Huu hapa msikiti wa majini

Kwamba anasema majini wenyewe walimuita mtume wakutane ili aje awasomee Quran ili wasilimu?

Ila kobazi bana, inahitaji kweli ujitoe ufahamu wa Akili ndo uyaelewe hayo mambo
Ila mkuu ukiambiwa leo hii 👽 Alien wanakuja dunia na kuwasiliana na watu unaamini?
 
😁😁

Waendelee kudanganya watoto na vilaza wenzao

Kuita watu "watoto" na "vilaza" si hoja, ni njia ya kukwepa mjadala. Kama unaamini yaliyomo kwenye video ni ya uongo, onyesha ni sehemu gani imekosea na ulete ushahidi.

Matusi hayabadilishi ukweli. Hoja hupingwa kwa hoja, si kwa kuwadharau wanaoisikiliza.
 
Huwezi kuona jini ukiwa katika normal human body. Maana jini ni spirit.
 
Wewe ni mdini sana. Juzi umewatukana sana walokole. Ila Leo unajifanya ni Imani yao tu.
Hapana mimi wala sina dini, sisali wala siamini mambo ya Mungu iwe kwa waislamu au kwa Wakristo, sasa wao kuamini majini, na walokole niliowazungumzia kule wanahusiana vipi?
 
majini ni malaika walionguka wakiongozwa na kiongozi wao Lusifa

Hilo ni dai la tafsiri ya kidini, si jambo lililo wazi moja kwa moja kwenye maandiko yote.

Biblia inataja mashetani/pepo, lakini kuhitimisha kwamba kila jini ni malaika aliyeanguka chini ya Lusifa ni tafsiri inayohitaji ushahidi wa maandiko.

Hoja nzuri huonyesha kifungu kinachosema hivyo, si kurudia tu imani fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…