Hussein Aman Marsha

Hussein Aman Marsha

Observer2010

Senior Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
195
Reaction score
44
Nimekuwa mfuatiliaji wa soka la kibongo na kimataifa kwa miaka ya kutosha, kuna wachezaji wengi sana wenye uwezo wa juu mno nimeshawaona, ila leo hii nimemkumbuka huyu holding midfielder, binafsi namuona ndiye bora zaidi kuwahi kumuona katika soka la kibongo, Hussein Aman Marsha. Natazama soka katika ligi bora zaidi duniani kwa sasa ila bado naamini huyu jamaa aliwazidi viwango wachezaji wengi mno katika hizo ligi.

Hivi ilishindikanaje watu kama hawa kucheza soka ligi bora kabisa na katika timu bora kabisa duniani ?
 
Nafikiri ilikuwa ni kukosa mipango ambayo ingemuwezesha kwenda kuonyesha kipaji chake huko kwenye ligi za wenzetu,isitoshe level ya ligi yetu na performance ya team yetu ya Taifa ni kikwazo kingine kikubwa tu,teoam za Ulaya huwa wana'consider sana nchi anayotoka mchezaji na mchango wake katika team ya Taifa.
Ni ukweli usiopingika Jamaa alikuwa Fundi haswa.
 
Yah, ni sahihi kabisa, ila nadhani pia exposure yetu watanzania ilikuwa ni ndogo sana. Ukiangalia mtu kama Geogre Weah alitokea nchi ambayo kisoka ilikuwa haijulikani kabisa, watu walikuwa wanaijua Liberia kwa sababu ya vita tu.
 
He was, by far, my favourite Simba player during his tenure at Msimbazi (alongside Mohammed Mwameja and George Masatu). He had excellent ball control, composed under pressure, and could defend as well as provide much-needed support to the striking force. He could play a multitude of positions. He was very polite and very accomodating to fans. I had the pleasure of meeting him a couple of times, and had a great time hanging out with him.
 
Hussein Marsha alikua mbaya lakini the late "Method Mogella" alikua nomaaa!!!

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Khalid Abeid? hakuna midfielder Tanzania mpaka leo aliyekuwa akiucheza mpira kwa raha na utaalam kama huyu.

Ni artist.
 
Yupo UK ila hata mie mara ya kwanza kuona mpira wa huyu Jamaa sio unazi wa kuipenda Simba, Jamaa alikuwa mkali akifuatiwa na Salvatory Edward Hussein, Masha mpira na nje kuna jamaa alicheza naye timu ya Taifa anaitwa Seif Khalfan Mzenji alikuwa Malindi niliwahi kukutana na Seif Khalfan namna alivyokuwa anamsifu Hussein Masha mpira na Tabia za Masha kuhusu wanavyokwenda kwao na anavyokaa na wachezaji wakiwa na matatizo, anasema hakuwahi kuona kama Hussein Masha anasema hata kambini Manager anashindwa kutatuwa jamaa anatatuwa matatizo na wachezaji wanamsikiliza kwa kumuheshimu alikuwa anaongelea mpaka Ukarimu wake wakienda kwake jamaa kuna mdau hapo juu kaongelea sasa nimeamini zaidi. Masha, Salvatory na Marehemu Method Mogella Soka ya sasa hivi Nje wangetesa sio Lunyamila kukimbia tu na kutizama chini.
 
Yah, hakika bongo vipaji vilikuwepo sema hakukuwa na support kubwa ya makampuni km miaka ya karibuni. Mmetaja majina kadhaa ila mmemsahau Hamis Thobias Gaga aka Gagarinho (RIP) huyu alikuwa mashine nyingine ya hatari sana pale kwenye kiungo ya kushambulia. Hope ni mmoja wa vipaji bora kabisa katika nchi yetu.
 
Sitamsahau huyo jamaa namkumbuka alikuwa pia mtaalamu sana wa kupiga penati, nakumbuka mechi ya Stars na Guinea uwanja wa Sheikh Amri Abeid pale arusha alipiga bonge la penati na mechi iliisha kwa bao 1 kwa bila ila tukio la ajabu lililotokea ni mashabiki kupiga magoti majukwaani kwani kipa wa Guinea alikuwa hatari balaa.
Kwa kipindi chake hapakuwa na watu wa kuwasaidia kama ilivyo kwa sasa.
 
Khalid Abeid? hakuna midfielder Tanzania mpaka leo aliyekuwa akiucheza mpira kwa raha na utaalam kama huyu.

Ni artist.

Mkuu Aluu Ally?
Unamkumbuka? hii ilikuwa mashine nyingine bana
 
Yah, hakika bongo vipaji vilikuwepo sema hakukuwa na support kubwa ya makampuni km miaka ya karibuni. Mmetaja majina kadhaa ila mmemsahau Hamis Thobias Gaga aka Gagarinho (RIP) huyu alikuwa mashine nyingine ya hatari sana pale kwenye kiungo ya kushambulia. Hope ni mmoja wa vipaji bora kabisa katika nchi yetu.

Huyu alikuwa akitinga na yule Lilla Shomari (RIP) basi ilikuwa raha tupu....Adolph Rishard naye alikuwa mzuri sana.
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa soka la kibongo na kimataifa kwa miaka ya kutosha, kuna wachezaji wengi sana wenye uwezo wa juu mno nimeshawaona, ila leo hii nimemkumbuka huyu holding midfielder, binafsi namuona ndiye bora zaidi kuwahi kumuona katika soka la kibongo, Hussein Aman Marsha. Natazama soka katika ligi bora zaidi duniani kwa sasa ila bado naamini huyu jamaa aliwazidi viwango wachezaji wengi mno katika hizo ligi.

Hivi ilishindikanaje watu kama hawa kucheza soka ligi bora kabisa na katika timu bora kabisa duniani ?
Mwaikimba je?
 
Eti miaka ile Magamba walituaminisha kuwa soka ni ridhaa na sio ajira. Yaani wametupotezea sana. HM alikuwa ktk levels za kina marehemu Rashidi Yekini,Amunike,Roger Mila na wengineo
 
Sasa mbona wachezaji wote mliowataja humu ni majina ya waislam.. Ina maana wakristu walikuwa fani gani..
 
Mkuu Aluu Ally?
Unamkumbuka? hii ilikuwa mashine nyingine bana

Namjuwa sana wacha kumkumbuka, ni cha mtoto kwa Khalid Abeid.

Halafu Yanga walikuwa nae Gilbert Mahinya. Akiitwa "mapafu ya mbwa", jamaa alikuwa hachoki. Enzi zao hawa Tanzania ndio ilikuwa inacheza mpira wa uhakika, kwa kuupenda haswa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom