Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Ngoja waje waosha viatu, na hili watashangilia kama walivyomshangilia Mkaa100.
 
hapa ndipo tunapigwa bao, C.C.M wao wanaweza kusimama hadharani wakasema ''katiba ya chama inasema bla bla kuhusu taratibu za kupokezana uongozi ..." Whilst huku kwetu sio tu hujawahi kusikia uchaguzi chamani lakini hata Katiba ya chama kuimiliki ni kama nyara za serikali.

Kuna mtu hapa anayo soft copy ya Katiba ya CHADEMA aniazime tafadhali?
 
Bora alivyotolea ufafanuzi.....

Sisi wengine tunaona lini atamaliza muda wake aende, halafu miccm eti inataka kumuongezea miaka mingine 2!
Sio ya kuyaamini hadi mda ufike hata kinyume chake pia ni maamuzi.
 
hapa tunaandaliwa!! hata kagame alisema wananchi wamemwomba ila yeye hakutaka, mwisho wa siku huyo hapo ikulu
 
Kikubwa ni kuimarisha taasisi imara, Miaka minne tu inatosha kumpima na kuona matokea ya kiongozi kwa ngazi ya Rais, Mbunge na Diwani

Africa inapaswa kuwa na taasisi imara zile zama za kuwa na 'strong man' kama kipindi cha kupigania uhuru kimepitwa na wakati

Refer hotuba ya Obama alivyo sema Ethiopia ktk kikao cha AU kipindi kile akiwa Rais wa US

Africa inatakiwa kuwa na taasisi zenye nguvu na sio mtu mmoja awe powerful
 
Rais Magufuli ameyasema hayo alipokutana na katibu uenezi wa CCM ndugu Hu!phrey Polepole. Rais amemtaka Polepole kuwahakikishia watanzania wote kwamba serikali ya awamu ya 5 kamwe haitafanya upuuzi wa kurekebisha katiba ili kumwongezea Rais muda wa kukaa madarakani. Source Clouds Tv habari!
 
Anakemea mangapi hili liwe gumu ?
Atoke hadharani aseme waoleta hizo habari ni wapumbavu sana.
 
Siasa zetu zimeshakuwa za ajabu sana. Kiongozi anapoingia madarakani watu wanaanza kujadili atakapotoka nani ataingia!.Hiyo ilikuwa kwenye awamu ya nne. Sasa awamu ya tano hoja za ajabu ni kuongeza kipindi cha uraisi! Nadhani Raisi amefanya vema kuliweka wazi hili jambo hivyo taifa liendelee na ajenda za maendeleo.Hoja za kujadili walau zingekuwa ni sera za awamu hii kuhusu sekta binafsi na umma na matokeo yake kwa taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja pamoja na kodi n.k. Ziwepo hoja za kusaidia kukuna vichwa na kufundishana na siyo kutetea kitumbua maana isije fika siku hata hicho kitumbua kikawa hakipo kiuhalisia bali kwenye majukwaa ya siasa tu.
 
Alikuwa wapi siku zote kukanusha kwa kutoa taarifa rasimi?
Alikuwa anapima upepo sasa kaona watu hawataki hiyo hadithi na hata kumuacha mpaka 2020 ni kwa vile ustaarabu umewajaa tuu, vingenevyo bungeni ingepelekwa hoja ya kutokuwa na imani na yeye na kupiga kura za siri kumng'oa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom