Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi: Kuna viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyotokana na kauli za watu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
434
1,000
Leo Dkt. Hussin Mwinyi anaendelea na kampeni ya kuwania Urais Zanzibar eneo la Micheweni kuiongoza serikali ya awamu ya nane na miongoni mwa mambo aliyoyazungumzia, amesisitiza kulinda amani ya Zanzibar. Mwinyi amesema sasa kuna viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyotokana na kauli za watu mbalimbali ambao hakuwataja. Mwinyi amesema wao wanaCCM waendelee kuwa wavumilivu na kudumisha amani yao kwani panapo amani ndipo patakapokuja maendeleo.

Pia Dkt . Hussein Mwinyi ameongelea kilio cha ajira kwa vijana na kusema kulingana na ilani ya CCM wamejipanga kutengeneza ajira laki tatu visiwani na ni matarajio yake kwa uchumi mkubwa wa kisasa watakaoujenga, uchumi wa bahari utakaokuwa na bandari ya kisasa utaweza kuajiri vijana wengi sana pia Zanzibar ya viwanda ili kuweza kutumia rasilimali zinazopatikana Zanzibar na idadi kubwa zaidi ya ajira.
 

Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
1,425
2,000
Hizi ajira laki tatu zitapatikana kutoka wapi? Na kwa utaratibu UPI? Hapa panahitaji maelezo. Bandari ipi wakati Tanganyika imekataa kutoa kibali cha ujenzi wa bandari ya Mpigaduri?
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,693
2,000
Namkubari sana Hussein Mwinyi ila aliyemshauri kugombea Zanzibar amempoteza, hata nafsi yake najuwa dhamira inamsuta.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom