barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Watu wasiojulikana wamechanganya maji na mafuta kwenye mashine ya kupandisha na kushushia vitu vizito inayotumika kubomoa jingo la shirika la umeme Tanzania (Tanesco).
Hatua hiyo ndiyo inayosababisha kazi ya ubomoaji wa jingo hilo kutokamilika ndani ya muda uliopangwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa majengo Tanzania (TBA). Elius Mwakalinga, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na tulipata kufahamu sababu zilizofanya kutokamilika kwa wakati ubomoaji wa jingo la Tanesco.
“Mashine hiyo ilikuwa na matatizo, wakairekebisha… yaani mtu anatoka huko anaweka maji kama plastiki mbili hivi kwenye mafuta. “Walitoa maji hayo, wakasafisha, wakarudisha pampu, kreni imeanza kufanya kazi, nilikuwa safarini na niliporudi ndiyo nikakutana na hizo taarifa,” alisema.
“Ubomoaji utakamilika baada ya siku 10 kutoka sasa. Leo wanaendelea na ubomoaji.”
Alisema kwa sasa TBA kwa kushirikiana na mwenye mashine hiyo wanafanya uchunguzi, ili kuwabaini watu waliohusika na kitendo hicho.
Mwakalinga alisema kazi ya kubomoa jingo hilo itakamilika baada ya siku 10 na kwamba siku nane zitakuwa za ubomoaji na ssiku mbili zitakuwa za kubeba kifusi.
Agizo la ubomoaji wa jingo hilo lililotolewa na Rais John Magufuli Novemba 15, mwaka jana, alipowasili jijini Dar es salaam akitokea kijijini kwao Chato, mkoani Geita.
Rais Magufuli alimwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Ndyamukama Julius, kuvunja sehemu ya jingo la Tanesco na lile la Wizara ya Maji na Umwagiliaji, ili kupisha ujenzi wa barabara ya juu (flyover) ya Ubungo.
Rais Magufuli alisema sheria ya hifadhi ya barabara katika eneo la Ubungo ni mita 90 kila upande kutoka katikati ya barabara, hivyo ni lazima sheria hiyo iheshimiwe, ili kuharakisha ujenzi wa daraja la ghorofa tatu bila kikwanzo.