Huku ni kufukua makaburi au ni kujipaka matope?

Ni kwa matumizi ya serikali.

PM anajifaragua tu huyu. Utaratibu wa kununua hayo magari huanza na kuomba kibali toka ofisi ya waziri mkuu kupitia TAMISEMI. Kwahiyo hapo PM anajikosha tu.
Ila ngoja Uchunguzi ufanyike alafu tupewe report ndiyo tutajua nani mkweli kati ya PM na Wakurugenzi!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kitu ninachokidhania ni kwamba aidha Majaliwa aina shida ya kujiamini katika nafasi aliyonayo kwa maana nafasi ya uwaziri mkuu imekuwa kubwa kwake au ana uzembe wa kufikiri/kuchambua mambo kama ofisi yake inahusika na suala la manunuzi ya magari ya viongozi halafu order ya manunuzi ya gari ya mkurugenzi wa Geita inafika ofisini kwake kashindwa kuing'amua kama aina ya gari hiyo haipo kwa mkurugenzi, basi ofisi yake ina matatizo sana na huenda kukawa na ubadhirifu mkubwa sana.
 
Report ya Uchunguzi itabainisha kila Jambo,hata yale ambayo wengine tulikua hatuyajui tutayajuwa!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kitu usichokijua ni hii kauli ya kuwa mkuu wa kaya anafanya kila jambo, na wamekuwa wakimtuhumu kwamba amekuwa one man show,

Ki ukweli inawezekana katika office ya waziri mkuu ilipitisha haya magari lakini kwa kupitia wakasimu madaraka wa waziri hasa kwenye masuara ya ndani.

Pia nakumbuka haimashauli zilipangiwa kunukua magari nadhani yasiyozidi milioni 200 kama si 150 na ni zile toyota double cabin hilux sasa hawa wa kahama na geita wanafukuzana kununua magari hayo kwa faida ipi?

Nakumbuka kipindi cha kikwete watu walilalamika sana kuhusu magari ya bei kubwa, sasa iweje kwa mbana matumizi wewe ukanunue gari la bei kubwa lisilozalisha ni mapato tena ambalo haliwezi kusaidia hata kubeba madawa kupeleka kwenye kituo cha afya?

Hao kama wanadhami wao ni special sana basi watumbuliwe tu. Niliona gari la mkuu wa mkoa wa mara baada ya ile ya zamani kupata ajari wakamletea plado sas iweje mkurugeni atembee na ya 400 au 270 wakati mkuu wa mkoa ana ya chini ya 200? Nasema hao watumbuliwe tu kwa kuwa hawakutumia akiri kufikili.

Sasa wafanya biashara tunakamliwa pesa kisha mtu umekaa offisini na mshahara kutoka kwetu unalipwa kisha ujione bishoo wakati watu bado hawana maji?

Watumbuliwe tu waje tusaidiane kuzitafuta ili nao walipe kodi kwa kusumbua akiri.
Yalinunuliwa kwa kibali Cha Nani Kama sio huyo mnafiki waziri mkuu na ofisi yake?
Alikuwa wapi miaka yote asiyaone? Magari ni kitu kisichoonekana?
Wasitufanye watanzania wajinga kiasi hiki....
 
Nimemaliza shughuli zangu za kila siku kama ilivyo ada nimechukua gazeti la Mwananchi, nashangaa kukuta hii habari, Waziri mkuu wa nchi yetu ambae ni mkuu wa shughuli za serikali ametoa amri kuwa wakurugenzi walionunua magari ya Sh 270 wajieleze. Kwamba walitoa wapi pesa za kununulia hayo magari. Wakurugenzi hao ni wa halmashauri za Kahama, Chato, jiji la mwanza na Msalala.

Ghafla bin vuu nikakumbuka kuwa mkuu wa kaya mwenyewe aliwahi kukiri kuwa Watanzania sio wajinga na unapowaletea habari ambazo haziingii akilini watakaa kimya ila kumbuka watakuchora na kukusanifu kama katuni

Tujiulize kama watu wenye akili timamu, taratibu za kununua magari zikoje? Yaani mpaka hawa wakurugenzi wanaambiwa wajieleze,je hawakufuata taratibu?

Au ndio kuondoa aibu kisa tu Mkurugenzi wa Geita alisimamishwa kimakosa? Na hii ni baada ya wananchi kuona kuwa mkurugenzi hawezi kununua gari kwa maamuzi yake!

Kwa nini hii habari ya kuhoji gharama za magari ya wakurugenzi iwe sasa awamu hii tunapoenda kumaliza ngwe ya pili? Hapo mwanzo mbona ilikuwa kimya? Na tuliona karibu kila halmashauri zina Vx v8 yenye thamani zaidi mil 270!

Je, huku ni kujipaka matope au ndio kufukua makaburi?
381F997C-7486-4E03-BF8E-F80EE527E44F.jpeg

Kwa kweli hata kwetu huku CCM, tunahitaji maelezo!
Chama chetu cha wanyonge.
 
Nani aliruhusu watumie pesa vibaya?
Mawazo yao wenyewe na kwa sababu serikari iliweka mwongozo kwa magari kila idara.
Kwa sababu maombi ni mahitaji yao kwenye haliamashauli zao.
Sasa kama geita bado sehemu kubwa ni njia za vumbi hilo gari ni kuongeza matumizi ya vipuri na kuongeza hasara kwa serikari ukizingatia vipuri vyake ni bei ghari.
 
Yalinunuliwa kwa kibali Cha Nani Kama sio huyo mnafiki waziri mkuu na ofisi yake?
Alikuwa wapi miaka yote asiyaone? Magari ni kitu kisichoonekana?
Wasitufanye watanzania wajinga kiasi hiki....
Yalinunuliwa kkwa kulingana na wao kuyahitaji pia ofisi zilizotumika inawezekana kupitisha maombi yao huenda walihongwa au walidanganywa na kupitisha kitu kisichokuwa sahihi,
Hoja inarudi kwamba endapo huyo mkurugenzi angeomba gari la milioni 100 akalazimishwa kupewa la mia nne hiyo isingekuwa shida kwake. Lakini aliomba mwenyewe na kwa faida yake mwenyewe, maana suo gari hata ya kubebe wagonjwa au mizigo.

Tatizo kwa akiri yake huo mkurugenzi aliona huko geita au tanzania shida zimeisha sasa ni wakati wa kutmia pesa?

Lazima tukatae upuuzi, hilo gari litatumika mwaka mmoja wanalihalibu kisha linauzwa kwa milioni 20, sasa hiyo si ni diri na uhalifu kwa mali za nchi?
 
Mkuu huwezi endeleza biashara inayokutia hasara, hivyohivyo huwezi endalea tumia haya madude aka mav8 yanatia taifa hasara.
Nini kifanyike,
Serikali itengeneze how room, iyakusanye yote, na kuyaweka hapo chini ya uratibu mahalum,yatangazwe ndani na katika ukanda unaotuzunguka na Bei zake yauzwe Mara moja,tz ipo tahasis ya takukuru hutumia gari za kawaida Sana sio kwamba nikutokana na kazi zao tu bali wanajitambua,hutumia mpaka suzuki jimny, so wengine wanashindwa nini kutumia,anaetaka gari nzuri anunue mwenyewe , ofisi inaweza kia na gari moja KWA kazi mahalum zingine zikawa za kawaida Sasa Hapa kwetu unakuta wizara moja Yani top ten wote kila mmoja ana dude hili,why
Napendekeza wizara zenye uhitaji mahalum ndo zimiliki mav8 na yasizidi matatu
Kilimo,ujenzi, viwanda na biashara,plus
Kila mkoa liwepo limoja kwa kazi mahalum, basi mwingine yakusanywe anaelitaka akanunue mwenyewe

Haya yanayotumiwa na wakuu wa wilaya na wakurugenzi yatapelekwa wapi? na kwa nini iwe sasa hivi?
 
Hapo anatafutwa mbuzi wa kafara tuu....walioganya makosa ndo wakati wao wa kujisafisha
 
Kitu usichokijua ni hii kauli ya kuwa mkuu wa kaya anafanya kila jambo, na wamekuwa wakimtuhumu kwamba amekuwa one man show,

Ki ukweli inawezekana katika office ya waziri mkuu ilipitisha haya magari lakini kwa kupitia wakasimu madaraka wa waziri hasa kwenye masuara ya ndani.

Pia nakumbuka haimashauli zilipangiwa kunukua magari nadhani yasiyozidi milioni 200 kama si 150 na ni zile toyota double cabin hilux sasa hawa wa kahama na geita wanafukuzana kununua magari hayo kwa faida ipi?

Nakumbuka kipindi cha kikwete watu walilalamika sana kuhusu magari ya bei kubwa, sasa iweje kwa mbana matumizi wewe ukanunue gari la bei kubwa lisilozalisha ni mapato tena ambalo haliwezi kusaidia hata kubeba madawa kupeleka kwenye kituo cha afya?

Hao kama wanadhami wao ni special sana basi watumbuliwe tu. Niliona gari la mkuu wa mkoa wa mara baada ya ile ya zamani kupata ajari wakamletea plado sas iweje mkurugeni atembee na ya 400 au 270 wakati mkuu wa mkoa ana ya chini ya 200? Nasema hao watumbuliwe tu kwa kuwa hawakutumia akiri kufikili.

Sasa wafanya biashara tunakamliwa pesa kisha mtu umekaa offisini na mshahara kutoka kwetu unalipwa kisha ujione bishoo wakati watu bado hawana maji?

Watumbuliwe tu waje tusaidiane kuzitafuta ili nao walipe kodi kwa kusumbua akiri.
Magari ya kifahari kwa serikali na CCM yamekuwa mengi mno,gharama za kuyanunua na kuyahudumia ni,mzigo mkubwa sana kwa wanyonge wanaokamuliwa hadi damu zinawatoka.
Wanyonge wanaotawaliwa na watawala wapenda misifa kwa gharama za wanyonge.
Watanzania, tudai Katiba ya Wananchi ili tuanze upya kwa kuweka misingi ya nchi tunayoitaka.
 
Hakuna haja ya Katiba kila Mtu ajitafakari na awe na hofu ya Mungu,kumiliki vitu vya kifahari hakukufanya kutokua Kama Binaadamu wengine, Maisha ni haya haya, wote tuishi kwa Upendo na Amani mengine yatakuja yenyewe!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nimemaliza shughuli zangu za kila siku kama ilivyo ada nimechukua gazeti la Mwananchi, nashangaa kukuta hii habari, Waziri mkuu wa nchi yetu ambae ni mkuu wa shughuli za serikali ametoa amri kuwa wakurugenzi walionunua magari ya Sh 270 wajieleze. Kwamba walitoa wapi pesa za kununulia hayo magari. Wakurugenzi hao ni wa halmashauri za Kahama, Chato, jiji la mwanza na Msalala.

Ghafla bin vuu nikakumbuka kuwa mkuu wa kaya mwenyewe aliwahi kukiri kuwa Watanzania sio wajinga na unapowaletea habari ambazo haziingii akilini watakaa kimya ila kumbuka watakuchora na kukusanifu kama katuni

Tujiulize kama watu wenye akili timamu, taratibu za kununua magari zikoje? Yaani mpaka hawa wakurugenzi wanaambiwa wajieleze,je hawakufuata taratibu?

Au ndio kuondoa aibu kisa tu Mkurugenzi wa Geita alisimamishwa kimakosa? Na hii ni baada ya wananchi kuona kuwa mkurugenzi hawezi kununua gari kwa maamuzi yake!

Kwa nini hii habari ya kuhoji gharama za magari ya wakurugenzi iwe sasa awamu hii tunapoenda kumaliza ngwe ya pili? Hapo mwanzo mbona ilikuwa kimya? Na tuliona karibu kila halmashauri zina Vx v8 yenye thamani zaidi mil 270!

Je, huku ni kujipaka matope au ndio kufukua makaburi?
Alitakiwa amuhoji Mwenyekiti wa chama kuhusu ununuzi V8 za CCM tulizokuwa tunaziona wakati wa kampeni
 
Kununua GARI LA MIL 270 iwe ishu LAKIN KUNUA NDEGE bila kufuata UTARATIBU sio ishu.
KILA KONA NI UPUMBAVU.
 
Ni hivi, waziri Mkuu ajue hatudanganyiki na kiki za bei rahisi. Hakuna mwizi wa kura ambaye ni muadilifu.
 
Back
Top Bottom