Humphrey Polepole apinga chanjo ya Malaria, amesema haiaminiki

Kupitia ukurusa wake wa Twitter Humphrey Polepole amepinga chanjo ya Maralia iliyoidhinishwa na WHO kwa kusema kuwa haiaminiki na kuwataka walioitengeneza waseme inafanyaje kazi kwenye miili ya watu.
Chanjo hiyo imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa miaka kadhaa na WHO imeshauri nchi zinazokabiliana na ugonjwa huo kuanza kuitumia baada ya kuonyesha mafanikio makubwa katika hatua za majaribio.

Huyu ndugu Polepole huyu....

Huyu komredi mwenzetu huyu.....

Kiongozi wetu wa zamani ANATUSHANGAZA SANA....

Leo amekua mtaalamu wa CHANJO ,MADAWA NA UTABIBU?!!!

Hivi kweli DAWA...CHANJO zitengenezwe bila ya kuelezewa ZINAFANYA KAZI VIPI? Kweli jamani? Khaaa 😳😳🤣

Ndg.Polepole aache kuwahadaa wasiojua......

Ndg.Polepole aache siasa za kufikirika.......

#SiempreJMT
#NchiKwanza
 
Haya mambo yana GHARAMA kubwa sana.....

Ukikaa maskani , vijiwe vya kahawa ,ubanda ,midandamo ya Komoni ,mabaa utajua ni kwa kiasi gani kuna kundi kubwa la raia WANAENDELEA KUWA WAKALI NA KUIPINGA CHANJO YA UVIKO kwa kutumia nguvu kubwa na kwa jazba mno......sasa anaendelea kujitokeza ndg.Polepole na kutambaa MULEMULE.........

Daaaah inasikitisha sana
 
Amefumgua shule yake ya uongozi mtandaoni, usajiri ni keyboard yako tu unapewa madini ambayo hukuyapata chuo kikuuu.
Vijana wa ccm muungeni mikono amewatendea jambo jema maana anajua hamna skills za uongozi.
 
Kupitia ukurusa wake wa Twitter Humphrey Polepole amepinga chanjo ya Maralia iliyoidhinishwa na WHO kwa kusema kuwa haiaminiki na kuwataka walioitengeneza waseme inafanyaje kazi kwenye miili ya watu.
Chanjo hiyo imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa miaka kadhaa na WHO imeshauri nchi zinazokabiliana na ugonjwa huo kuanza kuitumia baada ya kuonyesha mafanikio makubwa katika hatua za majaribio.

Mzee kijana pingapinga
 
Mwenyewe simpingi tujiulize kwanin ulaya hakuna mbu Wala malaria kwanin wasilete hizo dawa za kuzuia kusiwe na mbu kabisa? Kuna shida pahali
 
Angekataa na vipimo pamoja na dawa zote za wazungu.
Hizi sasa ni sifa.
Hivi kwenye kadindano kakupimia malaria ingewekwa sumu ya kuua kimyakimya wangapi tungekuwa hai mpaka leo?
 
Alternative ni nini ?
Kuendelea na Vifo vya Ndugu zetu au Yeye anayo yake aipeleke ifanyiwe majaribio..

Wakati mwingine ni busara kuacha watu wafanye kazi zao.., Katika mchakato huu wa Malaria ni kipi kimekiukwa ? Sababu hata time frame ya uchunguzi ni ya muda mrefu
 
Nataka niwatengenezee maji ya machungwa na limao niwaambie ni chanjo ya HIV ili nipige hela kama babu wa loliondo najua hata serekali ikikataa mtajileta tu ugonjwa umekaa pabaya ule.
watakufunga tu labda kama una miliki jeshi.
 
Mwenyewe simpingi tujiulize kwanin ulaya hakuna mbu Wala malaria kwanin wasilete hizo dawa za kuzuia kusiwe na mbu kabisa? Kuna shida pahali
na wewe unashindwa kuelewa tu suala la hali ya hewa pamoja na mazingira yanayotutofautisha sisi na wao kuwa ndiyo sababu hasa.
 
Back
Top Bottom