HUJUMA dhidi ya SLAA katika mdahalo wa JK leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HUJUMA dhidi ya SLAA katika mdahalo wa JK leo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by The Informer, Oct 29, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zanguni,


  Taarifa nilizopata leo ni kuwa 'mdahalo' utakaoneshwa na ITV leo usiku kuhusu mgombea Urais wa CCM Jakaya Kikwete, umeingiliwa na mafisadi kuhakikisha kuwa unakuwa ni mkutano wa kampeni badala ya mdahalo.

  Kwanza kabisa, jukumu la kualika waandishi wa habari na washiriki wengine halifanywi na waandaaji wa mdahalo huo (Rose Mwakitwange na Vox Media ya Ansbert Ngurumo) bali limepewa timu ya kampeni ya Kikwete.

  Sielewi kwa nini waandaji wa mdahalo huu wameruhusu uhuni huu haswa ikizingatikwa kuwa Ngurumo yupo kwenye campaign team by Dk. WILLIBROD SLAA wa Chadema.

  Waandishi watakaoalikwa kwenye mdahalo huo ni wale tu waliokuwepo kwenye kampeni ya Kikwete. Waandishi hawa ndiyo wale walikuwa wanalipwa posho ya shilingi laki 1 kila siku na CCM na kuvishwa nguo zimeandikwa "KIKWETE PRESS."

  Taarifa nilizopata ni kuwa tayari campaign team ya Kikwete, akiwemo Abdulrahman Kinana, January Makamba, Prince Bagenda na Muhingo Rweyemamu, wameandaa maswali ya kumbeba JK ambao waandishi hawa wamepewa waulize kwenye mdahalo.

  Waandishi hawa wamepewa maswali ya kumpamba Kikwete na kumponda SLAA kwenye mdahalo huo na tayari Kikwete ameandaliwa majibu ambayo atayasoma.

  Hivi sasa, mwandishi wa Tanzania Daima, anayeitwa IRENE MARK, ndiye amebeba bahasha kubwa yenye mialiko ya waandishi wa Kikwete watakao hudhuria mdahalo huu. Mwandishi huyu amepewa pesa azunguke newsroom zote na kugawa mialiko hiyo kwa "carefully selected journalists" ambao walikuwa kwenye kampeni za Kikwete.

  Cha ajabu mwandishi huyu yuko kwenye gazeti linalomilikiwa na Freeman Mbowe, mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA.

  Waandishi hawa wa Kikwete ambao tutawaona kwenye mdahalo leo usiku wamepanga kufanya party kubwa ambayo itafadhiliwa na CCM ili kujipongeza kwa mchango wao kwenye ushindi wanaotarajia wa Kikwete.

  Pia, CCM wamefanya hila makusudi ili mdahalo uliotia fora sana wa SLAA usirudiwe tena kwenye TV yeyote hapa nchini mpaka uchaguzi upite.

  Timu ya Kinana imewarubuni waandaaji wa mdahalo huu ili Kikwete awe mgombea wa mwisho kuzungumza kwenye TV leo ili ujumbe wake ubaki kwenye akili za Watanzania siku ya kupiga kura Jumapili.

  SWALI: Ngurumo wa Vox Media ambao wanaandaa mdahalo huu kwa nini anaruhusu hujuma hii yote dhidi ya SLAA?

  Naomba kuwasilisha...
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Tetesi or ?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Usiogope broda, kwani wewe unategemea kubadilika kwa maneno ya kusoma kwenye karatasi?
  Ukiona mbwembwe kwenye interview hiyo ujue kuwa ni HELA ZETU zinaendelea kutumika vibaya, kwahiyo pata HASIRA ZAIDI na kummaliza mtu 31/10.
  Sasa Party ya nini katika kipindi-tete kama hiki?
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama Kikwete ataweza kushawishi kama alivyofanya Slaa, after all watu wengi tayari wameshaamua nani wa kumpigia kura. Sana sana Kikwete atapunguza baadhi ya kura za watu makini ambao walikuwa hawana uhakika na uwezo wake
   
 5. T

  The Informer Senior Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni facts ambazo zitathibitishwa kwenye mdahalo wenyewe leo usiku.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu hili wala lisikutishe, end of the day ni JK ndiye atakuwa kizungumza nad he's completely not smart hata kama mtihani ni open book au anafahamu maswali tayari. Kwanza atakuwa na fake confidence na kutoka nje ya mada. Wait n see!
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Natumai Watanzania walishafanya maamuzi ya kumchua Dr. Slaa baada ya kuona rais tuliyenaye hana nia njema na maisha ya Watanzania wengi wanaoishi katika lindi la umaskini usioelezeka. Wacha wampe maswali na majibu yake lakini kwa mtu mwelewa na aliyefanya uamuzi wa nani wa kumpa kura yake atatambua ya kuwa hiyo ni danganya toto tu kwani baada ya uchaguzi ufisadi utaendelea kwa sana na maisha bora kwa kila mtanzania yataishia hapo kwani Kikwete anajua hatagombea tena. Kama ameweza kuwahifadhi mafisadi na kuwatetea majukwaani ili hali akijua anahitaji kura za waTZ kumrudisha madarakani itakuwaje sasa kwa kipindi hiki asichohitaji kura zetu tena? Watanzania wenzangu tusidanganyike na hila za CCM kwa namna yoyote ile.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,634
  Likes Received: 4,738
  Trophy Points: 280
  Kweli CCM wamefulia, hawa hasa ndiyo majuha kwani kwa kufanya hivyo ndiyo wanautangazia ulimwengu kuwa Kikwete ni kilaza hawezi kujitegemea yeye, naomba waendelee na huo upuuzi wao ili wammalizie kabisa huyo kilaza.
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mimi sitishwi na hilo
  kwanza nitashangaa kama umeme hautakatika
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Afadhali huu uchaguzi upite tuendelee na maisha mengine kama kawaida... nimechoka kabisa na mambo haya
   
 11. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #11
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  wala siangalii naweza vunja TV
   
 12. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu siiamini hii kitu, waandishi wa habari si watu waku nunuliwa kwa muda mrefu, wanajua kuwa kampeni imeisha na ujira wao washapata, mkataba kwisha, tegemea lolote lile leo.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwenye red: Katika swali lako hapo mwisho - sijaona ushiriki wa Ngurumo ktk mdahalo huu wa JK.
   
 14. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Aisee kwa hiyo Kiranja Mkuu sa'ivi yuko kwenye rehearsal...
   
 15. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  baada ya kulisikiliza mahojiano ya Power Breakfast na (out going) Rais Kikwete ya leo asubuhi, nina uhakika hataweza kuvuta watu!
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  watu tulishafanya maamuzi zamani sana
  sasa hivi tunapitia vituo ili tujue kama majina yetu yapo

  mbona Slaa ndo rais! wasikutishe kaka

  yule ni **** na punguani hawezi kuongoza nchi
   
 17. J

  Jafar JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  If God is on our side, who else ............
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Jk kumbukumbu atakazotuachia ni za kuwa hafai kuendelea kuwa Raisi na ya kuwa hana ushawishi wowote ule hivi sasa..................
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mkuu..,
  Achana na waandishi wahabari wa-Tanzania wanaendekeza njaa balaa..omba usikutane nao, trafiki nafuu..
   
 20. A

  Anold JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Hiyo ya kupanga waandishi waulize maswali maalum inaeleweka na nitashangaa kumuona mtu kama Ndg. Kubenea yupo kati ya hao walioalikwa. Ila tumsikikilize mgombea huyo tupime hoja zake na za wagombea wengine halafu tufanye majumuisho na kutoa hukumu ya haki siku ya kupiga kura. Kwangu mimi wagombea wote wanafaa ila lazima kuna anayefaa zaidi huyo ndiyo wa kumpigia kura.
   
Loading...