Huku Ndio Kusherehekea Muungano?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huku Ndio Kusherehekea Muungano??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabaDesi, Apr 26, 2009.

 1. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ninaangalia maadhimisho ya sherehe za Muungano yanayoonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV. Mvua inanyesha. Watoto waliokuwa wakionyesha michezo ya halaiki wamemaliza michezo yao na badala ya kutolewa kiwanjani, wamekalishwa chini kwenye uwanja uliojaa maji huku mvua ikiendelea kunyesha, waheshimiwa wakiwa wamekaa jukwaani wakiangalia ngoma. umri wa wengi wa watoto hawa ni chini ya miaka 16. Hivi hakuna kiongozi yoyote mwenye busara anayeweza kutoa amri watoto wale wanyanyuliwe pale walipo na wakajibanze banze sehemu nyingine badala ya kukaa chini ambapo pameloa chapa chapa?? Huku ndio kuwajali watoto wetu?? Huku ndio kusherehekea Muungano?? Imeniuma sana.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Ukiuliza utaambiwa wale ni wanajesshi wamejiandaa kwa hali yeyote mvua na jua....kwanza hawana sehemu ya kukaa maana wako 1000...na uwanja umeshajaa pomoni...
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  BabaDesi heshima mbele mkuu, hiyo ndiyo hulka ya viongozi wetu kujifikiria interests zao kwanza halafu watu wengine baadae; hata wakiwa watoto!!
   
  Last edited: Apr 26, 2009
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Inawezekana, Skills. lakini angalau basi wangeambiwa wasimame tu kuliko kukaa chini kwenye uwanja uliojaa maji. ama angalau basi wangeambiwa tu watawanyike maana shughuli yao iliishakwisha. Naamini wengi wangekimbilia nyuma ya jukwaa la kijani ambalo sijui siku hizi linaitwa nini!!
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  indirect harzadous works for children, ILO mko wapi?
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hata mimi kile kitendo kilinichukiza, nikafikiri labda ni mimi tu.
  Zaidi ya hapo uwanja ulikuwa umejaa wageni waalikwa kutoka kila kona ya dunia, sasa sijui tumejenga picha gani pale.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kwa nini kila siku sherehe kubwa za Muungano zinafanywa DAR?

  No wonder wenyewe kule ZANZIBAR hawautaki huu muungano
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Hata mimi kile kitendo kilinichukiza, nikafikiri labda ni mimi tu.
  Zaidi ya hapo uwanja ulikuwa umejaa wageni waalikwa kutoka kila kona ya dunia, sasa sijui tumejenga picha gani pale."
  __________________

  Kang:

  Mvua ilipozidi kuendelea huku watoto wamekaa chini, kwa kwa nini JK, kama Amiri Jeshi Mkuu asitoe agizo la kusitisha shughuli ile iliyobakia (ile ya ngoma) ili kuwanusuru watoto? Hivi kweli mtu huyu ana huruma ya viumbe hawa? Inavyoonekana huruma yake kubwa huionyesha kwa mafisadi tu siyo kwa binadamu wengine.
   
 9. O

  Oganga New Member

  #9
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba Desi,

  Muungano ndio huo kama ulikuwa haujui! Lakini cha msingi siyo watoto kulowa maji au kutokulowa maji, cha msingi ni Je, wanauthamini Muungano wenyewe?Wanaufahamu au tunawapeleka puta bila kuwaeleza umuhimu na thamani ya Muungano.

  Ahsante kwa kujali watoto wa Kitanzania.
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wanasheherekea muungano hewa.
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mambo ya kuwakalisha watoto kwenye mmvua yasingetokea hii sherehe ingefanyika Zanzibar
   
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Mkuu GT, una maana gani?
   
 13. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kweli bongo kazi ipo!, ufisadi ukipigiwa kelele wanalalamika unaharibu sifa ya Tanzania ulimwenguni. Sasa hao watoto waliokalishwa kwenye mvua hicho kitendo hakiharibu sifa ya Tanzania kwa hao viongozi waliokuja kushiriki. Very sad.
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwani waandahaji wa hilo tamasha, hawakujuwa kuwa kutakuwa na mvua?

  Sasa hao watoto maskini ya Mungu wakipata ugonjwa wa Pneumonia, litakuwa jukumu la nani kama si mzazi!?

  Si kazi vitoto vingine hapo vina matatizo ya ugonjwa wa Ngiri tayari (
  Hernia).

  sidhani hata hao walio waandaa/kuwataarisha kama watawasaidia kwa hilo.
   
  Last edited: Apr 27, 2009
Loading...