Baba mtakatifu91
JF-Expert Member
- Apr 25, 2026
- 3,270
- 6,719
Umuofia kwenu natumai mmekuwa na wakati mzuri sana.
Soma na hii pia itakusaidia pia
Chungu kimoja kilikuwa na mitumbwi mingi ufuoni. Kila mtumbwi ulikuwa na jina lake. Lakini kuna mtumbwi mmoja uliokuwa hauna mti mzima, ulichongwa kwenye gogo lenye vijiti vidogo na manyanyinyi. Watu walipouliza, "Huu mtumbwi wa nini?" wakasema, "Huu ni mtumbwi wa vibwengo."
Siku moja, wakaja wasomi na wanazuoni wenye Phd dhahania.Wakasema, "Tutavuka ziwa kwa laws za Physics fundi akaona isiwe nongwa akawapa mtumbwi wa vibwengo. Wakapiga makasia, wakafika katikati. Wakagundua mbao zina vishindo, maji yanaingia. Waliporudi, wakasema, "Huu mtumbwi hautuachi salama." Fundi akawajibu lakini niliwaonya hamkusikia
Kisha wakaja wafanyabiashara wa pupa. Wakasema, "Tunataka kusafirisha mizigo yetu." Wakapewa mtumbwi huo huo. Wakapakia mazao, wakapiga safari. Nusu ya maji waliikuta mizigo imezama. Wakasema, "Huu mtumbwi una wizi ndani yake." Wakajibiwa, "La, anayekuwa ndani ndiye mwizi. Mtumbwi ni vibwengo."
Kisha wakaja wala bata. Wakasema, "Sisi tunataka tu kuelea na kuimba." Wakapewa mtumbwi wa vibwengo. Wakaelea, wakaimba, wakacheka. Lakini kila wakicheka, mtumbwi uliyumba zaidi. Wakapiga kelele, "Eti huu ni mtumbwi wa kusherehekea?" Wakajibiwa, "La, huu ni mtumbwi wa kujifurahisha mpaka kuzama."
Mvua ikanyesha. Wakaja viongozi waliochaguliwa kwackura turufu. Wakasema, "Sisi tunajua kuzungumza na mvua, tutaikata." Wakapanda mtumbwi wa vibwengo, wakaanza kuparamia maongezi: "Ee mvua, shuka taratibu! Ee pepo, piga hapa si pale!" Lakini mvua haikawii kujibu: ilinyesha tu hadi mtumbwi ukajaa. Wakaogelea wenyewe, wakiacha sauti zao zimezama kwenye kina.
Kisha wakaja vijana wapenda single mother na mishangazi. Wakawaona wanawake wamechoka, wamebeba mizigo ya watoto na maisha. Wakasema, "Sisi hatutaparamia tu, tutaoa." Wakapanda mtumbwi, wakawapa pete na ahadi. Wakasema, "Tunawapenda kwa dhati." Lakini walipofika katikati ya ziwa, wakagundua hawana nyumba, hawana kazi, hawana subira ya kulea watoto wa wengine. Wakaanza kulaumiana. Vijana wakasema, "Umewachoka." Akina mama wakasema, "Ulijua mimi na mizigo yangu." Mtumbwi ukayumba zaidi. Maji yakaingia. Wadau wote wakazama pamoja, wakiacha watoto wakiwa wamebaki ufukweni wakiwalilia.
Hatimaye, wakaja watu wanaoenda kwa wachungaji matapeli. Hawakuja na shoka wala nanga. Walikuja na chupa tupu na mioyo iliyochoka kuzama. Wakasema, "Tumesikia kuna wachungaji wanaoweza kuziba mtumbwi kwa miujiza ya mafuta na maji. Tuende kwao."
Wakawafuata wale wanaojiita watumishi wa Mungu.Wachungaji wakawakaribisha kwenye mtumbwi wa vibwengo. Wakasema, "Ninayo maji ya kutuliza mawimbi. Ninayo mafuta ya kuziba uwazi." Watu wakafurahi. Wakatoa fedha zao. Wakatoa imani yao. Wakapata mafuta, wakapaka vipaji vya nyuso zao. Wakapata maji, wakanyunyiza pembe zote za mtumbwi.
Maji ya upako hayakufua dafu.Mtumbwi uliendelea kuyumba, maji yakaendelea kuingia. Wakamwuliza yule chungaji, "Mbona bado tunazama?" Akasema, "Hamkuwa na imani ya kutosha. Leteni zaidi. Mafuta mengine, fedha nyingine." Wakaleta tena. Wakapaka tena. Wakanyunyiza tena. Mtumbwi ukazama zaidi.
Wakamwuliza tena. Akasema, "Wachawi wamezidi. Niombeeni usiku kucha. Lakini kwanza, changia sadaka ya usiku." Wakachangia. Wakasali. Wakalia. Wakapaka mafuta hadi wanenepea. Wakanyunyiza maji hadi kuogea. Lakini asubuhi, mtumbwi ulibakiza kiwiko tu juu ya maji. Na wachungaji walikuwa wameshuka zamani. Walikuwa wamekwenda ufukweni mwingine, wakiwatafuta wateja wengine wenye chupa tupu.
Waliobakia mtumbwini wakasema, "Yamkini hatukuomba vya kutosha. Yamkini hatukupaka kwenye sehemu sahihi." Wakaanza kulaumiana. Lakini hakuna aliyesema, "Labda huyu mchungaji ni tapeli." Waliogopa kusema ukweli, kwa maana ukweli hauna kanzu ndefu wala sauti kubwa.
Mwisho, mtumbwi ule ukazama. Watu wakazama wakiwa wameshikilia chupa za mafuta tupu na vyungu vya maji ya udongo. Wachungaji matapeli wakajenga makanisa mapya ufukweni, wakasema, "Wale walizama kwa sababu ya imani ndogo. Lakini sisi tumebaki, sisi ndio waaminifu."
Na watu wengi wakaendelea kuwafuata. Wakaendelea kununua mafuta. Wakaendelea kukusanya maji. Wakaendelea kuzama. Kwa maana ni rahisi kununua mafuta kuliko kuchonga shoka.
Makinika!!