ipyax
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 4,752
- 7,301
Kuna jamaa mmoja mlemavu asiye na mikono alitumbukia shimoni usiku, akaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada.Bahati nzuri akatokea msamaria mwema aliyesikia mayowe akaenda kusaidia, lakini akakuta jamaa hana mikono huku nyenzo pekee aliyokua nayo ikiwa ni kamba.Akamshauri jamaa atumie meno yake kuiuma ile kamba kwa nguvu zote wakati yeye akimvuta toka shimoni.Wakalianza zoezi kwa mafanikio makubwa tuu mpaka kichwa cha jamaa kilipofika kwenye mdomo wa shimo yule msamaria mwema akaingiwa na huruma kumuona jamaa alivyokua amiuma ile kamba huku jasho na machozi vikimtoka,MSAMARIA AKAMWAMBIA JAMAA POLE HALAFU NAYE AKAJIBU AHSANTE,,,,,,,...