Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Kampeni zimeisha.
Bashe ana haki ya kumtetea rais wake aliyepo.
Ukumbuke kuwa Bashe ni ukanda mmoja na Prezdaa kwa hiyo hawezi mtupa.
Hapa nadhani unataka tu kumchonganisha Magufuli na Bashe.
Kumbuka kuwa Bashe ni Mbunge wa CCM na Magufuli ni Rais wa CCM na Tanzania sasa.
Hizo tuhuma zote unazomtupia Bashe hazina ushahidi.

Ninakuunga mkono kwenye suala la kujibu hoja za Membe ambazo kwangu ni hoja makini sana.

Kumzuia Bashe asitoe hoja zake utakuwa sawa na wale wanaomwandama Membe kwa hija zake kama mtanzania.
CCM imekua chama cha ajabu sana tangu kilipovamiwa na vijana wenye uchu wa madaraka. Hawataki kuona mtu anakosoa jambo lolote.
Tumeona mpaka Magazeti ya kifutwa kwa sababu tu ya kutofautiana mitizamo. Hii sio afya njema kwa demokrasia ya nchi yetu. Vijana ni lazima tujifunze kokosoana kwa hoja. Sio mtu anatoa hoja zake halafu anashambuliwa kama mwizi kwa kejeli ,uzushi na fitina.Bashe naye aache atoe dukuduku lake kama vipi ajibiwe kwa ushawishi ili aelewe na sio kuambiwa kuwa akae kimya.
 
Ni kweli kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo, na pia azingatie na kuelewa kuwa awe tayari kuwa huru kukosolewa mawazo yake; ndio moja ya sifa za wanazuoni (kutoa mawazo hadharani na kusubiri kujadiliwa na kukosolewa iwe ni chanya au hasi) - Huo ndio ukomavu wa kimawazo
uko vizuri sana.

umenena vyema
 
Naunga mkono watu kutoa maoni hasa hasa waliowahi kuaminiwa na kuongoza lakini wasitoe kwa staili kama ya kushambulia vile.
Haitakiwi wakae kimya eti kusubiri matokeo baada ya miaka mitano,uongozi wa Leo kujitathmini ni tendo la kilasiku sio mpaka wakati wa uchaguzi.
kuna vijana wamejipendekeza wakapata vinafasi basi hawana ata nidhamu,wanashambulia watu sawa na baba zao bila soni. Hekima ya uongozi haipo kwa vijana wengi kwenye siasa, wanajifunza matusi kabla ya namna ya utendaji kazi, deeeeeem!
 
Ukiwa unaponda ki2 ambacho watu wengi wanaona ni sahihi,ongea kwa hoja na mifano lukuki kuonesha uliwafanyia nini watanzania enzi zako zote za uwaziri
Ikumbukwe tu,Magufuli hakuwa chaguo la wafaidi serikali
《《Tuipende tanzania kama tanzania maake miaka mingi ijayo tutajivunia tulipoifikisha atakama tukiwa hatupo dunia hii》》
 
Kila mtatanzania ana uhuru wa kutoa maoni ila asivunje katiba.

sasa wanasiasa wana hofu nini mtu akitumia uhuru wake, au kwa sababu wameathiliwa na NDIOOOOOO.

Nchi haiwezi kuendelea kama kutakuwa na watu wanaowazuia wenzao kufikiri nje ya boksi.
CCM wajifunze utaratibu wa kusikiliza na kujibu hoja. Chama kikongwe ukomavu wenu uko wapi? mtakuwa lini? Hoja ya yaweza kutokea popote, wala kwa kushindwa hakumwondolei mtu haki ya kutoa maoni yake.
 
Membe si alimpigia debe magufuli Lindi sasa analalamika nn ? Walimchagua wenyewe.
Sio kosa kumshauri hata kumkosoa uliempigia. Watz hiyo ndio democracy ya kweli. Tusiogope kutofautiana ndio tutaijenga nchi hii.
 
Nimependa aya ya tatu,Bashe anasema Membe amekua sehemu ya mfumo dhaifu uliotufikisha hapa!!! Anataka kuungana na mnyika kwamba ba riz alikua dhaifu na kusababisha mfumo dhaifu?
Kwani anayemtetea hakuwa sehemu ya mfumo huo? Mbona rais akihutubia bunge alisifu awamu iliyopita na kusema anaendeleza ilipoishia hasa kwenye sera ya mambo ya nje?
nashauri wasiongee sana wajue kuhifadhi maneno
Membe alitoa hoja jibuni hoja, hamuwezi atajibu mhusika, ingawa nae anaweza kujibu kwa kunyamaza.
 
Ukiwa unaponda ki2 ambacho watu wengi wanaona ni sahihi,ongea kwa hoja na mifano lukuki kuonesha uliwafanyia nini watanzania enzi zako zote za uwaziri
Ikumbukwe tu,Magufuli hakuwa chaguo la wafaidi serikali
《《Tuipende tanzania kama tanzania maake miaka mingi ijayo tutajivunia tulipoifikisha atakama tukiwa hatupo dunia hii》》
 
Unakumbuka ticket ya ndege sh 600000 ,ofisi ya Membe walikua wanaandika sh 6000000????yaani wanaongeza sifuri.
Membe ni mtoa na mpokea rushwa.Pesa ya Gadafi kujenga kiwanda cha cement lindi kafanya ni mradi binafsi kupitia kwa mfanyabiashara feki
Unaonaje ukikusanya ushahidi ulionao ukapeleka swala hilo zito polisi
 
Membe ni jipu na linatumbuliwa taratibu linamuuma na bado rais atakamua zaidi tunakuonbea rais wetu uendelee kuyakamua kwa manufaa ya watanzania wa kawaida walio wengi kuliko kundi dogo la mabwanyenye
 
dah Mungu ni mwema wakati wote! tushao aina ya rais ambaye mkwere alikua anataka kutuchagulia...ila kumbukeni hayo majip yanayo tumbuliwa baadhi yapo mwilini kwa membe so anaumia sana
 
Hili ni andiko la Hussein Bashe:

Bashe:

Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi

Membe amekuwa Waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa Serikali haijapungua ama kubwa or ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekuwa sehemu ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa. Amefaidika na safari za nje yy binafsi bila manufaa kwa nchi. Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake Magufuli believes matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya Hovyo na yasiyo ya lazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu Membe afahamu Magufuli ana style yake tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari labda Membe kama yy binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kuli muathiri yy binafsi kwa kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Common wealth that's why leo anakosoa.

Tunafahamu maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka ktk Awamu ya nne. Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serikali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokuwa na mabalozi magufuli hana siku 100 yy amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

Amekuwa mmoja wa mawaziri walokuwa foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu yx mis use of funds ktk wizara yake. Kipindi chake safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Ni muhimu Membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathiriki directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi aliwahi kusema Sankara "You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliyekuwa akinyonywa hapo awali tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakuwa style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wa kuwanyonya wengi na wachache kufaidika.

Wassalaam
membe kazungmza tuu sio kwamba kasema alichokisema kifanyike jaman...... mbona alivyo criticise kuhusu mambo ya kurudia uchaguz zanzibar hamkumsema????????????????????
 
Ukiona watu wana pinga pinga kiongozi wanaye mpenda kufanyiwa constructive critism kuhusu uendeshaji wa serikali basi ujue kuna tatizo kubwa zaidi kwenye uongozi huo. Kiongozi haogopi critism bali huzichukulia kama changamoto kuimarisha utendaji wake....
 
Mijadala inayohusu namna bora zaidi ya kuendesha nchi ina tija sana kwa mustakabali wa taifa letu.Mijadala ni sehemu ya demokrasia.
Membe anaweza asiwe ni mtu msafi sana ila ameibua mambo mazito yanayohitaji tafakari ya Kina.Mathalani mgogoro wa Zanzibar.Ata Dkt.Salim Ahmed Salim nae ameongelea swala la Zanzibar kwa mtizamo tofauti na msimamo wa CCM.
Bashe hayuko sahihi kukataza mijadala ya kukosoana.Bashe angekuwa mwerevu angepinga hoja za Membe kwa kutumia hoja na takwimu.Mimi binafsi namuona Bashe ni mchanga sana katika ulingo wa siasa na yupo kichama zaidi katika kutafuta maslahi binafsi.
 
akina lowasa kumbe wengi aise! Ukikosa cheo kidogo unaanza kulalamika na kujifanya wajuaji kumbe
 
Back
Top Bottom