Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Majipu mengine ni hatari kwa afya ya Mh Rais,yanatoa mionzi badala ya usaha. Haya majipu jamii ya maembe,JPM avae mavazi maalum kama daktari wa kambi ya ebola
 
Membe.jpg

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ( Kushoto), Mbunge wa Nzenga Mjini (CCM), Hussein Bashe (Kulia)
Dar es Salaam. Mbunge wa Nzenga Mjini (CCM), Hussein Bashe amemtaka aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuacha kumshambulia Rais John Magufuli katika utendaji wake.

Kauli ya Bashe imekuja siku moja baada ya mfululizo wa habari zilizomnukuu Membe akimkosoa Rais Magufuli katika maeneo kadhaa likiwamo suala la kuzuia safari za nje, Rais kwenda nje ya nchi huku akimpa tahadhari ya kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa.

Kupitia taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, Bashe alisema Membe amekuwa waziri kwa miaka kumi na kutimiza wajibu wake, hivyo amuache Magufuli naye atimize wajibu wake kwa wananchi.

“Aliomba urais, hajateuliwa, asubiri 2020 au 2025 ili akipita aanzishe ‘uvasko da Gama’ tena,” alisema.

Alisema hoja alizotoa kumkosoa Rais Magufuli zinaonyesha ni mwanasiasa mufilisi. “Serikali haijapungua, kubwa au ndogo au hoja kuwa safari za nje ni muhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi.”

Bashe alisema mwansiasa huyo akisema amefaidika na safari za nje yeye binafsi bila manufaa kwa nchi na amekuwa sehemu ya mfumo dhaifu ulioifikisha Tanzania ilipo kama Taifa, hivyo anatakiwa kutulia kwa kuwa kila Rais ana mtazamo wake.

Alisema Rais Magufuli anaamini matatizo ya Taifa yatamalizwa na Watanzania wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya hovyo na yasiyokuwa ya lazima badala ya kutegemea safari za Ulaya zinazoendeleza tabia ya taifa kubakia ombaomba.

Alisema ni muhimu Membe akafahamu kuwa Rais Magufuli ana staili yake na atapimwa kwa kuangalia matokeo, lakini kwa sasa hatujaona athari za zake.

Bashe pia alisema anatambua maamuzi mengi ya Rais Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi waliofaidika na miradi kama Nida, fedha za Gadafi, na matumizi mabaya ya madaraka katika awamu ya nne.

Alisema majipu mengi yanayosubiri kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa mwelekeo wa Serikali ya awamu ya Tano.

Alihoji kwamba hoja ya kutokuwa na mabalozi, haina mashiko kwani Rais Magufuli hajafikisha hata siku 100 ofisini, lakini yeye amekuwa waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka minane na hakuona umuhimu wakati huo.

“Binafsi kama mbunge, naunga mkono ‘style’ ya Rais Magufuli ya uongozi, mabadiliko anayofanya sasa yanahitaji roho ngumu, uwendawazimu kidogo, kuungwa mkono na wananchi wote kwa kuwa waliofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko,” alisema Bashe.

Chanzo: Mwananchi
 
membe atulie wanaume wafanye kazi wakiongozwa na rais mpendwa jpm. walicheka na sasa wanalia. tulilia kwa uchungu na sasa tunacheka. hongera jpm, wanyonge tuko nyuma yako.
 
Kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake....kama yeye Bashe ana sifia tu.bila kukosoa basi asiwabwatukie wasokoaji. Yeye atoe mawazo na maoni yake kuhusu utawala wa JPM sio kuwalazimisha watu wawe na mawazo kama yake.

Yale yanayofanywa na JPM kuna watu walitoa mawazo hayo hayo wakati wa JMK na watu wa hulka kama ya Bashe wakawajia juu
 
Membe anatafuta kick za media tu hana lolote
 
Ndiyo!kila mtu ana haki lkn sio kwa mtindo huu aloutumia mh.Membe,kwa wadhifa aliokuwa nao na alichokiongea ni wazi ana kitu ndani yke inamnyima aman kwenye utawala wa awamu ya tano.yawezekana na yeye ni fisadi.au ana kona kona aliyoifanya ktk utumishi wake.
 
Mhesh.Bashe nakuunga.mkono 100%.You have made a case. Tusimame ktk misingi ya ukweli. Hatua anazochukua Magufuli ni kwaajili ya kuwanufaisha watanzania wa kawaida. Membe ni msemaji wa mfumo uliokubuhu kuwanyonya watanzania ktk awamu ya 4. Mfanyabiashara ambaye halipi kodi ni mnyonyaji. Afunge biashara zake/aondoke. Ni hoja ya kipuuzi eti kulinda wafanyabiashara. They must pay tax, otherwise they are useless to th welfare of th wananchi. Nchi zinazoongozwa na mafisadi huwa hazikusanyi kodi kwasababu wao ni beneficiaries wa ukwepaji kodi huo. Nina mashaka makubwa sana na "uadilifu" wa Membe. Huyu angekuwa raisi nchi ingeuzwa kwa wafanyabiashara wasiolipa kodi. Membe anawakilisha kundi lenye ajenda mbaya dhidi ya watanzania na raisi wao Magufuli. Vyombo vya dola vichukue tahadhari ktk hili. Magufuli songambele. Wewe ndo tulikuchagua. Una dhamana ya nyoyo zetu. Who is Membe?Atuambie juu ya fedha za Gafaffi. Kidumu chama cha mapinduzi!!!!!!
Mbona JPM aligawia mchumba wake nyumba ya serikali! Wote ni wale wale tu.
 
..hivi hii story ya fedha za Gaddaffi ilikuwaje,Membe alizipataje hizo pesa?
 
Membe naye eti anatoa maoni kuhusu serikali iliyopo madarakani na kuikosoa
Hili ni ajabu jingine la dunia
 
Bashe ana akili ya ki imla. Hizi siyo enzi za free pass. Tanzania ni demokrasia inayoruhusu mawazo tofauti, na siyo Korea Kaskazini ambako watu wote wana akili zinazofanana za kusifu kila anachofanya Dear Leader Kim Jung Un. JPM na genge lake wajiandae kuendelea kukosolewa na watazania wenye mawazo tofauti.
 
MAJIBU KWA HUSSEIN BASHE DHIDI YA DHIHAKA ZAKE KWA MEMBE.


Ndugu Bashe afadhali umeibuka maana tangu jana waachambuzi wa maombo walikuwa wanaulizana hivi Bashe uhasimu wake na Membe umeisha baada ya Edward Lowassa kuhamia ukawa????

Mosi inashangaza kwamba wakati wote wa kampeni ulizokuwa unapiga jimboni kwako kwa nafasi ya urais ulikuwa wampigia nani mchana ???

na ikifika usiku ulikuwa wampgia kampeni nani?

Pamoja na kauli ya Magufuli ya chama hiki kina wanafiki wengi ila bado hukujiongeza, wewe na wenzako mliendelea kuhubiri ccm mchana na ikifika usiku mnavaa magwanda yenu ya ukawa eti hamuwezi kumtupa Boss wenu ajiskie mkiwa ugenini huko ukawa.

Unapoibuka leo ghafla na kujifanya ni shabiki wa Magufuli, waandishi wenzako tuliokuwa tunakuheshimu ukiwa Habari Coproration ambayo mali ya Lossa na Rostam sio tu tushaangae bali pia tusikuelewe kuwa unapata wapi ujasiri kuihadaa dunia kuwa ni mpenzi wa Magufuli.

Nakuamuru ujibu hoja alizotoa Membe sio kurukia kwenye ngionjera zako za miaka yote zikileta habari za NIDA ama mabilioni ya Ghadafi,Ukishindwa hoja basi endeleaa na mradi wako wa kuwarejesha ccm waliohama akiwemo Lowassa, Msindai, Mgeja n.k……..

Bashe nakukumbushaa badala ya Kuwaonea huruma rafiki zako Bade na Bashir kwa waatakayo wakuta kutokana na uhumuju wao nchini naomba ujionee huruma wewe mwenyewe kwani ajira yako ya udalali wa kisiasa iliyokuwa yakuweka mjini 2005-2015 sasa imefika mwisho hivyo buni ajira mpya ya 2015-2020.

Hivi Bashe umesahahu ahadi za Lowassa kuwa akishinda Urais wewe utakuwa waziri wa habari, halafu leo ghafla unajifanya unatoa machozi ya mamba kujifanya unampenda magufuli ambaye kila uchao ulikuwa unammiminia kashfa kwenye mitandao ya kijamii kipindi chote cha kampeni ukiwatumia vijana wako uliokuwa unawalipa ujira mdogo.

Samahani Bashe hivi umesahau ulipokuwa St.Gasper hotel wewe ndiye uliyekuwa kwaya master wa ule wimbo wenu wa tunaimani na Lowassa uliowaimbisha kina Mgeja, Msindai, Sophia Simba?? Au ndani ya ule wimbo kulikuwa na ubeti unaomsifu Magufuli???

Msimfanye Rais ni zezeta kwani anawajua mahasimu na wanafiki kwa majina na vyeo vyao nchini.

Hivi hata wewe bashe siku hizi una ujasiri wa kunyoosha kidole kweli?? Au tukukumbushe zile dili zenu haramu zilizokuwa zinawaingizia mabilioni mliyokuwa mnawahonga wajumbe kila sikukuu???

Na pia sio wewe uliyekuwa unapinga swala la kujivua gamba?? Tulia Daktari Magufuli akutumbue jipu taratibu kwani nina imaani hujui kuwa kutumbua jipu ni neno la kibaiolojia lenye maana sawa na kujivua gamba.

Bashe mimi nakupenda sana maana wewe ni mmoja wa walimu wangu katika tasnia ya habari hivyo sipendi uwe mkurupukaji.

USHAURI WA BURE:

Ushauri wangu kwako kwa leo,hivi kwanini mambo kama haya usiwaachie watanzania wenyewe wajadili?? Au bado unaaamini hawanaa uwezo huo kiakili????.
 
ushindi masebo ulichofanya hapo juu ni kujivua ngua...Jibu hoja za Bashe otherwise acha kutetea ujinga
 
Back
Top Bottom