Hahahaaaaaa! Ndo ile unakuta mtu kafujwaaaaaa! Kachakaaaa ila anajipa moyo si NIMEOLEWA! Mwingine anachezewa na kirav 4 juu, mjengo wa maana, mivacation, acha kuku za mboga mpaka basi! MAISHA NI JINSI UNAVYO YAANGALIA,^^
Mbona wapo wengi sana! Wana magari yao, majumba, miradi yao, sema tu hawaoi wanawachezea tu.
Akina sie tusio navyo ndio juhudi zetu haziendi joshi. Hivyo vuteni subira pengine wataamua kuoa, subira yavuta heri
^^
Kibaoooooo! Tena wana DEMAND KABISAAA! Nipe hiki, nipe kile! WTF ( Huduma ya airtell incase your imigination goes wild)Hakuna men anaetegemea dem kwenye life lake,fanya tathmini upya.
Kijana umemaliza chuo umeajiriwa serikalini miaka miwili umeoa, mwanachuo mliehitim nae haujajipanga, haujandaa mirija ya kiuchumi zaidi akili yako yote kuwaza mshahara wa mkeo ambaye yeye kasomeshwa na wazazi wake wakulima wa mahindi pale ileje nasisitiza wanaume tubadilike sasa
Namuombea atakaekuja kuwa mume wangu mpenzi,popote alipo
Wewe ni mwanaume kama mimi lakini unawaza habari za hamsin kwa hamsin tena kwenye mshahara wa mkeo wa laki tatu kwa mwezi halafu unajipa moyo ooohhh nitatoka nani anakudanganya wewe, halafu bado unajiita wewe ni kichwa cha familia la hasha lazima tubadilike ndugu zangu la sivo tutaibiwa wake zetu na wale wenzetu wanaojituma kusaka salari
Habari kamiliiiiiiiii na ya uhakika
kwa masikitiko makubwa sana naona ongezeko kubwa la wanaume ambao wanakosa sifa za kua wame bora ndani ya familia zao kwa sababu ya kutoyatambua majukum yao kama baba wa familia, wengi wa wanaume wana ndoto za kufanikiwa maisha kupitia kazi au mishahara ya wake zao na ikifikia hapa jua wewe haufai kuishi na mwanamke, jitahidini kujipanga , acheni uvivu, vumbua fursa za kiuchumi na uwe na mipango endelevu hapo utakua ni husband material.
Haya masuala ni relative tu. Nini kipimo cha kujipanga? Kwa mwingine ni mpaka awe na kampuni ndio atasena now am ready, mwingine kibarua tu kinachompa riziki kinatosha kumfanya aseme yuko tayari.
All in all ndoa ni furaha period. Whether mna mabilioni kama Mengi na Klyn au ndio mnabagaiza, swali la muhimu ndoa yenu ina furaha,
Ni kweli kabisa inabidi wanaume tubadilike sasa..ila sio wa sikuhizi hata zamani ndo maana ulikua unaona mtu anazaa watoto anapeleka kwa mjomba .. huyu anapeleks kwa shangazi ..hiyo nayo ilikua ni kukimbia majukumu..
Umeamua kumfikishia ujumbe mumeo kupitia hapa?
Sio vyema ukaexpose stress zako
Haya masuala ni relative tu. Nini kipimo cha kujipanga? Kwa mwingine ni mpaka awe na kampuni ndio atasena now am ready, mwingine kibarua tu kinachompa riziki kinatosha kumfanya aseme yuko tayari.
All in all ndoa ni furaha period. Whether mna mabilioni kama Mengi na Klyn au ndio mnabagaiza, swali la muhimu ndoa yenu ina furaha,
mi nilijua we ni demu unalalamikia wanaume... Kumbe wewe dume zima unalalamikia wanaume wenzio? Halafu kama una bifu na mtu si umuambie? Dizaini kama unamsema mtu hapa kijanja...
hivi unazungumzia HUSBAND MATERIAL au HUSBAND ndani ya familia???