muungane kututetea ss maskini na ktk hilo hat mnyezi mungu atawabariki!ccm wameamu wale hadi mbegu ili wakiangua wawaachie nchi ikiwa ktk hali mbaya! wameshajua kuwa mwisho wao ni 015 na hakuna wa kupinga hili!nawaomba sana wabunge w ccm waangalie maisha ya wtz wngn.

wengn wametokea kwenye msoto lkn hv ss wam2sahau
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Asante sana kamanda Mnyika kwa kazi hii nzuri.

Its so unfortunate corruption ya Tanzania inaanzia kwenye system ya uongozi. Wabunge wanakuwa corrupted kirahisi rahisi na serikali danganyifu ili wasiibane katika baadhi ya matendo yake kwani wanajua maisha yakibana kwa wabunge basi serikali nayo itabanwa ili iwajibike. Hii inatoa picha halisi ya nini mtazamo wa serikali kwa raia wa kawaida; kwamba wao hata waki buruzwaje hawezi ku-react kwani wengi hawajui hata kama umaskini wao uko directly linked to poor policies za serikali iliyoko madarakani.

Ninaiomba CHADEMA ipeleke ujumbe huu kwa raia kokote waliko kuwa rushwa inaweza kutolewa kwa njia nyingi na mojawapo ni hii ya kuwapa wawakilishi wao ili kuziba sauti zao kwani wanajua kama shida zinazowapata raia ndizo ambazo zinawapata wawakilishi wao basi sauti za raia zitasikika kupitia wawakilishi wao vinginevyo wawakilishi wakiishi maisha tofauti na rai basi hata shida za raia zitakuwa zinawahusu wao tu huku hao wawakilishi wakiendelea kushirikiana na serikali kuwaibia raia pesa zao.

Ni aibu iliyoje kwa watu wanaojiita wawakilishi wa raia kuhongwa kwa pishi la mchuzi na kuuza haki yao ya uzaliwa wa kwanza. Ninawalaani wabunge wote wapenda posho huku maelfu ya raia wakikosa chakula malazi na matibabu wakati huo huo wakishindwa kuibana serikali itimize wajibu wake kwa raia na badala yake wakishirikiana na serikali kuwaibia wananchi pesa zao za kodi kwa manufaa yao binafsi na si kuleta maendeleo ya nchi.
 
nawachukia wabunge wa ccm kwa roho mbaya na kujali chama chao nakuweka masirahi ya chama mbele.Bila kukumbuka kabunge ama mwajili wao ni mwananchi. leo hii mbunge analalamika posho ndogo hakumbuki kwamba mpiga kura wake hata mlo kutwa hajui ataupata wapi Hivi tukisema wabunge mpo kwa ajili yenu na familia zenu tutakua tumikosea.Sasa mnajaribu kutufitisha na wabunge wetu wenye dhamila ya dhati ili tuone kwamba wabunge wote hawafai.Sisi wananchi wabunge gani wapo kwa ajili ya kututetea na wabunge gani wapo kwa masirahi ya chama. Inaniuma sana kuona mwashimiwa anapokea sh mil saba bado anaona ndogo harafu kuna mfannyakazi mwengine anapokea sh lak moja na nusu inabidi watoto shule apate nauli ya kwenda kazin na hela kula hapo hapo mbunge kweli una huruma na huyu mpiga kura wako. Ifike muda muwe na huruma na hawa masikini.Kama ghalama za maishs zimepanda kwa nyinyi waheshimia mkumbuke raia wakawaida ndiyo zaidi. Nani atawasemea hawa wananchi masikini ikiwa hata nyinyi wabunge ambao waliweka matumini kwenu mnawasaliti. Sheria mbovu mnazipitisha nakusahau kuwa zinawakanda wajomba zako shangazi zako shemeji zako wapwa zako na umesahau kwamba ubunge sio kiti cha milele ipo siku utakuwa raia wa kawaida.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Point of correction please sio msimamo wa Mh. J.J. Mnyika ni msimamo wa chama cha CHADEMA kwa ujumla wake ila umewakilishwa na Mh. Mnyika kama kaimu naibu katibu mkuu wa chama.

Now its time chadema waje wa strategic plan ya namna ya kujitoa ktk dhambi ya upokeaji hata kama wanapelekewa ktk akaunt zao ili kuonesha wanamaanisha basi watafute plan ya kuzikataa kabisa ikibidi wafungue kesi ya kupinga kuwekewa pesa kinyume na matakwa yao kama sheria inawaruhusu kufanya hivyo

If there is a political will there is a positive way of using such amount to get rid of this terrible government (kwaku inua maisha ya raia) which never listen to the cry of the commoners kwa kuonyesha jinsi umaskini ni product ya policy mbaya na matumizi mabovu ya tax payers money na jinsi CHADEMA can make a difference.
 
Hawa wabunge wasiwe vigeugeu someni hii

Posho, mishahara yaibuka tena bungeni Send to a friend
Wednesday, 09 November 2011 22:00
0digg

Neville Meena, Dodoma
SUALA la maslahi ya wabunge jana liliibuka tena wakati wabunge walipokutana kupewa maelekezo kuhusu mkutano wa tano, huku wabunge wa CCM na wale wa upinzani wakionekana kuwa na kauli moja ya kudai maslahi zaidi.Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika takriban kwa saa tatu, zinasema suala la maslahi ya wabunge lilichukua sehemu kubwa ya mjadala ndani ya kikao hicho, huku baadhi ya wabunge wakitaka kupuuzwa kwa wenzao wanaopinga posho hizo.

Hivi sasa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh2.3 milioni kabla ya kukatwa kodi, kiwango ambacho wanadai hakilingani na kazi wanazofanya na kwamba, kiwango hicho kimepitwa na wakati kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

“Kiwango cha mshahara tunaolipwa sasa kiliwekwa muda mrefu na inawezekana wakati huo kilikuwa kikitosheleza, lakini kimebakia hapo kwa muda mrefu licha ya watumishi wengine viwango vyao kubadilika, sasa tunadhani ni wakati mwafaka jambo hili kufikiriwa,” alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria kikao hicho.

“Hapa nina mialiko 26 ya kwenda kuchangia ujenzi wa shule na shughuli nyingine za maendeleo kule Rombo, zote hizi zinanihitaji kama mbunge nitoe fedha, sasa jamani fedha hizi zinatoka wapi,?” chanzo chetu kilimnukuu mbunge huyo akihoji na kuungwa mkono na wabunge wengi.

Chanzo hicho kilisema Selasini alieleza jinsi ambavyo wabunge hukutana na kero ya wananchi kuomba fedha ili wakatatue matatizo yao mbalimbali nakwamba ni vigumu kukwepa jukumu hilo kutokana na hali ya maisha ilivyo sasa nchini.

Wabunge wengine waliochangia suala hilo ni Mbunge wa Mbulu (Chadema), Mustafa Akunaay, ambaye alimuunga mkono Selasini akisema malipo ya mbunge hayalingani na wajibu wake kwa umma.

Mbunge huyo alinukuliwa akisema wabunge ambao wamekuwa wakipinga posho wanazopewa huenda wana vyanzo vingine vya fedha ambavyo wanavitegemea.

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde, yeye alinukuliwa akiitaka Ofisi ya Spika, Anne Makinda, kufanya jitihada za kuwaelimisha wananchi kuhusu wajibu wa mbunge ili wafahamu kazi nyingine wanazofanya wawakilishi hao wa wananchi ni nyongeza nje ya majukumu yao ya msingi.

“Malipo yetu ni kidogo sana, hayatoshelezi kabisa lakini wananchi tunaowawakilisha hawatuelewi katika hili, maana wanadhani tuna fedha nyingi, sasa hapa kuna tatizo. Nadhani kuwapo utaratibu wa kuwaelimisha, wajue hata kazi nyingine tunazofanya siyo wajibu wetu ila tunajitolea na nyingine hizi zina gharama kubwa,” alinukuliwa Lusinde.

Wabunge wengine waliochangia hoja hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, walisema suala la maslahi yao halipaswi kujadiliwa na wao, kwani Serikali ina wajibu wa kuona haja ya wabunge kuongezewa fedha kutokana na majukumu waliyonayo.
Habari ambazo Mwananchi lilizipata zilimnukuu Spika Makinda akisema suala hilo litafikishwa kwa wahusika kupitia Tume ya Huduma za Bunge, ili liweze kufanyiwa kazi.

Spika kwa mujibu wa taarifa hizo naye aliwalaumu baadhi ya wabunge ambao wamekuwa vinara wa kutangaza kuwa maslahi ya wabunge ni makubwa, ilhali wakifahamu fedha hizo ni kidogo hasa ikilinganishwa na wabunge wa nchi jirani.

Suala la malipo hasa ya posho liliibuka wakati wa Mkutano wa Bunge la Bajeti mwaka huu, hoja ambayo chimbuko lake lilikuwa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ambaye alisusia posho za vikao kwa kutokusaini karatasi za mahudhurio. Hoja hiyo ya Zitto iliungwa mkono na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ambaye alisema suala hilo lilipaswa kupewa mtizamo mpana wa kitaifa na kuitaka Serikali kufuta posho zote za vikao na badala yake kuboresha mishahara ya watumishi wa umma wakiwamo wabunge.
Source: Mwananchi
 
Hawa wabunge wasiwe vigeugeu someni hii

Posho, mishahara yaibuka tena bungeni
Send to a friend

Nimeshangazwa na post hii, "msimamo wa mnyika" wengine wanasema ni msimamo wa Chama cha silaha a.k.a chama cha wachaga! huku wabunge wao "selasini" , "akunay" na shibuda kama sikosei wote wanaitaka kwa nguvu posho na wanadiriki kusema kuwa wana mialiko mingi, je ruzuku maeneo haya haipelekwi? ! sasa mbona mnatuchanganya? nitaanza kuamini siku nitakaposikia magazeti ya ukweli yametangaza na vithibitisho kuwa chakudema wamekataa posho na ushahidi! msituletee longo longo hapa TOENI UPUUZI WENU!
 
Msimamo wangu juu ya suala zima la Posho! Kufuatia habari tarehe 28 Novemba kuhusu ‘kupanda kimya kimya kwa posho za wabunge kwa zaidi ya asilimia 150' tarehe 29 Novemba 2011 nilitoa kauli yangu kama mbunge na katibu wa wabunge wa CHADEMA kuhusu suala husika.

Katika kauli hiyo nilieleza kuwa: "Wabunge wa CHADEMA hatujapokea taarifa rasmi kwamba masharti ya kazi ya ubunge yamebadilika na kwamba viwango vya posho vimeongezwa. Wala kamati ya wabunge wa CHADEMA haijawahi kuridhia ongezeko lolote la posho ya vikao (sitting allowance) kwa wabunge. Napenda kutumia fursa kusisitiza msimamo wetu wa kutaka posho za vikao (sitting allowance) ziweze kufutwa kwa wabunge na katika mfumo mzima wa malipo ya wakati wa kazi miongoni mwa watumishi wa umma".

Hivyo, kama mbunge na katibu wa wabunge wa CHADEMA nilitoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kwa niaba ya Serikali na Spika Anna Makinda kwa niaba ya Bunge kutoa kauli kuhusu suala hili ili kuondoa hisia zinazojengeka kwamba ‘wabunge wote tumekaa bungeni na kukubaliana kujiongezea posho ya vikao'. Kufuatia Spika Makinda kutoa kauli na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari tarehe leo tarehe 7 Novemba 2011 naomba kutoa msimamo wangu kama ifuatavyo: " Ongezeko la posho ya vikao lilofanyika linapaswa kusitishwa kwa kuwa limefanyika kinyume na taratibu na pia halina uhalali wowote kimantiki na halijazingatia uhalisia wa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla; nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni haramu (Illegitimate).

Bado narudia kutoa mwito kwa Rais Kikwete kutoa kauli wake na wa Ikulu na Ofisi ya Rais kwa ujumla unaacha ombwe lenye athari kubwa kwa serikali na kwa bunge mbele ya wananchi ambao kwa mujibu wa katiba ibara ya nane ndio wenye mamlaka na madaraka. Aidha, kauli ya Spika Makinda kwamba nyongeza hiyo ya posho za vikao ni kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha mkoani Dodoma haina ukweli, wala mantiki na ina mwelekeo wa upendeleo. Nyongeza hiyo ya posho ya vikao ni matumizi mabaya ya madaraka na ni dharau kwa walipa kodi wanaohangaika na kupanda kwa gharama za maisha na athari za ubadhirifu wa fedha za umma.

Ni udhaifu kufikiri kwamba suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha ni kuongeza posho za kikao; tatizo la kupanda kwa gharama za maisha linapaswa kushughulikiwa kwa kuchukua hatua dhidi ya matatizo ya kiuchumi katika nchi ili kuweza kuwa na tija kwa wananchi wengi ambao ni waathirika zaidi wa kupanda kwa gharama za maisha kuliko wabunge. Pia, utetezi wa Spika Makinda kuhalalisha upandishaji wa kinyemela wa posho za vikao kwa wabunge haina maana kuwa kama sababu ingekuwa chanzo ni kupanda kwa gharama maisha ingepandishwa posho ya kujikimu (subsistence allowance) ambayo imebaki pale pale 80,000 .

Aidha kufuatia kauli ya Spika Makinda, hatua za kinidhamu zinapaswa zichukuliwe na Rais Kikwete dhidi ya Katibu wa Bunge Dr Thomas Kashilillah ya kutoa taarifa potofu kwa umma kwa kukanusha kwamba ofisi ya bunge haijaongeza posho kwa wabunge na pia kwa kufanya malipo kinyume na taratibu. Kugongana kwa kauli baina ya Spika na Katibu wa Bunge ni ishara ya kuwepo kwa jambo ambalo linafichwa kuhusu suala hilo la nyongeza haramu ya posho za vikao kwa wabunge na pia ni ushahidi wa taratibu kukiukwa hali ambayo inahitaji kauli kutoka kwa mwenye mamlaka kwa mujibu wa sheria kuhusu masuala ya posho za wabunge ambaye ni Rais.

Pia, katibu wa wabunge anapaswa kutuomba radhi wabunge kwa kauli yake kwamba mabadiliko ya posho za vikao yametokana na mkutano wa wabunge tarehe 8 Novemba 2011 kuiomba serikali ipandishe posho hizo za vikao.

Binafsi nilikuwepo kwenye mkutano huo wa tarehe 8 Novemba 2011 na hakuna uamuzi wowote ambao ulifikiwa wa kuiomba serikali ipandishe posho za vikao. Kilichotokea ni kwamba katika kuchangia maelezo ya serikali na ya bunge kuhusu masuala mbalimbali ya bunge na serikali yaliyojiri baada ya mkutano wa nne wa Bunge na mpangilio wa mkutano wa tano wa bunge, wabunge walipewa fursa ya kujadili taarifa hizo. Katika kujadili taarifa hizo wapo wabunge wachache waliotoka nje ya hoja za msingi na kuzungumzia kuhusu nyongeza ya posho ya vikao; hata hivyo mkutano huo wa wabunge haukufanya maamuzi yoyote na wala haukukamilika. Kabla ya majina yetu wengine kufikiwa kuweza kuchangia Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye kwa nafasi yake ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ni mwenyekiti wa mikutano ya wabunge alieleza kwamba muda umemalizika hivyo mkutano na kwamba tarehe nyingine ingepangwa kwa ajili ya kuendelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohojiwa na pia kuweza kutoa fursa kwa wabunge wengine kuweza kutoa maoni yao kuhusu masuala hayo. Katika hatua hiyo Waziri Mkuu Pinda alisoma majina yetu na kueleza kwamba mkutano huo wa wabunge ungeendelea katika tarehe nyingine lakini haukufanyika mkutano mwingine; hivyo katika mkutano wa tano wa bunge uliomalizika wabunge ambao mimi nilishiriki wabunge wote hatujawahi kukaa na kujipangia nyongeza ya posho za vikao kama inavyoelezwa hivi sasa wala.

Pia, wabunge hatujawahi kupatiwa nakala ya muktasari au kumbukumbu wa vikao vya kamati ya uongozi au vya tume ya bunge ambavyo vimekaa na kupitisha nyongeza ya posho ya vikao kutoka 70,000 mpaka 200,000 kama Spika alivyonukuliwa na vyombo vya habari. Ni muhimu watanzania wakazingatia kwamba mwenye mamlaka ya kupandisha posho za wabunge ni Rais na natoa mwito kwa Rais kukataa kupandisha posho za vikao kwa wabunge na badala yake azifute kabisa. Watumishi wote wa umma ikiwemo wabunge hatustahili kulipwa posho za kukaa kwenye vikao vyetu ambavyo mwisho wa mwezi tunalipwa mshahara kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Kufuatia hali hii, kwa kuwa sasa imeshatoka kauli rasmi ya bunge yenye kudhihirisha kwamba posho za vikao zimepandishwa kinyemela badala ya kufutwa kama tulivyotaka awali; tutaitisha kikao cha wabunge wa CHADEMA ili kukabaliana hatua za ziada za kuchukua kwa kuwa ofisi ya bunge na serikali wanaendelea kuingiza posho za vikao kwenye akaunti za wabunge hata baada za kuzipinga."

Katika kauli yangu ya tarehe 29 Novemba 2011 nilieleza kwamba ni vyema umma ukafahamu kwamba Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Administration Act) ya mwaka 2008 kifungu cha 19 kinataja aina ya posho ambazo zinaweza kutolewa kwa wabunge kama ambavyo Rais ataeleza kwa maandishi.

Katika kipengele (d) sheria imetaja orodha (i) mpaka (iii) ya posho ambazo wabunge wanastahili kulipwa za usafiri, kujikimu na wasaidizi. Katika orodha hiyo hakuna Posho ya Kikao (Sitting Allowance) ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja ambayo kamati ya wabunge wa CHADEMA tunataka ifutwe mara moja kama sehemu ya mchakato wa kubadili mfumo mzima wa malipo ya posho kwa watumishi wa umma.

Kifungu 19 (d) (iv) kimempa mamlaka Rais ya kutoa posho zingine kwa wabunge kwa kadiri atakavyoelekeza; kifungu hiki kimetoa mwanya wa kutolewa kwa waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais wa tarehe 25 Oktoba 2010 wenye kumbukumbu na. CAB111/338/01/83 masharti ya kazi ya mbunge ambao umeeleza viwango vya posho mbalimbali ikiwemo kutoa posho ya vikao (Sitting Allowance).

Hivyo, ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zinapaswa kuwaeleza watanzania iwapo waraka huo umebadilishwa na sababu za wabunge kutojulishwa kuhusu mabadiliko hayo. Aidha tarehe 29 Novemba 2011 nilieleza kuwa, iwapo mabadiliko hayo yamefanyika ni muhimu yakasitishwa kwa kuwa zitakwamisha utekelezaji wa mpango wa kufuta posho za vikao (sitting allowance) na kupunguza matumizi ya serikali kama ilivyoelezwa katika Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliopitishwa bungeni mwaka 2011.

Izingatiwe kwamba uchumi wa nchi hivi sasa unasuasua, serikali ina hali mbaya ya fedha kutokana na kupungua kwa kiwango cha fedha kinachopatikana katika kodi na washirika wa kimaendeleo ukilinganisha na mahitaji ya bajeti; na hivyo kukopa kibiashara kwa ajili ya kuziba nakisi iliyopo. Kupungua kwa uzalishaji, kiwango cha fedha pamoja na kuongezeka kwa ubadhirifu katika matumizi ya rasilimali za umma kunachangia katika mfumuko wa bei hali inayohitaji mpango wa dharura wa kunusuru uchumi wetu ukaohusisha pamoja na mambo mengine kubana matumizi ya serikali. "

Binafsi natarajia serikali ije kwetu wabunge na mpango wa kukabiliana na ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi badala ya kutuletea mpango wa kutuongezea wabunge posho za vikao huku mwelekeo wa uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo
ukiwa kwenye hali tete". Kamati ya wabunge wa CHADEMA ilikubaliana posho hizo zifutwe kwa kuwa Ilani ya CHADEMA ya mwaka

2010 imeeleza kwamba lengo la msingi ni kuondoa posho za vikao (sitting allowance ) hatua ambayo itaambatana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi, wajibu ili wafanyakazi walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki. Uamuzi huu ungewezesha pia kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo.

Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zizingatie kuwa Serikali ya CCM imeridhia msimamo huo na kuuingiza kwenye Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/2012-2015/2016 uliosainiwa na Rais Jakaya Kikwete tarehe 7 Juni 2011 ambao kwenye ukarasa wa 17 unatamka bayana kwamba posho za vikao na nyinginezo zinapaswa kufutwa au kuwianishwa hivyo kuziongeza ni kupuuza mpango huo.

J
ohn Mnyika (Mb) 07/12/2011

Craaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapo ! kamwambie maneno haya Shibuda, Selasini na wengineo uone km hawakukukamua macho !

Naomba kuuliza..hivi hatuwezi kuwafunga gavana hawa? Wanakimbia sana,hebu nambieni eWURA yao inaitwaje iwadhibiti
 
Uongozi wa bunge pamoja na wabunge walio wengi wamepoteza kabisa heshima na maana halisi ya uwakilishi wa wananchi.
Kwa hali ilivyo, bunge limekuwa kusanyiko la wanyonyaji, walafi wa kijinga wasiojua hata wajibu wao, wanaoongozwa kipuuzi.
Haivumiliki kuona spika na katibu wa bunge wakiongelea suala la posho kijingajinga namna hiyo. Labda vichwani mwao hakuna kitu na sijui walipata vipi hizo nafasi zao.
Kuna haja ya kuangalia namna tunavyowapata wabunge na viongozi wengine kwani kwa hali ilivyo sasa hivi, wajinga na hata wapumbavu wengi ndiyo wanaoshikilia ofisi nyingi za uma!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
mie mtu anayepinga kitu uku anakipokea ananichanganya..... acheni kupokea posho ya vikao ili tuone kweli mna nia ya dhati na mnamaanisha mnachokisema.
Kwa jinsi ninavoelewa hizi posho zinawekwa kwenye a/c ya mbunge pasipo kumwambia. Anakutana nazo benki iwe ameridhia au hajaridhia.
 
Binafsi napendekeza Wabunge wawe wanalipwa mshahara wa kima cha chini bila posho yoyote ili wawe na akili ya kuisimamia serikali!!!
 
Mbunge wangu Mnyika nakuamini na kukuheshimu sana nakuomba muangakie upya hili swala la kupokea posho na mzikatae kwa vitendo sio maneno tu kila siku halafu mnatwambia haziepukiki mradi tu umesaini daftari la mahudurio
 
mbunge wangu Mh. Highness wa CHADEMA jimbo la Ilemela,naomba useme lolote kuhusu nyongeza ya posho hizi. Nakufahamu sana,hupendi makuu,unavaa simple,gari lako simple,utawezaje kukubali wizi huu?
 
Back
Top Bottom