Huu mwaka 2023 kuna watu bado wanamsikiliza Issa Shivji?

Umesema vitu jumuishi bila kurejea vifungu alizosema Shivji...wewe utakuwa mnufaika wa DPW
Kakopi sehemu hilo andiko, nimesoma kwa paragraph kadhaa sioni mahali anaandika kuainisha mjadara wa Prof. Shivji.

Although kapewa au kakopi aweke hapa JF.
 
Kak Huna taarifa kuwa ktk kitabu Cha mkapa binafsi alikiri kuwa alifanya makosa ktk ubinafisishaji wa mashirika ya umma leo umekuja Tena unataka bandari apewe muarabu
 
Hayo anayojutia Mkapa kwenye kitabu chake haudhani kwamba we're repeating he same mistakes? Kwamba kwa huu uwekezaji Samia in the near future hawezi kuja na same stories?
Mkuu mimi sio mwanasheria ila Nina uzoefu na Bandari kwenye kampuni Binafsi, hata zilipokuja Habari za Ticts kuondolewa hata kabla ya mambo ya Dpworld kuja nilishauri watafute mtu mwengine mbadala wa Ticts.

Bandari sio madini kwamba utaibiwa ama Bandari itaisha, uendeshaji wake ni wa Ki pekee. Leo Dp akija akachimba kina kirefu cha bandari siku wakiondoka hawezi kuondoka na Kina chake ataacha vile vile, akijenga miundombinu vile vile.

Bandari Wakusanya mapato ni wale wale Tra, Dp haji kukusanya mapato,

Na Dp kwa interest zao ili wapate mapato zaidi inabidi meli nyingi zaidi zije, zipakuliwe haraka zaidi, Jinsi makontena mengi yanavyopita kwao ndio jinsi watakavyopata hela nyingi, hii interest yao inakuwa neema pia kwetu jinsi makontena mengi yatakavyopita ndio jinsi Ushuru mwingi na kodi utakavyokusanywa.

Turudi kwa Mkapa Alichojutia kikubwa kwenye Kitabu chake ni Hicho wawekezaji kung'oa miundombinu ya viwanda ama Uwekezaji wao na kwenda kutumia kwa maslahi yao Binafsi badala ya maslahi ya Taifa kwa ujumla, Hebu tu relate kwa Dp world, Wakija Kuna Risk ya kutoa crane zetu kuu kuu na kuziiba? Ama wataleta zao za Kisasa?

Kwanini tunawaogopa? Kama ni Bandari ilibinafaishwa toka mwaka 2000 kwa Ticts kampuni ya kina Karamagi, kuna nini Dp world Wakija wataharibu na Ticts walikua wakifanya Vyema?
 
AMEANDIKA MALISA GJ

#TimuYaWananchi
1. Profesa Anne Tibaijuka (Waziri Mstaafu, Mkurugenzi wa zamani UN Habitat, Mhadhiri mstaafu vyuo vikuu mbalimbali)
2. Profesa Issa Shivji (Nguli wa Sheria, Mwanamajumui wa Afrika, Mwanazuoni)
3. Tundu Lissu (Wakili Msomi, Mwanasiasa hodari, Rais mstaafu wa TLS)
4. Dr.Rugemezela Nshala (Wakili Msomi, Rais Mstaafu wa TLS, Mwalimu wa Law School aliyemfundisha Tulia Akson)
5. Dr.Charles Kitima (Katibu mkuu TEC, Mwanazuoni hodari, VC mstaafu Chuo kikuu SAUT)
6. Dr.Fredrick Shoo (Mkuu wa KKKT, Mhadhiri mstaafu vyuo vikuu mbalimbali, Mwanazuoni)
7. Sheikh Abubakar Zubeir (Sheikh Mkuu Tanzania, Mwanazuoni)
8. Freeman Mbowe (Mwanasiasa mbobevu, Mwenyekiti Chadema)
9. Jaji Joseph Sinde Warioba (Waziri Mkuu mstaafu, Jaji mstaafu, Mwanamajumui wa Afrika)
10. Dr.Wilbroad Slaa (Mwanasiasa Nguli, Balozi mstaafu, Katibu mkuu mstaafu Baraza la Maaskofu, katibu mkuu wa zamani Chadema).

#TimuYaMakasuku
1. Baba Levo (Chawa Mwandamizi)
2. Mwijaku (Chawa mwandamizi daraja la kwanza)
3. Zembwela (Msanii wa Futuhi aliyevamia taaluma ya habari)
4. Hando (Mwandishi aliyeamua kuharibu heshima yake ili kujaza utumbo mpana)
5. Kitenge (Dalali Mwandamizi daraja la kwanza)
6. Isaa Azam (Mtuhumiwa wa upinde)
7. Sophia(ni) Juma (Mtuhumiwa wa upinde)
8. Tivu ake (Msanii wa Futuhi)
9. Msukuma (darasa la 7 anayeamuni ana PhD bila kwenda darasani)
10. Kibajaji (Kepteni wa timu ya kusifu watawala ili kushibisha utumbo mpana)

Mechi ni dakika ya 25 kipindi cha kwanza, Timu ya Wananchi inaongoza bao 3 bila. Ukipenda sema tatu sifuri, au tatu nunge, au tatu yai, au tatu duara, au tatu bashite. Ngoma bado mbichi hii, hata half time bado.!
TimuYaWananchi!watu 10 out of 60 milioni raia.

10/60000000=1/6000000=0.0000166666%.

Ni ujinga kuamini kwamba watu asilimia 0.00001667 ya raia wote,ndiyo watushawishi kukataa makubaliano ya uwekezaji yaliyopitishwa na raia takribani asilimia 99.9999 huko,wakiwakilishwa na wabunge na serikali yao!?.
Endeleeni kupiga kelele za chura.
JamiiForums-633051173.jpg
 
Kwa hiyo mtoa mada unashauri tumsikilize/tuwasikilize akina nani? Tuwasikilize akina Joseph Kasheku Msukuma, au!!!!

Majibu tafadhali.
Msikilize Msukuma!Msukuma ana akili kuliko hao waliojaza vichwani vya kukariri darasani.
Einstein alitafasiri Akili kuwa"Nikile kinachobaki kichwani baada ya kuondoa yote uliyoingiziwa darasani".
 
Wezi na wapigaji bandarini hawataki mzigo apewe Dp world.

Huyo malisa GJ kaona akina baba levo tu? Nyuma ya hili la kusapoti Dp world wapo vichwa wengi ambao hakuwataja na hawatoki front kupiga makelele mtandaoni. Kuna Rais na washauri wake wote, kuna wataalamu wa wizara wa uchumi, sheria nk. Kuna maafisa usalama wa nchi na wataalamu wengi wanaoendesha nchi.

Lingine naona Malisa kwenye kundi la wagomea uwekezaji kajisahau yeye na Maria Sarungi au yeye yupo neutral?

Tuje kwa shivji, watu wanasema ajibiwe kwa hoja, mie sijasoma kokote hoja za shivji mpk sasa zaidi ya kuona akisema namna ya kuvunja kisheria, possibilities za kuuondoanmkataba na kadhalika. Tafadhari alie na hoja zake akiuchambua ubaya wa IGA ile aweke hapa tusome.

Unaweza kuwa profesa lakini una mlengo, na ukaweka akili pembeni ukasimamia mlengo.

Mwisho kabisa tujiulize simple, tukubali ni ndio DP world mkataba umewapa uwekezaji wa milele pale Bandarini, sawa, kama wameweka ufanisi na Serikali inapata mapato ya haki ipo wapi shida hata wakikaa mpk "Yesu arudi"? Kuna shida gani? Bandari imekuwapo hapo miaka nenda rudi wanashiba tu watu imetunugaisha nini? Tatizo watu wanapima urefu wa mkataba kwa umri wao wa kuishi, uwekezaji wa nchi hata ukiwa wa miaka 200 shida ipo wapi? Vitakuja vizazi vitaona si sawa watabadilisha kama si sawa kwa wakati huo. Hakuna kisicho na mwisho dunia hii "rejea uwekezaji wa makampuni ya mafuta libya" kwa wanaojua Historia.

Serikali inakupa Ardhi wewe Raia kwa miaka 99, na wengi hata huwa wanaamini ardhi ni yao wala hawajawahi hisi ujinga wa seriakli na kuandamana kuwa ni muda mrefu wamepewa itakuwa bandari?

Hivi kuna siku muarabu atabeba yale maji pale Dar es salaam nakuyakausha kupeleka Dubai?

Hacha tufanye, ikishindikana tutatoka hakuna mkataba usiovunjia hata kama sheria zimezuia vipi. Mbona Lowasa alivunja mkataba wa maji wa mto Nile wa kikoloni uliosainiwa miaka mingi nyuma?

Uoga ni kitu kibaya sana, wakati nyerere anaondoka madarakani wapo waliolia tutaishije, alipofariki wengi walilia nchi imefika mwisho machafuko yatakuwa mengi (ujinga). Ajabu tunaishi vema zaidi ya enzi za Nyerere.

Ni muda tusonge mbele. Kama wanaumia Muarabu kupewa Bandari na tulio upande wa kuunga mkono tunaumia kuona bandari imekuwa shamba la bibi miaka mingi.

Angalia Mashirika binafsi ya Simu yanavo perform, chukua TTCL walinganishe? Wana kila kitu hata mwenda ake alipojaribu kuwabeba hawakubebe lakini kuna watu wapo ofisi za TTCL nchi nzima na wako kwenye payroll na wanahodhi Check number wanafanya kazi kwa mazoea, wanakula kodi za wananchi bure. Hawa ukiwaambia TTCL ibinafsishwe awawezi unga mkono.

Wanaotoa bandarini mizigo kwa njia za mkato, hawawezi unga mkono DP world.

Tubishane kwa mawazo sio kwa hisia
Nchi hii tunaijenga wote.
 
Unajishushia heshima
Anajishushia heshima kwa kuwakosoa nyinyi mafisadi? Mbona hamjibu hoja za terms za mkataba ambazo huyo mama amesaini hata bila kuzielewa? Nobody is against private investments ,it is the terms of their investments that the Wananchi are questioning. Ni ujinga ulioje kumpa muwekezaji mkataba usiokuwa na ukomo ; na ujinga huu hauhusianai na dini ya mtu bali ni mapungufu ya mtu husika!
 
Miaka zaidi ya 25 iliyopita ISSA Shivji alikuwa miongoni mwa watu waliiongoza mijadala ya kupinga ubinafsishaji uliokuwa inafanywa na serikali ya Mkapa...aliendika Makala nyingi Sana na midahalo mingi Sana alishiriki...Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu na wengine Wengi....cha ajabu kabisa juzi wakati kajitokeza tena kwenye kupinga Dpworld...cha ajabu kabisa ISSA Shivji karudia maneno yake yale Yale ya kupinga ubinafsishaji kabisa ...akisema namnukuu".. Bandari ni Sawa na mabenki" na Mimi naamini biashara ya bandari kama ilivyo Benki "ifanywe na serikali...ni hatari ikifanywa na watu wengine nje ya Serikali".....

Yaani sometimes kutofautisha proffesa na mganga wa Kienyeji huku Africa ni kama impossible...

Issa Shivji aliongoza kabisa privatisation ya banking industry....licha ya hiyo industry kuja kuwa most reliable na stable Tanzania ..miaka 25 baadae bado anaongea habari za "kuamini"...kweli?? Kwa miaka zaidi ya 25 toka Rais Mkapa alipoibadili sekta yote ya Benki Tanzania hizo hatari alizokuwa anazisema Issa Shivji na wenzie si ndo zingejitokeza ndani ya hiyo miaka 25 na Leo akawa anatukumbusha "maono na maonyo yake na wenzie"?...zile hatari alizo hubiri miaka 25 iliyopita za Ku privatise banking industry Leo hii si ndo angekuwa anatuambia "nilisema"..

Leo miaka 25 later anarudi na story za "kuamini kuna hatari"??Proffesa wa heshima kama yeye amefanya research za hatari aliyotuhubiria miaka 25 iliyopita ukweli wake ukoje Leo hii??na sasa kabisa bila haya anatuletea habari za "hatari ingine "ya bandari...yaani Sura kavu anakuja kuleta habari za kuamini badala ya kuleta habari zenye facts na evidence Kwa sababu amekuwa anaongea mambo Yaleyale lakini tunaona "matokeo"ni tofauti na hatari alizotutisha nazo miaka 25 iliyopita?..

Kibaya zaidi Kila mara anapoulizwa "solution" ya kila shirika linalo taka kubinafsishwa anakuja na theory za farasi aliekufa " Dead horse theory"...kwamba serikali ifanye hiki serikali ifanye kile..wakati dunia nzima hizi theory zimeshathibitika ni 'dead horse theory "...kumchapa fimbo zaidi farasi aliekufa haitasaidia kumfanya ainuke aanze kukimbia ili ufike unapotaka kwenda".....

Inakuwaje mwaka huu 2023 Issa Shivji anazungumza Umuhimu wa bank za Serikali kama vile hazipo kabisa?au hajui kuwa Kikwete alijaribu tena kurudisha Benki za Serikali na zikafa tena mara ya pili?? Iko wapi TIB? Iko wapi women's Bank? Iko wapi Bank ya wakulima aliyoanzisha Kikwete??..

Shivji hajui kuna bank ya serikali imeenea nchi nzima inaitwa TCB zamani ilikuwa inaitwa Bank ya Posta lakini "ina perform chini ya uwezo wake"?...Shivji hajui bank inaweza ingiza faida lakini bado ikawa ina perform ovyo???..

Why kila siku serikali inatangaza Kwa mbwewe gawio la Crdb na NMB lakini hawasemi gawio la TCB??...watu wenye mawazo ya ki communism kama Shivji wanawezaje kuwa na watu wanawasikiliza dunia ya sasa mwaka huu 2023...??idea zake zote zime prove failure Kwa ushahidi kabisa Kwa miaka zaidi ya 25...mtu kama huyu anawezaje kupata ujasiri wa kuhubiri tena hizi dead horse theory tena na tena miaka 25 na zaidi???...kibaya zaidi hata kwenye suala la Bandari anaongea uwongo na kuji contradict mwenyewe bila aibu.

Mara aseme mkataba ule wa IGA hatuwezi vunja ..halafu aseme tena Bunge linaweza kuvunja mkataba ule ..na akaongeza njia zingine nne za kuvunja mkataba......Mkapa alikuwa sahihi kabisa kum ignore huyu Issa Shivji na mawazo yake yalio pitwa na wakati...only time will tell Kama kwenye hili la Bandari kuna lolote la maana jipya alilo shauri....zaidi ya kutaka serikali "iendelee kufufua farasi aliekufa"....
Chawa wa mama bwana, Sisi tunataka ujadili issues na siyo mtu
 
wasiomsikiliza shivji ni watu ambao ubongo wao upo kwenye masaburi tu. kwa mtu mwenye akili timamu anajua kuwa anachoongea shivji ni cha faida kwa taifa na yeye hana maslahi yeyote kama watetezi walivyo.

Mkapa hakuwa sahihi to ignore Shivji kwasababu baadae, baada ya Kustaafu alikili kuwa alifanya makasa jinsi alivyotekeleza sera ya ubinafsishaji!!! Hao wakina Rostam walinunua viwanda vya ngozi kwa bei ya che ambavyo baadae hawakuviendeleza kama mikataba ilivyotaka wafanye; leo wanasimama kutetea uwekezaji wa masharti ya kijinga ili wanufaike tena!!
 
AMEANDIKA MALISA GJ

#TimuYaWananchi
1. Profesa Anne Tibaijuka (Waziri Mstaafu, Mkurugenzi wa zamani UN Habitat, Mhadhiri mstaafu vyuo vikuu mbalimbali)
2. Profesa Issa Shivji (Nguli wa Sheria, Mwanamajumui wa Afrika, Mwanazuoni)
3. Tundu Lissu (Wakili Msomi, Mwanasiasa hodari, Rais mstaafu wa TLS)
4. Dr.Rugemezela Nshala (Wakili Msomi, Rais Mstaafu wa TLS, Mwalimu wa Law School aliyemfundisha Tulia Akson)
5. Dr.Charles Kitima (Katibu mkuu TEC, Mwanazuoni hodari, VC mstaafu Chuo kikuu SAUT)
6. Dr.Fredrick Shoo (Mkuu wa KKKT, Mhadhiri mstaafu vyuo vikuu mbalimbali, Mwanazuoni)
7. Sheikh Abubakar Zubeir (Sheikh Mkuu Tanzania, Mwanazuoni)
8. Freeman Mbowe (Mwanasiasa mbobevu, Mwenyekiti Chadema)
9. Jaji Joseph Sinde Warioba (Waziri Mkuu mstaafu, Jaji mstaafu, Mwanamajumui wa Afrika)
10. Dr.Wilbroad Slaa (Mwanasiasa Nguli, Balozi mstaafu, Katibu mkuu mstaafu Baraza la Maaskofu, katibu mkuu wa zamani Chadema).

#TimuYaMakasuku
1. Baba Levo (Chawa Mwandamizi)
2. Mwijaku (Chawa mwandamizi daraja la kwanza)
3. Zembwela (Msanii wa Futuhi aliyevamia taaluma ya habari)
4. Hando (Mwandishi aliyeamua kuharibu heshima yake ili kujaza utumbo mpana)
5. Kitenge (Dalali Mwandamizi daraja la kwanza)
6. Isaa Azam (Mtuhumiwa wa upinde)
7. Sophia(ni) Juma (Mtuhumiwa wa upinde)
8. Tivu ake (Msanii wa Futuhi)
9. Msukuma (darasa la 7 anayeamuni ana PhD bila kwenda darasani)
10. Kibajaji (Kepteni wa timu ya kusifu watawala ili kushibisha utumbo mpana)

Mechi ni dakika ya 25 kipindi cha kwanza, Timu ya Wananchi inaongoza bao 3 bila. Ukipenda sema tatu sifuri, au tatu nunge, au tatu yai, au tatu duara, au tatu bashite. Ngoma bado mbichi hii, hata half time bado.!
 
team makasuku wanahaha wamefika hatua hadi kama wanaona aibu kuendelea

imagine darasa la 7 b wanashindana na maprofesa..... wataweza kweli?????
 
Back
Top Bottom