Huko maziwani mwaka huu kuna nini?

Huko maziwani mwaka huu kuna nini?

RtsHjcq

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2017
Posts
4,753
Reaction score
5,516
Wakuu Habari,

Siku za hivi karibuni tumesikia ziwa victoria liliongezeka kina cha maji na kupelekea maji kujaa(maafuriko) kwenye makazi ya watu. Ikumbukwe makazi ya watu yalikuwa zaidi ya mita 100 kutokea usawa wa ziwa.


Sasa hivi nasikiliza habari hapa, wanadai ziwa Tanganyika huko maji yameongezeka na kupelekea mafuriko kwenye makazi ya watu hali ambayo haijatokea kwa zaidi ya miaka 60

Sasa najiuliza, hii hali inatokana na nini? Kwanini mwaka huu ni maziwa yote?

Kuna nini huko maziwani mwaka huu?

Bado kuna taarifa nyingine kuwa ziwa Nyasa nalo lina dalili
FB_IMG_1590430477896.jpeg
FB_IMG_1590430425555.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom