Hussein Tuwa vs Eric Shigongo (Riwaya)

Mkuu! Uthibitisho wa ubora wa utunzi wa vitabu Si sawa Na football player kwamba huwezi kuthibisha ubora wake kwa mechi moja, mtunzi bora WA story utamuona Tu toka anavyokushawishi uendelee kusoma toka page ya kwanza, Tuwa mpaka sasa Ana zaidi ya Novel 5 ambazo nimezisoma, kweli unashindwa kujua uwezo WA Mtunzi ambaye Ana Novel tano sokoni, Tuwa Ni bora kuliko Shigongo, hadithi zake ukiwa unasoma muda wote anamweka msomaji roho juu, Na style yake ya uandishi sio level za Shigongo!
 
hussein Tuwa ni mkali, hadithi zake zimetulia na ametumia akili, shigongo hana jipya hadithi zake zote zinafanana, hazihamasishi kusoma, na ukianza kusoma tu unapredict itakuaje maana matukio yafanana
Sometime akijua kuwa umejua itakavyoisha anabadiri gia angani, bas story inakuwa ya kusadikika
 
Acha kabisa Tuwa mzee wa taharuki ni habari nyingine kabisa. Shigongo anasubiri sana kwa Tuwa . Mkimbizi kuna huyu dada wa kuitwa TIGGA kila siku kwake ilikuwa taharuki mpaka unatamani hadithi isiishe.Namkubali sana Tuwa kuliko Shigongo though financially Shigongo yupo juu.
 
yani Hussein Tuwa ni mkalii alinifanya niache kusoma hadithi za shigongo.
Soma Mkimbizi, Mtuhumiwa na utata yani ni noma jamaa anajua sana sana.
Hivi willy Gamba aliishia wapi??
Alikufa mkuu aristabus elvis musiba.
 
Mmhh TUWA ni mtu matata sana .. Saana .. Ila shigongo anaonekana mkali kwa waswahili kwa kuwa ana miliki kampuni ya magazeti ambayo inampa nafasi ya kujitangaza zaidi
 
Mimi niliacha kisoma simulii za Erik shigongo pale lipotoa kitabu kikuuiuiibwa Cha rais anamtaa mke wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usifananishe James A chase na watu wako wanaonunua riwaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hussein Tuwa kiboko...ile hadith ya mkimbizi, ilikuwa ukisoma Roh inakuwa juu juu....acha tu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…