Huu huwa ni msisitizo au ni kunajisi ?

Huu huwa ni msisitizo au ni kunajisi ?

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Unamsikia mtu anasema ;
"Nilishalipa na kulipa"
Au
"Nilishakula na kula"
Ama
"Nilishakwenda na kwenda"
"Nilimpiga na kupiga"
Au
"Mimi kama mimi sikubaliani na hiyo bei"
Na
"Wewe kama wewe usinipe shida"
Au
"Mazishi tutazikia hapa , alafu msiba tunauhamishia kijijini kwao marehemu" (msiba unahamishwaje? mazishi na msiba wa kifo hua vinaachana?)
HII misemo ina ufasaha au lugha yetu adhimu inanajisiwa?
Ujinga si kuuliza .
 
Judgment, kwa mtazamo wangu nadhani maneno kama "mimi kama mimi sikubaliane na hiyo bei " yako sawa.
kwani mtu anaweza asikubaliane na hiyo bei husika kwa shinikizo la wengine. hivyo mtu akisema "mimi kama mimi sikubaliane na bei hiyo" humaanisha kuwa, kwa akili yake mwenyewe bila kuchanganya na ya mwingine hakubaliani na hiyo bei
 
Labda inaweza kua na maana na ndiyo mana nikauliza .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom