Huku nchini Peru na mifuko ya we plastiki

Huku nchini Peru na mifuko ya we plastiki

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,353
Huku Peru kuanzia watoto hufundishwa shuleni umuhimu wa kutunza mazingira. Hii mifuko ya plastic hawaitaki lakini wanajuasolution ni step by step;

2014 ilikuja policy ya kusema dukani unanunua mfuko sh 500, wakati zamani ilitolewa bure. Hii imefanya tukumbuke mifuko kila tukienda madukani.

Kuna maduka yameacha kutumia mifuko ya plastic, mengine bado yanaendelea na hakuna fine.

Wana mpango wa kuanzisha utaratibu wa kurudisha makopo ya bia na soda dukani ili upate bia au soda ya bonas.

Hii sheria ya jela siku saba kwa kumiliki au kutumia mfumo wa plastic itafunga wengi sana.
 
Hivi kuna kifungo?. Mimi najua ni faini tu mkuu
*FAHAMU MAKOSA NA ADHABU ZITOLEWAZO NA SHERIA ZINAZOKATAZA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI TANZANIA*

*By Omari Kilwanda-Wakili*

Kimsingi kuna *Makosa Makuu Matano* yaliyotajwa na kukatazwa ndani ya Sheria husika. Sheria hiyo Ndogo inajulikana kama *The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019*. Sheria hii Ndogo imetungwa kwa Mujibu wa Kifungu Na. 230 (2) (f) cha Sheria inayojihusisha na Usimamizi wa Mazingira *(The Environmental Management Act, Cap. 191)*.

*A: MAKOSA*
Kwa mujibu wa Kifungu/Kanuni Na. 8 Cha Sheria ya Kuzuia Matumizi ya Mifuko ya Plastiki ambayo ni *The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019* kuna Makosa Matano ambayo ni;
(A). Kuzalisha na Kuagiza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 a )*;
(B). Kusafirisha nje ya nchi Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 b )*;
(C). Kuhifadhi na Kusambaza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 c )*;
(D). Kuuza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 d )*;
(E). Kumiliki na Kutumia Mifuko ya Plastiki? *(Kifungu/Kanuni Na. 8 e )*.

*B: ADHABU*
Kwa kila kosa tajwa hapo juu, Sheria husika imetaja Adhabu yake. Hivyo basi kuna Adhabu aina tano kama ilivyo kwa Makosa husika. Kifungu/Kanuni Na. 8 cha Sheria tajwa hapo kilichotaja Makosa Matano ndicho hicho kimetaja Adhabu ya kila Kosa kama ifuatavyo;

(A). *Adhabu kwa Wazalishaji na Waagizaji.*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (a) cha Sheria tajwa hapo juu, kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 20 na isiyozidi Billioni 1*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miaka Miwili*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(B). Adhabu kwa Wasafirishaji kwenda nje ya nchi.*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (b) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 5 na isiyozidi Milioni 20*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miaka 2*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(C). Adhabu kwa Wanaohifadhi na Wasambazaji*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (c) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 5 na isiyozidi Milioni 50*,
ii. Kifungo Kisichozidi Miaka 2,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(D). Adhabu kwa Wauuzaji*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (d) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Laki 1 na isiyozidi Laki 5*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miezi 3*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(E). Adhabu kwa Watumiaji na Wanaomiliki*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (e) cha Sheria tajwa hapo kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Elfu 30 na isiyozidi Laki 2*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Siku 7*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo.
 
Nadhani Mh Makamba hawajakaa pamoja na Mh Ummy kwa sababu kuna mfuko mmoja pendwa sana unaotumika mara moja tu. Ndomu. Je, huu itakaa vipi tutakapo kutwa nao ndani ya pochi kama zana imara??
 
Kuna sheria zinatungwa kwa kukurupuka. Sina uhakika kama mifuko mbadala imeshafika mujini.
 
huko peru wametumia akili zaidi kuliko nguvu, huku kwetu serikalini kuna akina bashite na kabudi sasa matokeo yake ndio haya, wanaamini katika vitisho na faini kubwakubwa 'ili iwe fundisho' kwa wengine.
 
Kuna kifungo cha siku saba kumiliki au kutumia mfumo wa plastic
Tatizo kubwa la nchi yetu ni kukurupuka. Mtu anaamka asubuhi anatunga sheria na mchana anasema kuanzia kesho au mwezi ujao ni marufuku hiki na hiki. Kwa nini tusijiandae kwa kujipa muda na kutafuta mbadala wa hiyo mifuko ya plastiki? Au kwanini tusitafute njia za ku-discourage matumizi makubwa na yasiyo na lazima ya hii mifuko? Kama hili la kutoza kodi kubwa kwenye mifuko inayozalishwa au kuingizwa nchini ingekuwa option nzuri sana. Mfuko 1 ukiuzwa sh hata elfu au elfu mbili kutawafanya watu wa-re-cycle mifuko badala ya kuitupa hovyo. Pia wanaweza kuweka sheria mifuko ya plastic inayotumika iwe ile migumu na mizito ambayo inaweza kutumika mara nyingi.
 
Kuna sheria zinatungwa kwa kukurupuka. Sina uhakika kama mifuko mbadala imeshafika mujini.
Unashangaa wakati imeshaanza kutengenezwa hapa hapa bongo na mingine inaletwa kutoka nchi za nje na tayari ipo madukani na watu wameshaanza kuitumia.
 
Tatizo kubwa la nchi yetu ni kukurupuka. Mtu anaamka asubuhi anatunga sheria na mchana anasema kuanzia kesho au mwezi ujao ni marufuku hiki na hiki. Kwa nini tusijiandae kwa kujipa muda na kutafuta mbadala wa hiyo mifuko ya plastiki? Au kwanini tusitafute njia za ku-discourage matumizi makubwa na yasiyo na lazima ya hii mifuko? Kama hili la kutoza kodi kubwa kwenye mifuko inayozalishwa au kuingizwa nchini ingekuwa option nzuri sana. Mfuko 1 ukiuzwa sh hata elfu au elfu mbili kutawafanya watu wa-re-cycle mifuko badala ya kuitupa hovyo. Pia wanaweza kuweka sheria mifuko ya plastic inayotumika iwe ile migumu na mizito ambayo inaweza kutumika mara nyingi.
Mkuu wewe hufuatiliagi matangazo ya serikali, hili suala walilitangaza tangu mwaka 2017 isipokua wafanyabiashara na wenye viwanda wamekua wakiomba kuongezewa muda, wakawa wanapewa miezi sita mara wanaomba tena wanapewa, sasa serikali imeamua mwisho tarehe moja.
 
Serikali imejiandaaje huo muda wote kama ni kweli? Halafu kama walikuwa wanaongezewa muda ni kosa kubwa. Kwa kiongozi aliye makini anasema eg baada ya mwaka mmoja na nusu kuanzia siku fulani ni mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastic. Kipindi hichi cha mpito zinatafutwa njia nyingine mbadala za ku-replace hiyo mifuko.
 
Back
Top Bottom