Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,085
- 6,564
Nimemaliza shughuli zangu za kila siku kama ilivyo ada nimechukua gazeti la Mwananchi, nashangaa kukuta hii habari, Waziri mkuu wa nchi yetu ambae ni mkuu wa shughuli za serikali ametoa amri kuwa wakurugenzi walionunua magari ya Sh 270 wajieleze. Kwamba walitoa wapi pesa za kununulia hayo magari. Wakurugenzi hao ni wa halmashauri za Kahama, Chato, jiji la mwanza na Msalala.
Ghafla bin vuu nikakumbuka kuwa mkuu wa kaya mwenyewe aliwahi kukiri kuwa Watanzania sio wajinga na unapowaletea habari ambazo haziingii akilini watakaa kimya ila kumbuka watakuchora na kukusanifu kama katuni
Tujiulize kama watu wenye akili timamu, taratibu za kununua magari zikoje? Yaani mpaka hawa wakurugenzi wanaambiwa wajieleze,je hawakufuata taratibu?
Au ndio kuondoa aibu kisa tu Mkurugenzi wa Geita alisimamishwa kimakosa? Na hii ni baada ya wananchi kuona kuwa mkurugenzi hawezi kununua gari kwa maamuzi yake!
Kwa nini hii habari ya kuhoji gharama za magari ya wakurugenzi iwe sasa awamu hii tunapoenda kumaliza ngwe ya pili? Hapo mwanzo mbona ilikuwa kimya? Na tuliona karibu kila halmashauri zina Vx v8 yenye thamani zaidi mil 270!
Je, huku ni kujipaka matope au ndio kufukua makaburi?