Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Anasema kamwe hatavunja Katiba.

Nashundwa kuelewa hapa..!
Kwani kuongeza mda wa urais ni kuvunja katiba? Japo kweli nisingependa aongeze mda lakini tukubaliane kuwa wanaisema hivo lengo la kwanza ni kuifanyia mabadiliko katiba ambapo itampa mamlaka ya kuendelea kugombea awamu nyingine na hapo ina maanisha hatokuwa amevunja katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi jamani mnadhan kuongeza muda wa urais ni jambo jepesi kwamba unalala tu unabadili katiba,..wapo watu ccm huko wameanza kupiga jaramba la kuutaka urais halafu uwaambie leo jamaa anaongeza muda sidhani kama hawatamuua mtu
 
Juma Nkamia ni mstaafu

Ally Kessy ni mstaafu

Jah people ameishia darasa la pili

Musukuma ameishia darasa la saba

Babu Tale ameishia madrassa.

Hawa hawawezi kumshawishi Dr Magufuli aongeze mihula.

Maendeleo hayana vyama!
Wewe jidanganye, wanaomwamini Magufuli ni madokta na Maprofesa, hao Ngulumbili uliowataja ni vibendera tu.
 
Nimeona clip sasa hivi kutoka M4C Magufuli akimwagiza Polepole awaambie watanzania kuwa hataki kusikia habari ya kuongeza muda wa urais. hataki mjadala huo kabisa. Anasema kamwe hatavunja Katiba.

TAZAMA:

View attachment 1697821

My take: Sidhani kama ni wa kumwamini!


Utamaduni wa kujipendekeza kwani nani kasema Mambo ya kuongezewa muda kama sio wenyewe haohao!. Wananchi wanakufa kwa Corona badala ya kuweka mikakati tunafikiria UJINGA
 
Hivi jamani mnadhan kuongeza muda wa urais ni jambo jepesi kwamba unalala tu unabadili katiba,..wapo watu ccm huko wameanza kupiga jaramba la kuutaka urais halafu uwaambie leo jamaa anaongeza muda sidhani kama hawatamuua mtu

Kwa huyu jamaa hakuna jambo jepesi kama hilo. Kama aliweza kupokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha mchana wa saba, huku jeshi likiwa limetengwa na mambo ya siasa, anashindwa nini kubadili katiba? Toka ameingia madarakani umewahi kuona uchaguzi wowote halali? Kwa huku kwetu Afrika jeshi likishakubali kutumiwa kisiasa, hakuna mtawala anashindwa kubadili katiba ili aendelee kukaa madarakani.
 
UJUE hiyo mijadala inamletea matusi mengi mno mtandaoni na amepata kujua vile WATANZANIA TULIVYOMCHOKA aliowapanga kutest mitambo wamekuja na furushi la matusi na sasa anawakana
 
Wewe msaulifu sana kwanza alisema kazi ya urais ni ngumu miaka mitano inatosha, baadaye akachukua fomu peke yake akamwekea mizengwe Membe asigombee, kwenye kampeni akadai kwa nini tunamnyima miaka mitano tena, akasahau alishasema kazi ya urais ni ngumu na miaka mitan inatosha.
Kikwete watu walisema sana ataongeza muda. Hakuongeza.

Na huyu asipoongeza mtasemaje?

Unataka kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hajalifanya bado?

Kwa kupiga ramli kwamba mwaka 2025 atafanya kosa hili?

Kama vile mtu hana makosa ambayo kayafanya tayari? Wakati anayo makosa kibao kashafanya?
 
Cha kushangaza wale wanaoshadadia aongezewe muda mbona hawakemei kama anavyofanya kwa mambo mengine yenye athari kwa Taifa.
 
Tunapoteza muda kujadili jambo ambalo mwenyewe kashasema halifanyi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom