Huko maziwani mwaka huu kuna nini?

Huko maziwani mwaka huu kuna nini?

Wakuu Habari,

Siku za hivi karibuni tumesikia ziwa victoria liliongezeka kina cha maji na kupelekea maji kujaa(maafuriko) kwenye makazi ya watu. Ikumbukwe makazi ya watu yalikuwa zaidi ya mita 100 kutokea usawa wa ziwa.

Sasa hivi nasikiliza habari hapa, wanadai ziwa Tanganyika huko maji yameongezeka na kupelekea mafuriko kwenye makazi ya watu hali ambayo haijatokea kwa zaidi ya miaka 60

Sasa najiuliza, hii hali inatokana na nini? Kwanini mwaka huu ni maziwa yote?

Kuna nini huko maziwani mwaka huu?

Bado kuna taarifa nyingine kuwa ziwa Nyasa nalo lina daliliView attachment 1459614View attachment 1459615

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni mvua mkuu, zimekuwa nyingi kuliko kawaida
 
Duh ivi hayo makazi itakuaje kwamfano hayo maji yakaamua kufanya makazi yakudumu hapo yani ikawa ndo forever hayapungui zaidi yakuongezeka
 
Wajerumani wa mwanzo waliotia nanga Ziwa Nyanza baada ya kufanya tafiti waligundua Ziwa hilo miaka takribani 500-350 halikuwa walipolikuta bali lilipungua (Kusogea).

Kuthibitisha hilo ni pale uwapo katika miji mikubwa inayozunguka Ziwa Nyanza, Mwanza na Bukoba utagundua bonde la miji hii linatitia huku mchanga wa Ziwa ikichukua nafasi.

Pia ujenzi wa kale wa Mjerumani alilenga zaidi kujenga milimani, mfano;- Chamber Deutsche Stag (Ofisi za Chamber, Manispaa ya Bukoba), Armore Pillas (Field Force Unity Base 1).

Chanzo: Kitukuu cha Mmoja wa Mjerumani na tafiti yangu mwenyewe.
 
Mkuu ukiona mtu wa dini dini anajenga safina tushtuane aiseee.
Maana hali inavyoelekea yale majanga ya wakati wa Nuhu kama yanataka kujirudia kwa kweli.
 
Wajerumani wa mwanzo waliotia nanga Ziwa Nyanza baada ya kufanya tafiti waligundua Ziwa hilo miaka takribani 500-350 halikuwa walipolikuta bali lilipungua (Kusogea).

Kuthibitisha hilo ni pale uwapo katika miji mikubwa inayozunguka Ziwa Nyanza, Mwanza na Bukoba utagundua bonde la miji hii linatitia huku mchanga wa Ziwa ikichukua nafasi.

Pia ujenzi wa kale wa Mjerumani alilenga zaidi kujenga milimani, mfano;- Chamber Deutsche Stag (Ofisi za Chamber, Manispaa ya Bukoba), Armore Pillas (Field Force Unity Base 1).

Chanzo: Kitukuu cha Mmoja wa Mjerumani na tafiti yangu mwenyewe.
Ook Ahsante kwa history swaf kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom